Dakika 45 ITV: Jobu Ndugai apasua siri jinsi nchi inavyofilisiwa na serikali iliyoko madarakani

Pamoja na kumlaumu Ndugai, kuna haja y akuyajadili aliyoyasema pia. Jamani hii nchi imefikia mahali ambapo kila mtu anakufa na chake. Ndugai anayoyasema ni kweli wala hayana ubishi. Juzi tu kuna Assistance mmoja alihudhuria kikao kwa niaba ya bosi wake wizarani, alirudi baada ya masaa mawili na machozi usoni!!!!!!!

Analia kwani baada ya kikao cha masaa mawili walipewa bahasha yenye shilingi za kitanzania 800,000/= (laki nane) posho ya kikao!!! Aliposhangaa akaambiwa ni kwa kikao hiki tu lakini vingine posho yetu huwa shilingi millioni moja na laki mbili!!!

Ndugai anamaanisha anachokisema! Tukiyaona na kuyajua tutajinyonga kama sio kuipiga nchi kiberitii tukose wote...


Ni kwlei kabisa. Lakini jamaa wakati analia alikuwa ameshalamba 800,000 au aliikataa??
Kama aliiikataa, basi alikuwa na sababu ya kulia.
 
very stupid indeed!!
Kazi ya bunge ni kuisimamia serikari, kwa hiyo serikali ikiiiba na bunge liiibe? pumbavu kabisa!!
Two wrong can't make it right
 
hata kama kuna mihimili mingine ya serikali ambayo inakula pesa zaidi ya wabunge lakini dhambi ni dhambi tuuu, hakuna cha ndogo wala kubwa,,,,so tuanzie na wabunge alafu tutaendelea na hao wengine!
 
nimemshanga sana na inaonyesha upuuzi huu wanaufanya kwa makusdi ajui hata anachokizungumza unajua kuna siku kaka yangu aliniambia hata jobndugai kawa mbunge tena naibu speaker nikasema kwan vp akanijibu basi kumbe hata mimi naweza kuwa kiongozi safi kama kweli huyu bwana amekuwa kiongozi tena mkubwa nikabaki nimeduwaa sasa leo ndo nimeamini huyu ndugai uwezo wake ni mdogo sana wa kujenga hoja



Hata mimi jan sikuamini mtu mwenye nafasi kubwa kwenye muhumili mkubwa kama Bunge kuwa kama NDUGAI,majibu yake yalikuwa mepesi muno ambayo hayana mashiko.Alisema anasikitika kuona watanzania kuwachukia viongozi wao,yaani hata yeye kanikela saana huyu jamaa,alafu ameonyesha dhaili ana wivu saana
 
Ndugai asifananishe majaji na wabunge, majaji ni proffesional wakati wabunge ni siasa tu mdomoni. kweli ccm imekuwa kila kiongozi ni kambale, mtoto ana ndevu, mama ana mdevu na baba ana ndevu. hakuna kuheshimiana.
Hiindo post ya kufungua mwaka hii!!!!!
 
Me sikubaliani naye manake anao uwezo wa kuyatatua yote haya lakini amekazania "heshima ya chama"
 
Huyu Ndugui[Ndugai] ni pumbaffu kama zilivyo pumbaff zinginezo kwene chama chake!! Kazi moja wapo ya Bunge ni kuhoji matumizi ya serikali na kutunga sheria ikiwemo kuisimamia serikali!! kwa hivo kama kaona mihili mingine inapata zaidi, angehoji mantiki ya kuwa na posho kubwa ilhali watumishi kama madaktari, walimu na wengineo wakisota kupata mishahara yao na posho!!!!!
ASIWAFANYENI NINYE MNAOMSIKILIZA MAMBUMBUMBU HADI KUMUUNGA MKONO ETI KAPASUA JIPU JAMANI HALAFU NANYI MKAKUBALI KIRAHISI!!
Ni mmoja wa hao wezi anayejaribu kubadilisha upepo wa mjadala ili aingize hizo posho wakti ninyi mko busy kujadili posho za mahakama!!!
 
Job Ndugai kanisikitisha.
Nae anaingia kwenye orodha ya magamba yasiyofaa kuwa viongozi wa uma.
How the hell did he become a deputy speaker?
OTIS
Alichaguliwa na wabunge wote wa CCM, NCCR mageuzi, TLP na CUF.
Rejea kumbukumbu za bunge....alipata kura 197 za ndio ndani ya chama chake, huku moja tu ikimkataa na moja kuharibika.
That is to say, hiyo ndio product ya CCM. halafu CUF wakawaunga mkono wame zao.!!
 
I agree ni wote wanaomwona huyo jamaa (Naibu spika) ni mzushi.Ina maana na yeye anaendelea na muendelezo huo huo wa kufuja pesa za walipo kodi.Mstaafu alisema ukweli, subirini wanajeshi nao watakapo anza kudai kudai hizo posho,waje na walimu ,madaktari ndo tuone kama nchi itatawalika.Kila kazi ina umuhimu wake usidharau kazi ya mwenzako hata kama ni kuzibua vyoo
 
Baada ya kusoma posts za hapa JF, sijutii hatua yangu ya kuamua kuangalia Setanta Africa badala ya kuangalia ITV jana usiku pamoja na kufahamu kuwa alikuwepo Ndugai. Kweli nchi inaelekea kubaya sana
 
inaniuma sana nikifikiria.hivi hawa wametuona sisi ni weapumbavu kiasi gani.??watu wasio na huruma.inamaana kjama kuna watu wanapata posho kubwa sasa wao si wakemee nao wanajionge
 
Job Ndugai kanisikitisha.
Nae anaingia kwenye orodha ya magamba yasiyofaa kuwa viongozi wa uma.
How the hell did he become a deputy speaker?
OTIS
Kiongozi unasema naye anaingia kwenye orodha ya magamba!!!!kwani Ndugai alitoka lini kwenye hiyo orodha ya magamba???yupo humo, anaishi humo, anazeekea humo na anafanya yanayofanyika humo kama wengine wanavyofanya humo. Huwezi kuwa comfortable ndani ya CCM kama huna sifa zaCCM.
 
Naibu Spika Jobu Ndugai amedai kuwa watanzania inabidi wasilaumu sana wabunge kuongezewa posho, Ndugai kasema kuwa kuna muhimili mitatu ya nchi ambayo niBUNGE, SERIKALI NAMAHAKAMA, Ndugai kasema kama watanzania wangejua ni kiasi cha posho kubwa wanacholipwa viongozi wa seikali na mahakama basi watanzania wangejinyonga kabisa badala ya kulaumu hizi wabunge ambacho ambacho kadai kuwa ni kidogo kuliko wananchi wanavyofikilia,

Hii kauli ya Ndugai ilimshitua hadi mtangazaji baada ya kusikia kuwa nchi hii kuna zaiudi ya maefu ya wafanyakazi wanapokea posho za kutisha kuliko hata wabunge, Ndugai kadai wabunge ni wafanyakazi wasiozidi hata 350 lakini ndoo wamenyooshewa kidole na waandishi wa habari bila kufahamu kuwa kuna posho zinalipwa mara 10 zaidi ya hizo zao kwa siku na kudai kuwa ni maelfu ya wafanyakazi wa mihimili ya serikali na mahakama na hii ndoo imefanya hadi wabunge waamue kujiongezea.

Huyo ndoo Ndugai kaamua kutoboa siri iliyojificha, ama kweli kumbe wafanyakazi wanaweza kulipwa kima cha chini kisichopungua 350000, hapa ndoo nimeamini baada ya Ndugai kumwaga mboga,.

