Dakika 45 ITV: Mwigulu Nchemba kufanya mahojiano

D2050

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
1,958
Reaction score
1,190
Mheshimiwa naibu waziri wa fedha Mwigulu atakuwa akihojiwa leo katika kipindi cha dakika 45 ITV saa tatu usiku.

attachment.php

Mtoto wa mfugaji na naibu Waziri wa Fedha, mh Mwigulu Nchemba kupitia kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV amethibitisha kuwa yeye ni kiongozi mwenye maono thabiti juu ya nchi yetu ya Tanzania, akizungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa kama Ajira kwa Vijana, Mikopo kwa wanafunzi wa elimu Juu, Ufufuaji wa viwanda, Maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi, mh Mwigulu ametoa taswira mpya yenye matumaini mapya kuelekea nchi ya kipato cha kati.

Ajira kwa Vijana.
Akiongea kwa kuonesha uhalisia kabisa wa tatizo la ajira kwa vijana hasa waliomaliza vyuo. Mwigulu amesema serikali inaendelea kutengeneza ajira mpya maana karibu ofisi zote za umma zinalalamika kutokuwa na ufanisi kwa sababu ya uhaba wa watumishi hivyo ameagiza either wizara zitangaze ajira au watoe attachment na vijana waweze kulipwa nauli na fedha za kujikimu kuliko kuwaacha vijana wakiwa mtaani wanazurura na hili linaanza kabla ya December japo ameomba vijana watakaopata nafasi hizo wawe na moyo wa Uzalendo wa kutumikia taifa. Maana wafanyakazi wengi wanafanyakazi kwa mazoea

Mikopo Ya Elimu Juu
Hakika kiongozi bora ni yule anayejua maisha na changamoto za wananchi wake kwa hili mh Mwigulu ametuonesha kwa Vitendo akisisitiza kuwa bila yeye kupewa mkopo basi ndoto yake ingeishia f6 hivyo kwa kufahamu changamoto ya mwanafunzi kukosa mkopo amesisitiza kuwa kila pesa atakayoiokoa ataenda kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Mfano zaidi bilion 87 zilizookolewa zimepelekwa bodi ya mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Ufufuaji wa Viwanda

Akizungumzia kwa uchungu mzito mh Mwigulu amesema hapingani na sera ya ubinafsishaji bali ni ujanjaujanja unaofanywa na wawekezaji wenye mtazamo wa kama ni wahujumu uchumi maana kuna wengine toka wanunue hayo mashirika tena kwa bei ya kuhamasisha uwekezaji (Sio Market Value) ya mashirika lakini bado wameshindwa kulipa madeni na pia kuendeleza uzalishaji ili kutoa fursa za ajira kwa vijana zaidi ya kukopea fedha kwenye taasisi za fedha kama benki nk

Mwigulu tayari amemwagiza TR (Treasure Register) wa hazina awakumbushe wote wanaodaiwa walipe madeni yao na waanze uzalishaji mara moja tofauti na hapo serikali itachukua mashirika yote yaliobinafsishwa na hayapo katika uzalishaji kwani serikali inakosa kodi na pia Ajira kwa wananchi wake.

Maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi
Pia mh Mwigulu aliendelea kugusia makundi mbalimbali ya jamii yetu na akazungumzia maslahi ya wakulima na akawapongeza kwa kuzalisha mazao mengi hadi tumepita lengo la taifa, serikali imekuwa ikiwatafutia masoko katika nchi za Congo na Sudan Kusini lakini kutokana na changamoto ya Ebola na machafuko huko Sudan impala imekuwa ni migumu lakini ametoa kibali na sasa wananchi wanaweza kuuza mazao yao nje ya nchi.Pia upo mchakato unaoendelea wizarani katika kuhakikisha wafanyakazi walau mishahara yao inaboreshwa ili kuweza kukabiliana na changamoto na gharama za maisha ya sasa.

Mabadiliko ni Vitendo,Tuache Kufanya mambo kwa Mazoea.
Tunaye Mwigulu Rais Aliyependekezwa 2015
Tunakuunga mkono Mwigulu
 
Tunataka taarifa za iptl na kwa nini haijawekwa kwenye ratiba za bunge
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Gaidi hatuna haja ya kumsikiliza,naona ameamua kufanyia kazi ktk media
 
mheshimiwa naibu waziri wa fedha mwigulu atakuwa akihojiwa leo katika kipindi cha dakika 45 itv saa tatu usiku.

