Daktari huyu ni muuaji

hannibali

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
468
427
Habari za muda huu wanaJF, niende moja kwa moja kwenye mada

Leo nilienda dispensary moja ( jina linahifadhiwa) kwa tatizo langu binafsi, sasa nilikaa na mama mmoja ambaye ametoka kwa Daktari alikuwa anasumbuliwa na tatizo la UTI, tulikaa pamoja tukawa tunapiga stori mbili tatu yule mama alikuwa ana ujauzito wa miezi mitatu pia.

Nilitahamaki kuona aina ya dawa ambazo alikuwa amepewa na daktari; dawa zilikuwa na composition za namna hii. Doxycycline. 100mg
Acid bacillus 60 spores Mecoson.

Dawa hii ipo katika mfumo wa kitaalamu kama capsule. Dawa hii ina uwezo wa kuingilia mfumo wa utengenezwaji wa mtoto ikitumiwa katika miezi mitatu ya mwanzo ya mimba na madhara yake inaweza kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa na viungo dhaifu na mara nyingine hata ulemavu.

Nilimuuliza huyu mama kwamba kwanini daktari amekupa dawa hii akanambia yeye hajui nikamuuliza au hajui hali yako akanambia anajua hali yangu na alishamwambia.

Nikaona ngoja niende kwa daktari huyo kumuhoji vizuri kwanini aliamua kumpa dawa hizi. Kwakweli nilistaajabu kuona daktari hana majibu ya kueleweka zaidi ya janja janja za hapa na pale. Kwakweli niliondoka nae yule mama kwenda kumchukulia dawa sehemu nyingine sikuweza kuvumilia kwani yale yalikuwa kama mauaji.
 
Hongera sana kwa kuokoa maisha ya huyo mama pamoja n kiumbe ambacho kipo tumboni, wataalamu wetu wakati mwingine wanatia shaka sana

Ifike mahali serikali iweke madaktari bingwa kwa ajili ya kuwahudumia wanawake na wajawazito katika vituo vyote vya afya
 
Ndio maana ni vizuri mwanamke ukishajijua ni mjamzito hata kama una malarea kaonane na specialist wa wanawake, ukienda kwa hawa ma general doctor lazma litakukuta la kukukuta.

kuna dada mmoja yeye mimba iliharibika akaenda hospitali akasafishwa akapewa na vidoge vya kumsaidia, alipoanza kutumia vile vidonge ndo hali ikazidi kuwa mbaya zaidi badala damu ikatike akawa ana bleed kupita maelezo.

Mume wake kusoma kikaratasi (vile vikaratasi vya maelekezo ya dawa vinayokuwaga ndani ya box la dawa) akakuta zile dawa zinaweza kusababisha mimba kutoka, ndo ikawa salama yake ikabidi aache kutumia zile dawa arudi hospitali nyingine
 
Back
Top Bottom