Maelezo ya Mhe Ndugai jana katika kipindi cha Dakika 45 yalikuwa ni ya kujikosha, kwa kauli zake inammanisha yakuwa wabunge wetu hususana kutoka CCM ambao wamekuwa wakikwamisha wabunge wa upinzani kuchukua hatua mbali mbali wameshindwa kutekeleza majukumu yao ya kuismamia Serikali kama inavyoelekezwa na ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 (Tazama hapa chini); hivyo wameamua kuungana na wezi wa fedha za watanzania ili nao wanifaike na wizi huo unaojuikana kama Posho na marupurupu.

63.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.
(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza-
(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.



kwa kauli zake za jana Mhe Ndugai kama Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhimili wa Bunge) kulithibitishia taifa kuwa katika hiyo mihimili mitatu ya uongozi hapa nchini (yaani Bunge, Serikali na Mahakama) watu wanalipana malipo tata kwa nia ya Posho kwa kufanya kazi walizoajiriwa kuzifanya na kupokea mishahara, Vile vile amelithibitishia taifa kuwa mhimili wa Bunge ambao kwa kiwango kikubwa wabunge wake wengi ni kutoka chama cha CCM umeshindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa ibara ya 63 ya Katiba kwa kushindwa kuihoji Serikali kuhus malipo haya tata wakati wa majadiliano ya bajeti.

Uzoefu unaonyesha kuwa mika nenda mika rudi wabunge wa vyama vya upinzania wamekuwa wakhoji kasma mbali mbali za wizara mbali mbali wakati wa mjadala wa bajeti bungeni, lakini wamekuwa wakikatishwa tamaa na wabunge wa CCM ambao mara zote huwazomea na wabunge wa upinzani. Wabunge wa CCM husbiri muda wa kupitisha bajeti kwa mtindo wa "Gilloting" ambapo Spika huwahoji wanaokubali waseme ndio na wabunge wote wa CCM husema "NDIYO" na kupitisha makadirio ya wizara mbali mbali yaliyosheheni Malipo tata ya hizi Posho na wizi mwingine mwingi

Hivyo wabunge wa CCM licha ya kushindwa kutimiza wajibu wao kama wabunge kwa mujibu wa Ibara 63 ya Katiba pia wanashindwa kutekeleza wajibu wao kama Raia wema wa Tanzania kwa mujibu wa Ibara 27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.


(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.

NJIA PEKEE YA WATANZANIA KUJIONDOA KATIKA HALI HII YA BUNGE KUTEKWA NA CCM NA SERIKALI YA CCM NI KUJAZA WABUNGE WA UPINZANI, ILI KUFIKIA LENGO HILI WATANZANIA WANATAKIWA KUPUNGUZA NA KUACHA KABISA UBINAFSI ULIOJENGWA NA CCM WA KILA MTU KUJALI JIMBO LAKE KABALA YA TAIFA. HII ITAWAPATIA WABUNGE NAFASI ZAIDI YA KUSHUGHULIKIA MAMBO YA KITAIFA HUSUSAN KUISIMAMIA SERIKALI ILI IWEZE KUKUSANYA FEDHA ZA KUTOSHA KUTOKA VYANZO MBALI MBALI KAMA VILE MADINI, RASLIMALI, KODI N.K NA PIA KUISIMAMIA SERIKALI KATIKA MATUMIZ YA FEDHA ZILIZOPATIKANA ILI BADALA YA KULIPANA POSHO FEDHA HIZO ZIENDE KATIKA SEKTA ZA MAENDELEO
 
Bahati mbaya ndio hivyo tena Mh. Regia hatunaye tena; ningemwomba akaliulize hili Bungeni katika kikao kilichotarajiwa kuanza leo kikaahirishwa kwa ajili yake - R.I.P.

Hata hivyo, kwa kuwa hili suala la posho linaonekana sasa kuvuka mipaka, na kwa kuwa linaonekana kuwa chanzo kikuu kilichohalalishwa cha ufujaji wa mali ya taifa na hata Naibu Spika Ndugai katuthibitishia hivyo, niwaombe wabunge wote wenye mapenzi mema kwa taifa hili hususan wale wa CHADEMA waihoji serikali iweke bayana viwango vyote vya posho serikalini na mashirika yake, mihimili mingibe na aina ya wafanyakazi wanaofaidi posho hizo.