Kwa hiyo hawa ndiyo tunaotakiwa kuwasikiliza na si wengine.CCM inatuelekeza pabaya sana.
 
Tunataka taarifa za iptl na kwa nini haijawekwa kwenye ratiba za bunge

Kwani unadhani kwanini ripoti hawajatoa mpaka sasa? Bunge likianza tu ripoti inatolewa alafu tunasema tusubiri bunge lijalo na kuwa hatukulipanga kwa sababu ripoti haikuwa tayari
 
Ripoti ya nini ulishaona lini jambo limeamuliwa na mahakama tena mahakama kuu linatenguliwa na bunge hiyo sheria ya nchi gani.
 
Ningemsikiliza ila hawa easy tv hawana itv!!!!!!! Yaan we acha tu
 
Ripoti ya nini ulishaona lini jambo limeamuliwa na mahakama tena mahakama kuu linatenguliwa na bunge hiyo sheria ya nchi gani.

Naomba nikuulize bwana simuyu yetu! Ni kwanini Kafulila aliruhusiwa kuibua hoja ambayo mahakama kuu imeamua tayari? Wewe kama mzalendo na mwana ccm kama Mimi hutaki ripoti ipelekwe bungeni?.
 
Yeye huyo Mwigulu ni baadhi ya watu wasioamini katika kusikiliza na kuheshimu mawazo ya wengine haswa wapinzani wa mitazamo ya chama chake, iweje leo tumsikilize yeye? Kama anadhani ni vyema akasikilizwa iweje awe ni mmoja ya watu wasioamini wengine kusikilizwa? Rejea mkutano wa Dr. Slaa iramba kuhusu katiba mpya alipowapeleka simba ili watu wasiende kujua mambo ya katiba. Anaweza kusema kwamba hakumzuia mtu kwenda kwenye mkutano wa Dr. Slaa hilo ni kweli, kama kweli hakuwa na nia ovu mbona hakuwahi kuwapeleka simba/yanga tena? Kumbukeni yeye ni mmoja ya watu walioasisi wanaccm kujibu mapigo mitandaoni, ndio tukaanza kuona akina Lizaboni, ifweero, msalani nk. Tatizo sio kuleta wanaccm kujibu mapigo mitandoni bali wanajibu hoja? Hapana tumeona mitandao ya kisiasa ikichafuliwa kwa siasa chafu na kashfa zinazolenga kuficha uovu na kuendekeza mawazo mgando na taifa la watu wa mipasho. Ni vizuri tukampuuza akaendelea kuongea hayo anayosema ni mazuri mpaka atakapoona wengine nao wanapaswa kusikilizwa kwani yeye si aina ya viongozi mwenye dira ya watanzania wote bali dira ya ccm kubaki madarakani tu.
 
mkuu thank because umeona mbali
 
mheshimiwa naibu waziri wa fedha mwigulu atakuwa akihojiwa leo katika kipindi cha dakika 45 itv saa tatu usiku.

mkumbushe kuhusu kikundi alichokiandaa kutoka mbagala kwenda mkurumah hall na kukiita kikundi cha wanachuo, mkumbushe kuzungumzia kikundi cha kihuni alichokileta jana ubungo plaza
 
Naomba nikuulize bwana simuyu yetu! Ni kwanini Kafulila aliruhusiwa kuibua hoja ambayo mahakama kuu imeamua tayari? Wewe kama mzalendo na mwana ccm kama Mimi hutaki ripoti ipelekwe bungeni?.
1. Una uhakika gani kuwa huyu ni ccm mwenzio?
2. Ame challenge ukiukaji wa sheria na taratibu ila hajakataa mswada upelekwe bungeni. Kwamba hiyo hoja ilishaamuliwa na mahakama haiwezi kurudishwa tena bungeni
 
Nauliza tena ingawa umechukua nafasi ya msemaji wa #Simiyu yetu! Kama unachosema ndicho ni kwanini bunge liliamuru suala Hilo lishugulikiwe na CAG na TAKUKURU? Alafu Naona unachanganya mambo kilichoamuliwa na mahakama sio kinacholeta mjadala na mashaka.
 
mkumbushe kuhusu kikundi alichokiandaa kutoka mbagala kwenda mkurumah hall na kukiita kikundi cha wanachuo, mkumbushe kuzungumzia kikundi cha kihuni alichokileta jana ubungo plaza

Nkrumah tena?
 
mheshimiwa naibu waziri wa fedha mwigulu atakuwa akihojiwa leo katika kipindi cha dakika 45 itv saa tatu usiku.

