Daladala zimegoma

Daladala zimegoma

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,508
Reaction score
167,120
Tabata kumechafuka,
usafiri hamna daladala zimegoma,
wanadai kuwa majembe auction mart ndio chanzo cha mgomo wao.
Magari ambayo yanaendelea na kazi ya kubeba abiria,
yanatupiwa mawe, kitu ambacho ni hatari sana kwa usalama wa gari lenyewe na abiria.
Polisi wa pikipiki wapo wanashindwa kuwadhibiti wahuni wanaofanya u nyani huo.
 
Kwani hao majembe wapo Tabata tu? Mbona maeneo maengine hawajagoma? au huko tabata ndio daladala zinaongoza kwa kuvunja sheria na kutoa rushwa kwa matrafiki?!!!!.
 
Tabata kumechafuka,
usafiri hamna daladala zimegoma,
wanadai kuwa majembe auction mart ndio chanzo cha mgomo wao.
Magari ambayo yanaendelea na kazi ya kubeba abiria,
yanatupiwa mawe, kitu ambacho ni hatari sana kwa usalama wa gari lenyewe na abiria.
Polisi wa pikipiki wapo wanashindwa kuwadhibiti wahuni wanaofanya u nyani huo.

hE! Mvunja sheria ni mtunga sheria!
 
Hawa watu wa daladala nao wanataka kujifanya kuwa wana himaya yao?
 
Tanzania Bwana. OK leo nilikuwa nasikiliza radio one asubuhi, kuna watangazaji wawili walikuwa wanazungumza kadhia hii.

Mimi sioni logic yeyete kwa SUMATRA kuwa tenda ya ukaguzi wa magari hawa majembe Action mart.

Kwani hii ya ukaguzi na usimamizi wa magari ni taaluma kamili inayojitegemea. majembe yeye ni mfanya biashara tu ( Dalali).

Ndani ya ukaguzi na usimamizi wa magari ni lazima kwanza ujue taratibu na sheria za barabara, Sheria za usafirishaji abiria, sheria za usalama barabarani, sheria za uendeshaji daladala na usimamizi wake.

Nafikiri kuna idara kuu kama mbili, tatu zinazosimamia mambo hayo, Kuna Jeshi la Polisi ( usalama barabarani), Sumatra ( sheria za usafirishaji,) Wizara ya usafirishaji ( leseni).

Suala langu. Je majembe wamefundishwa hayo yote na taasisi hizo au ndio ufisadi mwingine.

Poleni sana Dar kwa Usafiri na Joto.
 
Wacha wagome CCM wanalazimisha kujipatia pesa za kampeni wazi wazi Watanzania siyo wajinga tena
 
Back
Top Bottom