Daktari mtarajiwa afariki!

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,978
5,025
kuna mwanachuo wa udaktari mwaka wa nne muhas ajulikanaye kwa jina la Erick hyera amefariki dunia usiku wa kuamkia jumatatu kwa ajali ya gari. Ajali hiyo ilitokea mandela road maeneo ya mabibo hostel gari waliyokuwa nayo ilipogongana na gari jingine lililokuwa linakata kona. Aliyefariki ni mmoja wenzake wawili wakipatwa na majeraha na wanaendelea vizuri. Mwili wa marehemu unaagwa kesho muhimbili kwenda kwao songea kwa mazishi. R.I.P daktari wetu. Mungu awape faraja ndugu na jamaa wa muhas.
 
rip dokta..ajali ilitokea lini? dah so sad mtu keshapiga aka 4 za medicine..
 
rip dokta..ajali ilitokea lini? dah so sad mtu keshapiga aka 4 za medicine..

usiku wa kuamkia j3 ya pasaka. Hii ni mara ya pili, kuna mwingine alifariki last year 4th yr kipindi kama hiki kwa ajali ya gari naye. It is painful for the parents and those close to him wanapokutana na rafiki waliosoma naye wamemaliza chuo na wao hawanae tena. Nakumbuka kuna rafiki yangu alifariki tukiwa form 4, kutokana na kwamba tulikuwa karibu sana mama yake mpaka leo nikikutana naye huwa analia na imepita miaka zaidi ya kumi. Nikimuona kwa mbali huwa nabadili njia ninapokuwaga home. Nikitaka kumsalimia naenda nyumbani maana najua atalia na kulala usingizi lakini siyo njiani.
 
R.I.P Dr. kwenye madai yenu mlidai mpewe na magari, sasa msipokuwa makini yatawamaliza zaidi
 
Back
Top Bottom