MAGAMBA MATATU
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 646
- 1,174
- Thread starter
- #21
Magamba Matatu(3) na Wana JF,
Hii ndio tatizo la Wabunge wa Chama Tawala kuwa wengi na kupitisha kila kitu hata kama kibaya, kuna haja ya kuwa na Wabunge wengi wa Upinzani watakaoleta Ushindani wa Hoja. Huu ni Uoga wa hali ya juu, Mh Ndugai kwanza ni mzoefu wa miaka mingi, anajua kinachoendelea ana cheo cha Unaibu Spika, sasa atashindwaje kukemea na kubadilisha mambo yote yasiyokuwa na tija na Taifa letu, au analinda kibarua chake ?? Anataka kujisafisha kuwa wao Wabunge wanalipwa kidogo kuliko mihimili mingine yaani Serikali na Mahakama ?? Tuacheni Siasa za kinafiki, tujenge Nchi yetu.
My Take: Tunamtaka Mh Ndugai atuambie Mahakama na Serikali Viongozi wao wanalipwa Posho Tshs ngapi ?? Ili wananchi ambao ndio wenye Nchi tuamue !!! otherwise Samaki mmoja akioza wote wameoza. Sipo Upande wowote haya ni Maoni na Mawazo yangu tu
Nawakilisha
Lakini kasema kuwa siyo vizurikutaja posho za watu, ila cha msingi kasisitiza kuwa kama watanzania wakijua posho hizo wanazolipwa hiyo mihimili ya mahakama na serikali basi watajinyonga tena sana, ila ilikuwa imebaki kidogo aanze kuzitaja hizo posho baada ya mtangazaji kumbana ila akagundua angekiweka kitumbua chake rehani akasema hawezi kuweka mambo hadharani kama alivyoweka mshahara wa Mh waziri mstaafu Sumaye, Ndugai alidai kuwa Sumaye anapta posho kama za wabunge japo kastaafu,, duuu nilitamani hiki kipindi kiwe dakika 90 na siyo 45 kwani Ndugai alikuwa anaelekea kumwaga kila kitu.