Waziri wa Fedha atoe majibu sahihi ya kwa mafano kwa miaka mitano iliyopita ni kiasi gani cha fedha kimetumika kulipana posho hizo na ni nini tija yake (posho) kwa taifa. Wananchi tunahiaji majibu ya maswahili haya na mengineyo ya nyongeza kuhusu posho. "Tunamshukuru" sana Makinda, Ndugai na "mgomvi" wake (Sumaye) kwa kutufumbua macho.
 
Mahakamani kuko chokest ile mbaya......ndugai asiwaamushe watumishi wa muhimili huo maana ni eneo ambalo halijui hata haki zake
 
Naibu Spika Jobu Ndugai amedai kuwa watanzania inabidi wasilaumu sana wabunge kuongezewa posho, Ndugai kasema kuwa kuna muhimili mitatu ya nchi ambayo niBUNGE, SERIKALI NAMAHAKAMA, Ndugai kasema kama watanzania wangejua ni kiasi cha posho kubwa wanacholipwa viongozi wa seikali na mahakama basi watanzania wangejinyonga kabisa badala ya kulaumu hizi wabunge ambacho ambacho kadai kuwa ni kidogo kuliko wananchi wanavyofikilia,

Hii kauli ya Ndugai ilimshitua hadi mtangazaji baada ya kusikia kuwa nchi hii kuna zaiudi ya maefu ya wafanyakazi wanapokea posho za kutisha kuliko hata wabunge, Ndugai kadai wabunge ni wafanyakazi wasiozidi hata 350 lakini ndoo wamenyooshewa kidole na waandishi wa habari bila kufahamu kuwa kuna posho zinalipwa mara 10 zaidi ya hizo zao kwa siku na kudai kuwa ni maelfu ya wafanyakazi wa mihimili ya serikali na mahakama na hii ndoo imefanya hadi wabunge waamue kujiongezea.

Huyo ndoo Ndugai kaamua kutoboa siri iliyojificha, ama kweli kumbe wafanyakazi wanaweza kulipwa kima cha chini kisichopungua 350000, hapa ndoo nimeamini baada ya Ndugai kumwaga mboga,.
Nimeamini kuwa ni kweli mwendawazimu anaweza kuonekena ni mwenye busara pale anapoamua kukaa kimya na asipofanya hivyo ndipo utapobain kuwa kumbe huyu mwenzetu hamnazo. Huyu jamaa kaamua kujiacha uchi kwa kiherehere cha kutaka kuonekana anajua kuongea. Sasa hii ndio aina gani ya ujengaji wa hoja???huyu anafedhahesha sio tu wabunge waliompigia kura za kuwa naibu spika, bali hata wapiga kura wake huko jimboni. Na ndo maana tunasisitiza vijana wengi waingie kwenye siasa na kuchukua majimbo haya mana naona waliyoyashika wameanza kujamba hadharani.

Kwanza sidhani kama yupo sahihi na anafanya wananchi hawaelewi wanazungumzia nini ktk hoja nzima ya posho tunazozipigia kelele. SISI TUSICHOTAKA KWAO KWANZA NI POSHO AMBAZO NI DOUBLE PAYMENTS, Pili tunataka mfumo mzima wa posho uangaliwe upya. Sasa sijui huyu mpuuzi anaongea nini. Nchi imepigika, watu wapo choka mbaya mambo hyaendi yeye anaongea utumbo. Hawa ni wakuwaezeka makofi kama wezi wengine tu.
 
Tumsupport Job Ndungai atoboe zaidi ni posho kiasi gani kinalipwa kwenye muhimili wa serikali.
Vita vya panzi neema ya kunguru. Acha watoboleane siri ili tuwabane wote vizuri. Afterall, it is all our tax money inayolipa hayo yote.

Bwana Ndunga: tafadhali fafanua in details hizo posho za serikali.
 
Back
Top Bottom