Porojo tu[/QUOTE
Mwigulu:
Kiboko cha wakwepa kodi,kiongozi aliyedhamiria kuwabana Wakwepa kodi.
-
Na Mwandishi Wetu
Hivi karibuni serikali ilitangaza vita na baadhi ya wafanyabiashara nchini wanaofanya hujuma kwa kukwepa kulipa kodi na kuwaonya baadhi ya watumishi wanaoshirikiana na -wafanyabiashara hao kukwepa kodi na kusababisha serikali kupoteza mapato.
-
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu Nchemba, alisema kuanzia sasa, serikali itapambana kufa kupona dhidi ya wafanyabiashara na mawakala wake wanaoshiriki kukwepa kodi.
-
Mwigulu, alikuwa katika ziara ya kukagua maendeleo na miradi ya maji wilayani Gairo, mkoani Morogoro ambapo alisema kuwa tayari serikali imeingia rasmi kwenye mapambano.
-
Anachokisema Mwigulu ni sahihi kwamba serikali haiwezi kuwatoza kodi wauza vitumbua wakati kuna matajiri wakubwa wanakwepa kodi.
-
Mwezi Juni ya mwaka huu, Mwigulu alisema kuwa serikali haitawaogopa wala kuwaonea haya wakwepa kodi na kwamba, kuanzia sasa misamaha yote ya kodi itawekwa hadharani.
-
Aidha, alisema kuwa msamaha utakaotolewa na serikali utatakiwa kuendana na huduma za kijamii zilizolengwa na kuwa itawekwa kwa kufuata utaratibu wa kisheria na si kiholela.
-
Mwigulu, alikuwa akizungumzia mwelekeo wa bajeti na jinsi serikali ilivyojipanga katika kusimamia makusanyo ya ndani.
Mwigulu alikuwa akirejea tabia ya ujanja ya baadhi ya watu ambao wanaingiza bidhaa- kwa msamaha -lakini ukija kwenye huduma za jamii unakuta bidhaa hizo zinauzwa kibiashara.
-
-
Ndio maana alisema jambo kubwa ni ushirikiano wa wananchi na kwamba alishawaeleza mawakala wa forodha kwamba popote wanapopata taarifa za mtu kukwepa kodi ama mtu kudanganya kuhusu bidhaa ikiwa ni pamoja na kupitisha bidhaa tofauti na iliyopewa msamaha, atoe taarifa kwa kuwa ni hujuma.
-
-
Yawezekana hili la ushirikiano kwa wananchi ndio liliweza kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumia mmoja wa wakwepa kodi- siku chache baada ya kutoa kauli hiyo bungeni.
-
Kwa kutumia wasamaria wema Mwigulu mwenyewe -alifanikiwa kukamata mtuhumiwa wa uhujumu uchumi -katika eneo la Changombe jijini Dar es Salaam.
-Inaelezwa kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kuliwezesha kuokoa jumla ya shilingi -bilioni 7. Mtuhumiwa -alipandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo.
-
Yawezekana pia tukio hilo ndilo lilimfanya Mwigulu apachwe jina la Sokoine mdogo,
Sokoine akiwa Waziriri mkuu wa Tanzania alijitoa mhanga kupambana na wahujumu- uchumi bila- woga hadi mauti yalipomkuta kwa ajali ya gari akitokea Dodoma.
-
Nidhahiri kuwa katika suala hili kuna changamoto nyingi ambazo serikali inatakiwa kuwa makini katika kushughulikia kikamilifu.
-
Yapo madai kuwa baadhi ya -maofisa waandamizi wa polisi wanatajwa kuhusishwa katika kashfa ya kuwalinda wakwepa kodi.
Hili ni eneo ambalo Mwigulu anatakiwa kulitupia macho kwani sio siri kwamba baadhi ya askari wamekuwa wakiwalinda na- wakati mwingine kuwasaidia -wafanyabiashara wanaokwepa kodi.
Ni madai mazito ambayo si vema kuyapuuza, kwani lisemwalo lipo.
Katika kuthibitisha hili, Mei mwaka jana -Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliwahi kuagiza kukamatwa kwa baadhi ya askari waliodaiwa -kuonekana kwenye picha zilizokuwa zikirekodiwa.
Namini serikali imefanya kazi kubwa hadi sasa.- Kwani miaka michache tu iliyopita serikali iliweka mkakati wa kudhibiti mianya ya ukwepaji wa kodi kwa wafanyabishara.
Mkakati huo ni pamoja na kutumia -mashine maalum ya kukusanyia kodi kutoka kwa wafanyabiashara wa kada zote.
Mashine hii -inayojulikana kwa jina la Rejista za Kodi za Kielektroniki (Electronic Tax Register-ETR), nako kumesaidia kuwabana- wakwepa kodi.
-
Kama Mwigulu amepania kweli kuwabana wakwepa kodi, anatakiwa kudhibiti katika usimamiaji wa- suala hilo kwani bado kuna ujanja katika matumizi ya mashine hizo.
Ukweli ni kwamba wengi hawazitumii ipasavyo ingawa kuna taarifa -kuwa -tangu kuanza kutumika kwa utaratibu huo wa mashine, kumekuwa na ongezeko la makusanyo ya kodi.
-
MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI
Kwa kawaida kazi ya serikali ni kukusanya kodi lakini pia inapaswa kuwa na mipango thabiti ya matumizi yake. Hapa- nataka kuzungumzia matumizi ya fedha za serikali.
-
Kila mtu anafahamu kuwa mara kwa mara na kila mwaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekuwa akifichua madudu ya kutisha katika mfumo mzima wa matumizi ya fedha za Serikali.
Tunaweza kulihesabu kuwa jambo hilo ni janga la kitaifa kutokana na kuwa ni tukio linalotokea kila mwaka hali inayochukuliwa kana kamba hakuna dawa yake maalum.
-
DENI LA SERIKALI
Hili la mfumo mbaya wa matumizi ya fedha za serikali,- linakwenda sambamba- na kuzalisha deni la serikali.
-
Nakumbuka katikati ya mwaka huu, Bunge liliambiwa kwamba Deni la Taifa limeongezeka kwa kasi na kufikia jumla ya shilingi trilioni 8.2- kwa kipindi cha miezi saba tu.
-
Aidha, bunge hilo liliambiwa kuwa hadi kufikia mwezi Juni mwaka jana deni hilo lilikuwa Shilingi trilioni 21.2 na hadi Januari mwaka huu, deni hilo lilipaa hadi na kufikia shilingi trilioni 29.4.
-
Ikaelezwa pia kuwa sehemu ya fedha hizo zikikopwa kwa ajili ya kuendesha semina, warsha, safari, mafunzo na matengenezo ya magari. Kwa maana hiyo, kila Mtanzania sasa anadaiwa Shilingi 600,000.
-
Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara bungeni, Mwenyekiti wake, Luhaga Mpina alisema Sh24.18 trilioni ni deni la Serikali, Sh3.75 trilioni ni deni la sekta binafsi na Sh1.15 trilioni ni deni la Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
-
Hali hiyo ya kutisha imetokea hata baada ya taasisi za kifedha za kimataifa na mabingwa wa masuala ya uchumi kuonya kuwa, Tanzania inakabiliwa na janga kubwa la mzigo wa madeni iwapo Serikali haitapunguza kasi ya mikopo isiyokuwa na tija katika kuinua uchumi.
-
Onyo hilo linapaswa litukumbushe jinsi janga la deni la taifa lilivyoligharimu taifa kiuchumi katika miaka ya 90, ambapo karibu rasilimali zote ambazo Serikali ingezitumia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na pia kuziwekeza katika huduma muhimu za kijamii zilielekezwa katika kulipa madeni.
-
Mwaka 2006, Deni la Taifa lilikuwa asilimia 70 ya Pato la Taifa. Deni la Taifa hivi sasa linakadiriwa kuwa kati ya asilimia 47 na 50 ya Pato la Taifa, ambalo linakadiriwa kuwa Shilingi trilioni 50.
-
Ni jambo lililowazi kuwa Deni la Taifa limekua kwa kasi ya kutisha kutoka Shilingi trilioni 10 mwaka 2005 hadi Shilingi trilioni 29.4 Januari mwaka huu.
Kinachooekana hapa ni kwamba deni hilo haliendi sambamba na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ujenzi wa miundombinu hapa nchini.
Baadhi ya wataalum wa mambo ya uchumi wanasema wazi kuwa huenda deni hilo limekuwa uchochoro wa ubadhirifu wa fedha za umma.
-
Ndio maana wataalum hao- wanasema kuwa suala la msingi hapa siyo Serikali kukopa, bali mikopo hiyo inayokadiriwa kuwa Shilingi zipatazo -trilioni 2 kila mwaka inachukuliwa kwa ajili ya kuufanya kitu gani.
-
Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zinaonyesha kwamba kati ya Januari na Oktoba mwaka uliopita, Deni la Taifa lilipaa kwa shilingi trilioni -5.
-
NI VIPI DENI HILO LINALIPWA?
-
Katika mahojiano maalum na- gazeti hili hivi karibuni,- Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alielezea mikakati kadhaa ya serikali katika kulipa madeni.
-
Mwandishi: Bila shaka Naibu Waziri unafahamu kuwa serikali inadaiwa takribani trilioni 8. 4. Wewe kama kiongozi wa serikali mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya kifedha, nini kinafanyika kuona kuwa deni hilo linalipwa?
-
Mwigulu: Siku zote, dawa ya deni ni kulipa. Kwa kuzingatia dhana hiyo, ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa serikali inaandaa utaratibu wa jinsi ya kulipa madeni inayodaiwa na taasisi za hifadhi ya jamii pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).
-
Mifuko hiyo inaidai Serikali Sh8.43 trilioni. Nikitaja mfuko mmoja mmoja ni kuwa, Mfuko wa PSPF unadai shilingi bilioni 429, PPF unadai jumla ya shilingi bilioni 192, NSSF unadai shilingi bilioni 467 bilioni, NHIF unadai shilingi bilioni 107, -LAPF unadai shilingi bilioni 170- na GEPF unadai shilingini bilioni 6.8.
Jumla hiyo ya deni la Serikali linahusisha deni jingine la PSPF la Sh7.06 trilioni ambayo ni malimbikizo ya madeni ya muda mrefu.
Mwandishi:- Unaweza kuwaeleza wananchi deni hilo linakujaje yaani linapatikana au linatokana na nini?
-
Mwigulu:- Mifuko hiyo huikopesha Serikali kupitia wizara mbalimbali, fedha ambazo hutakiwa kulipwa baada ya muda fulani.
-
Wizara zisipolipa na hivyo deni kukaa kwa muda mrefu, huingizwa kwenye deni la Taifa.
-
Madeni hayo ni makubwa, kwa maana hiyo yanahitaji baraza la mawaziri kujadili utaratibu gani utatumika kulipa.
-
Mwandishi: Kuna jitihada zozote ambazo serikali imeonyesha katika kulipa angalau kwa kiwango kidogo?
-
Mwigulu: Madeni haya ni makubwa. Lazima kuwe na utaratibu wa kuyalipa, sio kwamba serikali imelala tu kuhusu jambo hilo, la hasha.
Kwa mfano deni la PSPF ni kubwa na linahitajika kulipwa, hivyo tunaweka utaratibu, katika kuthibitisha kauli yangu ni kwamba mwaka jana tuliilipa PSPF zaidi ya Shilingi bilioni 50.
-
Tumefanya hivyo kwa kutambua kuwa mifuko hiyo nayo ina mahitaji yao ili kujiendesha.
Mwandishi: Vipi kuhusu deni la MSD?
-
Mwigulu: -Kuhusu deni hili la -Bohari ya madawa (MSD), tulichofanya ni kwamba tumetaka mchanganuo wa wizara na kila halmashauri, -jinsi gani fedha zilizotolewa kwa ajili ya dawa zimetumika.
-
Mwaka jana Serikali ilitoa shilingi bilioni 47- kwa ajili ya dawa katika wizara na halmashauri, lakini fedha zilizotumika kununulia dawa ni Shilingi bilioni 7 tu.
-
Nyingine wamefanyia mambo mengine na ndiyo maana tunasema hatuwezi tukawa tunatoa tu fedha bila kupewa mchanganuo wa fedha hizo zimefanyiwa nini.
-
Mwandishi: Ahsante sana mheshimiwa Mwigulu.
Mwigulu: Ahsante, kazi njema.