Dalili 10 (na zaidi) za kuharibika kwa uhusiano wako. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalili 10 (na zaidi) za kuharibika kwa uhusiano wako.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MAMMAMIA, Apr 29, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Iwe umeoa/umeolewa, iwe ni wachumba wa muda mfupi au mrefu, yanapotokea baadhi ya mambo haya (na mengine), ujuwe kuwa uhusiano wenu uko matatani na iko haja ya kutafuta ufumbuzi haraka.

  1. Unapekuapekua simu, akaunti zake za mitandao ya kijamii, mifuko, mikoba…
  Kwa nini unafanya hivyo?” Inasemwa “atafutaye hupata”, jee wewe ndicho unachotaka kuona hicho unachokitafuta? Umeshajitayarisha na matokeo yake? Ikiwa bado, wacha kumchunguzachunguzza mwenzako. Siku akigundua kuwa humwamini na yeye ni mwaminifu kwako, utakuwa umelikoroga, jitayarishe kulinywa.

  2. Kila wakati anaangalia simu yake
  Kiasi kwamba hana wakati na wewe. Unasema naye, yeye hayupo kazama kwenye Facebook, JamiiForum n.k. Hii itakuwa ama kuna mtu anayempumbaza kuliko wewe, au hata kama hayuko, WEWE SIO KIPAUMBELE TENA KWAKE.

  Hebu jaribu kupanga naye siku jioni/asubuhi moja tu mufanye mengine nje ya teknolojia za kisasa uone atakujibu nini. Usisubiri manyoya ndio ujue kuwa ameliwa.

  3.Hashirikiani nawe / hushirikiani naye tena.
  Mwanzoni mlikuwa kila kitu au vitu vingi mnafanya pamoja, hata kama hafanyi yeyé lakini alikuwa karibu yako. Hata safari zenu zilikuwa pamoja, lakini sasa kila mmoja kivyake, pengine mmoja wenu atafuta kila sababu usimfuate.

  4. Unamfikiri mwanamke/mwanamme mwengine.
  Kwa nini iwe hivyo? Ni ishara kuwa tayari wako uliye naye ameanza kupoteza mvuto, na kuna uwezekano ukipata fursa ndoto tu unaweza kumsaliti.

  5.Utani wake haukuchekeshi tena.
  Mwanzo ulikuwa unacheka naye hata kwa mambo ya kipuuzi, lakini sasa unamhisi hana “sense of humour”. Mizaha yake inakuboa na ungetamani awe mbali asikuboe. Kwa nini mwanzo alikuwa anakufurahisha, sasa hakufurahishi tena?

  6. Mnagombana kipuuzi puuzi.
  Watu husema hata vikombe vikikaa pamoja hugongana, lakini hali yenu imepita mipaka. Mnagombana saa zote, mara nyengine hata mkiwa katika tendo la faragha. Mbaya zaidi, mnagombana hata hadharani, pengine mmoja wenu kwa makusudi anatumia maneno kwa dhamiri ya kukuumiza mwenzake.
  7. Amepata/umepata kitu cha kupoteza wakati ambacho hakushirikishi/humshirikishi.
  Inaweza kufanana na ile ya tatu juu, tafauti ndogo ni kuwa hapa “havumiliki tena,” na wala sio kuwa umepata au amepata mtu mwengine, bali mmoja wenu anahiari awe peke yake kupoteza wakati kuliko kuwa karibu na mwenziwe.
  8. Hamzungumzi tena kuhusu hatma yenu.
  Kwa watu walio na dhamiri ya kuishi pamoja, huwa wanapanga juu ya maisha yao, lakini ile hamu ya “kuota ndoto zenu an kupanga” mipango ya maisha yenu ya baadaye haipo tena. Au hata mkizungumzia hilo, kila mmoja ana msimamo wake na hayuko tayari kufuata wa mwenzake.
  9. Hufanyi lolote la kumvutia mwenzako
  Si mavazi, si vijizawadi vya kipuuzi, si kutomasana, si kuandaa siku/usiku maalumu. Mnaishi kwa mazowea tu na pengine “kutimiza wajibu”, lakini hakuna kilichobaki kinachokuvutia kwake au unachofanya wewe avutike nawe.

