Mkuu kwenye mambo hayo, hili ndo angalizo langu;
1) Kamwe usipambane kupata dawa ya kujua/kumuona mchawi
2) Mganga mzuri atakushauri usiweke zindiko kali mwilini kwako wala kwenye kaya yako.
KWANINI?
Kwa kufanya hivyo, unakaribisha vita na wachawi. Maana wakijua ya kuwa unaona siri zao ama wamekuja kwako kukutest wakakuta ukinzani, wataenda kuripoti kwa wakubwa zao kwamba huyu jamaa yuko fiti.
Hapo utawalazimisha kwenda chimbo kukutafutia dawa yenye level kali kuliko yako.
Utakuwa umejikaribishia vita kubwa na wachawi.
Chakufanya;
Tafuta dawa ya kumkatisha tamaa adui(mchawi) mwenye nia ovu na wewe. Yaani kila akipanga kukufanyia mabaya, ajikute kakata tamaa ama kusahau au kukudharau tu na kukupotezea.
Hii mbinu nilipewa na mzee mmoja konki ktk stori za hapa na pale.
Epuka kuchokoza mambo usiyo na utaalam nayo.
Uchawi ni taaluma za watu na husaidiana panapokuwa na ugumu.
Huu ni ushauri tu, mimi sijawahi practise mambo hayo na sitaki itokee.