Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

  1. Unapoenda haja ndogo huku ukiamini kua umefungua zipu na kumbe hujaifungua,
  2. Unapoanza kuisahau njia ya kurudi nyumbani,
  3. Unapoanza kuwachanganya watoto wako kwa sura zao na majina yao.
  4. Unapoanza kula vidonge kama chakula chako badala ya chakula,
  5. Unapokua na appointment za Hospitali kila mara,
  6. Unapoanza kulala mapema na kuamka mapema,
  7. Unapoanza kuutambua umuhimu wa majirani zako,
  8. Unapoanza kuwakumbuka rafiki zako wa zamani na kuwathamini zaidi,
  9. Unapoanza kuachiwa Nyumba na watoto ili ukae nao pindi wahusika wanapotoka out,
  10. Unapoanza kuachiwa funguo na majirani.....
 
_Unapoanza kulimalima vibustani vya mboga mboga nyumbani.

_unapoanza kusuluhisha watu uonapo wanagombana/kupigana maana dalili ya ujana nikufurahia mabifu na kusema acha wanyooshane.

_kuanza kuvaa mabagi mkanda unavalia tumboni.

_kuanza kumind hata vitu vidogo mf mtu asipokusalimia shughuli anayo anaanza kusema hana nidhamu.

_kuanza kujali hata vitu visivyoeleweka mara ukiona kauchafu tu uwanja au kajani unakaokota na kwenda kutupa shimoni

Kuanza kupenda kuhudhulia kila sherehe na kupenda kupewa kauongozi hata kakugawa soda katika sherehe.

Kuanza kusahau mambo ya fashion ukienda kununua kitu mfano nguo hauangalii fashion ww unaangalia ugumu wa bidhaa.
JamiiForums-1500520960.jpg


Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Nimeanza utaratibu wa kuangalia taarifa za habari kila jioni, nikikuta mda wa habari watu wanaangukia mambo mengine nawauliza hivi ninyi hamtaki kujua ya duniani!!

Hizi ni dalili nzuri za uhenga!
Watu tuna robo kaline tu ¼ lakin shikamoo kwa madogo zimekua nyingi kwangu mpka kelo!!! ..

Kinachouma zaid ni hiv vibint vilivozaliwa 2000's vikiniamkia (Shikamoo) nahtikia lakin roho inauma kinoma!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom