Dalili 10 (na zaidi) za kuharibika kwa uhusiano wako.

Good analysis brother, but some of these I don't agree with


QUOTE=MAMMAMIA;3809300]Iwe umeoa/umeolewa, iwe ni wachumba wa muda mfupi au mrefu, yanapotokea baadhi ya mambo haya (na mengine), ujuwe kuwa uhusiano wenu uko matatani na iko haja ya kutafuta ufumbuzi haraka.

1. Unapekuapekua simu, akaunti zake za mitandao ya kijamii, mifuko, mikoba…
Kwa nini unafanya hivyo?” Inasemwa “atafutaye hupata”, jee wewe ndicho unachotaka kuona hicho unachokitafuta? Umeshajitayarisha na matokeo yake? Ikiwa bado, wacha kumchunguzachunguzza mwenzako. Siku akigundua kuwa humwamini na yeye ni mwaminifu kwako, utakuwa umelikoroga, jitayarishe kulinywa.

2. Kila wakati anaangalia simu yake
Kiasi kwamba hana wakati na wewe. Unasema naye, yeye hayupo kazama kwenye Facebook, JamiiForum n.k. Hii itakuwa ama kuna mtu anayempumbaza kuliko wewe, au hata kama hayuko, WEWE SIO KIPAUMBELE TENA KWAKE.

Hebu jaribu kupanga naye siku jioni/asubuhi moja tu mufanye mengine nje ya teknolojia za kisasa uone atakujibu nini. Usisubiri manyoya ndio ujue kuwa ameliwa.

3.Hashirikiani nawe / hushirikiani naye tena.
Mwanzoni mlikuwa kila kitu au vitu vingi mnafanya pamoja, hata kama hafanyi yeyé lakini alikuwa karibu yako. Hata safari zenu zilikuwa pamoja, lakini sasa kila mmoja kivyake, pengine mmoja wenu atafuta kila sababu usimfuate.

4. Unamfikiri mwanamke/mwanamme mwengine.
Kwa nini iwe hivyo? Ni ishara kuwa tayari wako uliye naye ameanza kupoteza mvuto, na kuna uwezekano ukipata fursa ndoto tu unaweza kumsaliti.

5.Utani wake haukuchekeshi tena.
Mwanzo ulikuwa unacheka naye hata kwa mambo ya kipuuzi, lakini sasa unamhisi hana “sense of humour”. Mizaha yake inakuboa na ungetamani awe mbali asikuboe. Kwa nini mwanzo alikuwa anakufurahisha, sasa hakufurahishi tena?

6. Mnagombana kipuuzi puuzi.
Watu husema hata vikombe vikikaa pamoja hugongana, lakini hali yenu imepita mipaka. Mnagombana saa zote, mara nyengine hata mkiwa katika tendo la faragha. Mbaya zaidi, mnagombana hata hadharani, pengine mmoja wenu kwa makusudi anatumia maneno kwa dhamiri ya kukuumiza mwenzake.
7. Amepata/umepata kitu cha kupoteza wakati ambacho hakushirikishi/humshirikishi.
Inaweza kufanana na ile ya tatu juu, tafauti ndogo ni kuwa hapa “havumiliki tena,” na wala sio kuwa umepata au amepata mtu mwengine, bali mmoja wenu anahiari awe peke yake kupoteza wakati kuliko kuwa karibu na mwenziwe.
8. Hamzungumzi tena kuhusu hatma yenu.
Kwa watu walio na dhamiri ya kuishi pamoja, huwa wanapanga juu ya maisha yao, lakini ile hamu ya “kuota ndoto zenu an kupanga” mipango ya maisha yenu ya baadaye haipo tena. Au hata mkizungumzia hilo, kila mmoja ana msimamo wake na hayuko tayari kufuata wa mwenzake.
9. Hufanyi lolote la kumvutia mwenzako
Si mavazi, si vijizawadi vya kipuuzi, si kutomasana, si kuandaa siku/usiku maalumu. Mnaishi kwa mazowea tu na pengine “kutimiza wajibu”, lakini hakuna kilichobaki kinachokuvutia kwake au unachofanya wewe avutike nawe.

10. Unatafuta ushauri nje
Ikiwa umeridhika na uhusiano wako, huna haja ya kuuliza maswali nje (kwa marafiki, kwa wazazi, kwenye mitandao). Unapoanza kufanya hivyo, ikiwa si kwa lengo la kujifunza bali kulinganisha uhusiano wako na wa watu wengine, uelewe kuna kitu kimeanza kuharibika.

Una ishara nyengine?[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom