Dalili gani zinakujulisha kuwa umri umesogea?

Hapa nimeshaanza kuwaza kukaa sehemu iliyotulia nifuge kuku, ng'ombe na kulima tubustani.......nadhani sio utu uzima nakumbuka tu stadi za kazi
Hiyo ya kulima bustani ni ukweli 92% wanasayansi tumethibitisha hilo kwa hiyo hatutaki kuona mtu ana mashaka na hilo.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣hii imenivunja mbavu lol! Hahahahahaha
Mie kuna siku mwendokasi inaanza nikapanda kuona likoje. Nimeingia nimekosa siti kuna mtu mzima akanipisha akaniambia kaa mzee. Nilijitathmini njia nzima na ndio ilikuwa mwisho wa kupanda mwendokasi
 
Ha haha! Basi age ishakupiga kikumbo na vipi mkono hauiweki nyuma ya mgongo unavyotembe hii style kisayansi tunaiita 'unyenyekevu style'
Bado Ila Tabia za kizee nyingi zinaninyemelea mfano MTU akinichukulia charger yangu ya simu natamani kupasuka. Kuna siku niliingia gharama ya kumnunulia MTU charger ya SHS 15000 ili asiguse yangu. Ukizeeka hutaki usumbufu kabisa.
 
Hiyo ya kulima bustani ni ukweli 92% wanasayansi tumethibitisha hilo kwa hiyo hatutaki kuona mtu ana mashaka na hilo.
Mimi nashangaa maisha yangu yote sikuwahi kupenda Maua wala bustani Kwanza nilikuwa Naona wanapoteza muda. SASA hivi hata Mie siamini ninalima tena kwenye containers mboga ikifa au ikiliwa na mdudu natamani kulia. Du uzee shikamoo.
 
Bado Ila Tabia za kizee nyingi zinaninyemelea mfano MTU akinichukulia charger yangu ya simu natamani kupasuka. Kuna siku niliingia gharama ya kumnunulia MTU charger ya SHS 15000 ili asiguse yangu. Ukizeeka hutaki usumbufu kabisa.
sasa si bora ungemwachia hiyo ya zamani alafu ww ununue mpya ila naamini ni uzee unakunyatia sio kupenda kwako, ukiwa mzee unakuwa mkoloni automatic.
 
Kuna siku moja nilienda shule moja ya chekechea aliyokuwa anafundisha rafiki wa kike wa mdogo wangu. Baada tu ya kufika na kukaa kama dakika tano wale watoto wakawa wananong'onezana "wewe Frank baba yako amekuja" hahahahaaaa nilicheka sana nikajisemea kimoyomoyo kumbe sasa ninalazimika kuwa na familia ya watoto kadhaa.
Kwani mkuu huna familia?
 
kwa sisi ambao tupo kwenye ajira kwa zaidi ya miaka mitano au zaidi, unapoanza kuletewa vijana freshers from university kwenye kitengo chako uwasimamie katika mafunzo yao ya kazi (internship), basi hiyo ni wake-up call kuwa umri wako umeanza kuwa mkubwa.
 
Nilienda kucheza Moira jumamos/jumapili mazoezi nashangaa watu wanamuita mzee nipasie huku,mshua kwangu,dingo niwekee halafu nikiwaangalia nawaona ni wakubwa

Nimeshtuka nishaanza kuwa muhenga pro max
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom