acer
JF-Expert Member
- Apr 4, 2012
- 1,595
- 142
Heri hata huyu;
Ameweza hata kukusanya kodi na kuondoa majina hewa kwenye payroll ya serikali;
Sasa ameanza kupambana na tatizo la ajira kwa vijana
Heri hata huyu;
Ameweza hata kukusanya kodi na kuondoa majina hewa kwenye payroll ya serikali;
Heri hata huyu;
Ameweza hata kukusanya kodi na kuondoa majina hewa kwenye payroll ya serikali;
Time will tel
ajitose sasa kupambana na escrow,ujangiri,rushwa,madawa ya kulevya n.k japo kua mengine ni nje ya wizara yake.
Sasa ameanza kupambana na tatizo la ajira kwa vijana
Mh!Na percent yake ataipata wapi bila hiyo?Hizo zote ni blablah lakini anajua anachokifanya.Hawa wote wanaongea wakidhani watanzania bado tupo wajinga,angekuwa anaubavu angeikataa Katiba ya Mafisadi .
Ukiisha ikubali ile Katiba ya Chenge hata uwe mzuri kivipi wewe ni FISADI pia.Inakuwaje kuondoa vipengele vya kuwawajibisha hawa watawala,unakubali mafisadi wafungue account nje ya nchi ili iwe nini,halafu unakuja kutupigia blahblah za ajira kwa vijana,yaani huyu muuaji wa Arusha alitakiwa kuwa ndani saa hizi lakini kulingana na sheria za KiCCM ukiwadhuru wapinzani basi unahongwa cheo.
Mwigulu ni kiongozi shupavu, jasiri, mzalendo na mwenye uthubutu
Mwigulu ni rais wetu 2015
Hana uthubutu wowote ule.
Kuna kashfa kibao za ulaji wa pesa za umma, mikataba feki ya wawekezaji, n.k.
Sijamuona hata kutoa kauli ya kulaani ulaji huo.
Tunataka taarifa za iptl na kwa nini haijawekwa kwenye ratiba za bunge
![]()
Mtoto wa mfugaji na naibu Waziri wa Fedha, mh Mwigulu Nchemba kupitia kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV amethibitisha kuwa yeye ni kiongozi mwenye maono thabiti juu ya nchi yetu ya Tanzania, akizungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa kama Ajira kwa Vijana, Mikopo kwa wanafunzi wa elimu Juu, Ufufuaji wa viwanda, Maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi, mh Mwigulu ametoa taswira mpya yenye matumaini mapya kuelekea nchi ya kipato cha kati.
Ajira kwa Vijana.
Akiongea kwa kuonesha uhalisia kabisa wa tatizo la ajira kwa vijana hasa waliomaliza vyuo. Mwigulu amesema serikali inaendelea kutengeneza ajira mpya maana karibu ofisi zote za umma zinalalamika kutokuwa na ufanisi kwa sababu ya uhaba wa watumishi hivyo ameagiza either wizara zitangaze ajira au watoe attachment na vijana waweze kulipwa nauli na fedha za kujikimu kuliko kuwaacha vijana wakiwa mtaani wanazurura na hili linaanza kabla ya December japo ameomba vijana watakaopata nafasi hizo wawe na moyo wa Uzalendo wa kutumikia taifa. Maana wafanyakazi wengi wanafanyakazi kwa mazoea
Mikopo Ya Elimu Juu
Hakika kiongozi bora ni yule anayejua maisha na changamoto za wananchi wake kwa hili mh Mwigulu ametuonesha kwa Vitendo akisisitiza kuwa bila yeye kupewa mkopo basi ndoto yake ingeishia f6 hivyo kwa kufahamu changamoto ya mwanafunzi kukosa mkopo amesisitiza kuwa kila pesa atakayoiokoa ataenda kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Mfano zaidi bilion 87 zilizookolewa zimepelekwa bodi ya mikopo kwa ajili ya elimu ya juu.
Ufufuaji wa Viwanda
Akizungumzia kwa uchungu mzito mh Mwigulu amesema hapingani na sera ya ubinafsishaji bali ni ujanjaujanja unaofanywa na wawekezaji wenye mtazamo wa kama ni wahujumu uchumi maana kuna wengine toka wanunue hayo mashirika tena kwa bei ya kuhamasisha uwekezaji (Sio Market Value) ya mashirika lakini bado wameshindwa kulipa madeni na pia kuendeleza uzalishaji ili kutoa fursa za ajira kwa vijana zaidi ya kukopea fedha kwenye taasisi za fedha kama benki nk
Mwigulu tayari amemwagiza TR (Treasure Register) wa hazina awakumbushe wote wanaodaiwa walipe madeni yao na waanze uzalishaji mara moja tofauti na hapo serikali itachukua mashirika yote yaliobinafsishwa na hayapo katika uzalishaji kwani serikali inakosa kodi na pia Ajira kwa wananchi wake.
Maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi
Pia mh Mwigulu aliendelea kugusia makundi mbalimbali ya jamii yetu na akazungumzia maslahi ya wakulima na akawapongeza kwa kuzalisha mazao mengi hadi tumepita lengo la taifa, serikali imekuwa ikiwatafutia masoko katika nchi za Congo na Sudan Kusini lakini kutokana na changamoto ya Ebola na machafuko huko Sudan impala imekuwa ni migumu lakini ametoa kibali na sasa wananchi wanaweza kuuza mazao yao nje ya nchi.Pia upo mchakato unaoendelea wizarani katika kuhakikisha wafanyakazi walau mishahara yao inaboreshwa ili kuweza kukabiliana na changamoto na gharama za maisha ya sasa.
Mabadiliko ni Vitendo,Tuache Kufanya mambo kwa Mazoea.
Tunaye Mwigulu Rais Aliyependekezwa 2015
Tunakuunga mkono Mwigulu
Matamko hayana tija,hapa ni vitendo tu mipasho tumewaachia upinzani.
Matamko hayana tija,hapa ni vitendo tu mipasho tumewaachia upinzani.
Mhe. Mwigulu mwanzo wa mazungumzo yake na Emmanuel Buhohela alisema eti wakati akiwa amemaliza degree yake ya pili yaani Masters hakuwa na kazi. Ili kuhudumia familia yake alifanya kazi ya kufyatua matofali huku mke wake mwenye degree moja akipika vitumbua/mandazi/chakula cha mama ntilie katika eneo la kazi ya kufyatua matofali! Kwa bahati mbaya mtangazaji Buholela hakumuuliza ni wapi na walifanya kazi hiyo kwa muda gani! Sitaki kuamini hata kidogo, kwa umri wa Mhe. Mwigulu na wakati anapata hiyo Masters angeweza kufanya kazi alizosema mbele ya watanzania. Alisema maneno haya kwa lengo gani? Ni kwanini viongozi wanapenda kuonekana ni masikini huku ni matajiri wa kutupwa. Tafakari
Wizi wa Pesa za EPA BOT zilifanyika 2006Onyesha 'vitendo' alivyofanya kudhibiti ulaji wa mali ya umma..!!
Jikite kwenye ulaji wa TPA, Escrow, EPA, na Richmond.
Tuanzie hapo kwanza....!!!!
Kama matamko hayana tija, anaenda kwenye TV kufanya nini..??
Kwenye mahojiano anakaa kimya au anatoa kauli mbali mbali..??
Juzi-juzi alitoa kauli rasmi la kugombea urais 2015...!!
Upo hapo..??