Ahsante sana kwa taarifa lazima nimsikilize kiongozi mwenye maono makuu na makubwa kwa taifa letu la Tz
 
attachment.php

Mtoto wa mfugaji na naibu Waziri wa Fedha, mh Mwigulu Nchemba kupitia kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV amethibitisha kuwa yeye ni kiongozi mwenye maono thabiti juu ya nchi yetu ya Tanzania, akizungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa kama Ajira kwa Vijana, Mikopo kwa wanafunzi wa elimu Juu, Ufufuaji wa viwanda, Maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi, mh Mwigulu ametoa taswira mpya yenye matumaini mapya kuelekea nchi ya kipato cha kati.

Ajira kwa Vijana.
Akiongea kwa kuonesha uhalisia kabisa wa tatizo la ajira kwa vijana hasa waliomaliza vyuo. Mwigulu amesema serikali inaendelea kutengeneza ajira mpya maana karibu ofisi zote za umma zinalalamika kutokuwa na ufanisi kwa sababu ya uhaba wa watumishi hivyo ameagiza either wizara zitangaze ajira au watoe attachment na vijana waweze kulipwa nauli na fedha za kujikimu kuliko kuwaacha vijana wakiwa mtaani wanazurura na hili linaanza kabla ya December japo ameomba vijana watakaopata nafasi hizo wawe na moyo wa Uzalendo wa kutumikia taifa. Maana wafanyakazi wengi wanafanyakazi kwa mazoea

Mikopo Ya Elimu Juu
Hakika kiongozi bora ni yule anayejua maisha na changamoto za wananchi wake kwa hili mh Mwigulu ametuonesha kwa Vitendo akisisitiza kuwa bila yeye kupewa mkopo basi ndoto yake ingeishia f6 hivyo kwa kufahamu changamoto ya mwanafunzi kukosa mkopo amesisitiza kuwa kila pesa atakayoiokoa ataenda kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Mfano zaidi bilion 87 zilizookolewa zimepelekwa bodi ya mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.

Ufufuaji wa Viwanda

Akizungumzia kwa uchungu mzito mh Mwigulu amesema hapingani na sera ya ubinafsishaji bali ni ujanjaujanja unaofanywa na wawekezaji wenye mtazamo wa kama ni wahujumu uchumi maana kuna wengine toka wanunue hayo mashirika tena kwa bei ya kuhamasisha uwekezaji (Sio Market Value) ya mashirika lakini bado wameshindwa kulipa madeni na pia kuendeleza uzalishaji ili kutoa fursa za ajira kwa vijana zaidi ya kukopea fedha kwenye taasisi za fedha kama benki nk

Mwigulu tayari amemwagiza TR (Treasure Register) wa hazina awakumbushe wote wanaodaiwa walipe madeni yao na waanze uzalishaji mara moja tofauti na hapo serikali itachukua mashirika yote yaliobinafsishwa na hayapo katika uzalishaji kwani serikali inakosa kodi na pia Ajira kwa wananchi wake.

Maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi
Pia mh Mwigulu aliendelea kugusia makundi mbalimbali ya jamii yetu na akazungumzia maslahi ya wakulima na akawapongeza kwa kuzalisha mazao mengi hadi tumepita lengo la taifa, serikali imekuwa ikiwatafutia masoko katika nchi za Congo na Sudan Kusini lakini kutokana na changamoto ya Ebola na machafuko huko Sudan impala imekuwa ni migumu lakini ametoa kibali na sasa wananchi wanaweza kuuza mazao yao nje ya nchi.Pia upo mchakato unaoendelea wizarani katika kuhakikisha wafanyakazi walau mishahara yao inaboreshwa ili kuweza kukabiliana na changamoto na gharama za maisha ya sasa.

Mabadiliko ni Vitendo,Tuache Kufanya mambo kwa Mazoea.
Tunaye Mwigulu Rais Aliyependekezwa 2015
Tunakuunga mkono Mwigulu
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1415084574.692407.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1415084574.692407.jpg
    17.1 KB · Views: 1,497
Heri hata huyu;
Ameweza hata kukusanya kodi na kuondoa majina hewa kwenye payroll ya serikali;
 
Back
Top Bottom