  10. Unatafuta ushauri nje
  Ikiwa umeridhika na uhusiano wako, huna haja ya kuuliza maswali nje (kwa marafiki, kwa wazazi, kwenye mitandao). Unapoanza kufanya hivyo, ikiwa si kwa lengo la kujifunza bali kulinganisha uhusiano wako na wa watu wengine, uelewe kuna kitu kimeanza kuharibika.

  Una ishara nyengine?
   
 2. M

  Mama Ashrat Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Namba 5 inahusika sana. Hata kwenye urafiki, hicho ni kipimo kizuri cha kujua kwamba mwenzako ameshakuboa au la.
   
 3. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi ikifika hatua hiyo unachukua hatua gani? Unakomaa au unaachia ngazi?
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  vijana wanasema....unacheua mdogo mdogo......
   
 5. Erotica

  Erotica JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 2,514
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  siku hizi la msingi ni kuweka zege moyoni ili ukipanda usafiri ukifika kituo
  unashuka bila wasi wasi. Kucheua inakua kwa uraisi kama vile kichanga.
   
 6. Loy MX

  Loy MX JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  umenena namba 6 inanihusu!
   
 7. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  yote ni kweli na nimeyapitia
   
 8. hothowtie

  hothowtie Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hayo mambo tuyasome tu..yanauma kama nini!it so freaking hurts!!#sniffsniff#
  Upumbavu tu-kama huntaki si useme!
   
 9. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Inategemea mkosa nani na kwa sababu gani.
  Ikiwa unayefanya hivyo ni wewe itakuwa unajua unafanya kwa dhamiri gani.
  Ikiwa anakufanyia, tafuta usuluhishi wa amani wa mgogoro wenu.
  Ukiona hakuna maslahi, hakuna liwalo, lala mbele.
   
 10. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kuna watu hawana ubavu wa kusema, hasa ikiwa wao ndio wanaotaka lizame, hvyo wanatafuta sababu.
   
 11. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwa mtu mmoja au watu tafauti?
  Umetenda umentendewa?
   
 12. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  11. Kupungua kwa kiwango cha mawasiliano (kwa wale ambao hawaishi pamoja). Hakupigii simu au txt mpaka wewe ndo umtafute. Nawe ukichuna hata 3 days zinaweza pita hamjawasiliana ilhali unakuta mwanzo haikwa ivyo!
   
 13. k

  kisukari JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,759
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  mambo ya relationship ni pasua kichwa kwa kweli.kila mtu analalamika kwa upande wake.
   
 14. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi sana. Kama inavyosemwa, "every person or couple is a world of his/her/their own". Kuna walioharibikiwa na mengine kabisaaa tafauti na hizo sababu 10. Na hata tukitaja 1001 bado kutakuwa na nyengine nyingi.
   
 15. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Well said! Hii nayo ishara ya msingi. Fikiri ikiwa mko mbalimbali inauma, je mkiwa karibu na ikawa hakuna mawasiliano?
   
 16. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  kama watu wanne(4) hivi.
  nimetendewa na nimewatendea pia
   
 17. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Nimekukubali ! Umefunguka Mama!
  Mengi kati ya haya yanatufika then currently!
   
 18. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,394
  Likes Received: 6,578
  Trophy Points: 280
  kuwa king'anganizi is like a death sentence..ukishaona dalili kama hizo..sepaaaa...bora ya shari kamili
   
 19. Baby M

  Baby M JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 1,036
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  True fact mairo
   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  It's almost 3 yrs an half since my last relation i dont remember this stage kama zilikua hivi!
   
Loading...