Dakika 45 ITV: Jobu Ndugai apasua siri jinsi nchi inavyofilisiwa na serikali iliyoko madarakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dakika 45 ITV: Jobu Ndugai apasua siri jinsi nchi inavyofilisiwa na serikali iliyoko madarakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Jan 16, 2012.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Naibu Spika Jobu Ndugai amedai kuwa watanzania inabidi wasilaumu sana wabunge kuongezewa posho, Ndugai kasema kuwa kuna muhimili mitatu ya nchi ambayo niBUNGE, SERIKALI NAMAHAKAMA, Ndugai kasema kama watanzania wangejua ni kiasi cha posho kubwa wanacholipwa viongozi wa seikali na mahakama basi watanzania wangejinyonga kabisa badala ya kulaumu hizi wabunge ambacho ambacho kadai kuwa ni kidogo kuliko wananchi wanavyofikilia,

  Hii kauli ya Ndugai ilimshitua hadi mtangazaji baada ya kusikia kuwa nchi hii kuna zaiudi ya maefu ya wafanyakazi wanapokea posho za kutisha kuliko hata wabunge, Ndugai kadai wabunge ni wafanyakazi wasiozidi hata 350 lakini ndoo wamenyooshewa kidole na waandishi wa habari bila kufahamu kuwa kuna posho zinalipwa mara 10 zaidi ya hizo zao kwa siku na kudai kuwa ni maelfu ya wafanyakazi wa mihimili ya serikali na mahakama na hii ndoo imefanya hadi wabunge waamue kujiongezea.

  Huyo ndoo Ndugai kaamua kutoboa siri iliyojificha, ama kweli kumbe wafanyakazi wanaweza kulipwa kima cha chini kisichopungua 350000, hapa ndoo nimeamini baada ya Ndugai kumwaga mboga,.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ndugai nae namlaumu kwanini asingekemea,at the same time angeacha 70 elf itumike?so it meanz that nao wanataka wawe kama wa juu
   
 3. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hako kabwana kaongo tu. Kanajikosha kwa lugha nyepesinyepesi tu. Halafu eti anamwita Mhe. Sumaye kaka yangu. Ama kweli sasa nimeamini kuwa wanasiasa wetu ni wanafiki wakubwa sana. Anachofanya Ndugai ni mwendo mdundo wa KUCHUMIA TUMBONI unaofanywa na chama cha magamba. Anaongea kitu ambacho hata nafsi yake inamsuta lakini anaendelea tu. Ndiyo maana haitatokea na wala sitarajii kwa namna yoyote ile iwayo kujiunga na chama kinachojiita ccm.
   
 4. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Mwishoni kashauli kuwa inabidi katiba ijayo kiwekwe kipengere cha tume maalumu ya kuunda posho na mishahara ili wabunge wasiwe na gape kubwa sana na hii mihimili mingine ambayo ni serikali na mahakama.
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kahiyo hoja ni kwamba Bunge sio wahujumu pekee. Je swali ni kwamba kiwango wanacholipwa wabunge ni haki kwa nchi masikini kama Tanzania?
   
 6. A

  Anizetha Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makubwa bado tutasikia mengine kwahao wanaolipwa posho marakumi zaidi ya wabunge
   
 7. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Mbona sisikii mtu akimzungumzia mwananchi wa kawaida? Mihimili... mihimili...
   
 8. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugai asifananishe majaji na wabunge, majaji ni proffesional wakati wabunge ni siasa tu mdomoni. kweli ccm imekuwa kila kiongozi ni kambale, mtoto ana ndevu, mama ana mdevu na baba ana ndevu. hakuna kuheshimiana.
   
 9. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tanzania yetu kweli imeisha, but its true fikiria posho wanazolipwa watumishi wa umma wa foreign affairs na idara zingine inapotokea wamesafiri na mh rais nje ya nchi. na kama mjuavyo safari za mkuu wa nchi
   
 10. k

  kakapeter Member

  #10
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninachokiona mimi mpaka sasa ni kwamba uwezo wa kujieleza na kujenga hoja wa hyu mnayemuita mheshimiwa ni duni sana,kwamba wengne wengi wanatenda kosa haijustify hilo kosa.Yeye amekuwepo bungeni kitambo,hizi posho za serikalini na mahakamani kama ni kuzifahamualizifahamu zamani na ilikuwa ni wajibu wake kama mbunge kuhakikisha zinasitishwa.Sasa yeye kwa uelewa wake anaamini tutakubaliana na posho zao kwa vile tu mijizi mingine serikalini na mahakamani inachukua posho kubwa?Basi kila Mtanzania apewe hiyo posho,I guess hii nchi ina hela nyingi kuliko mambo ya msingi tunayoweza kufanya otherwise sielewi watu bila huruma mnagawana tu kodi zetu and you are not even ashamed to stand and justify it!Hii kodi ninayolipa inaniuma saaaaaana,kiungwana ilibidi hawa watu waone aibu washindwe hata kusimama kwenye media kutetea hili ila wao waaaaaala...f**&@K them all
   
 11. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Kwa hiyo ukimwona jambazi anapora na wewe unakuwa jambazi ili upore? Ujinga. Nyie kuleni hela za wavuja jasho wasio kula jasho lao, Mungu hawezi kusamehe upuuzi huu. Hivi hakuna kiongozi hata mmoja serikalini mwenye akili timamu?
   
 12. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Job Ndugai kanisikitisha.
  Nae anaingia kwenye orodha ya magamba yasiyofaa kuwa viongozi wa uma.
  How the hell did he become a deputy speaker?
  OTIS
   
 13. k

  kiche JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sisi watanzania wengi wetu ni wendawazimu (samahani kwa lugha kali!inauma) inawezekana vipi mtu anaongea upumbavu wa aina hii bado anapeta kutuongoza!!?si ajabu 2015 utasikia amepita bila kupingwa achilia mbali kushindwa kwa kura!tumeziweka wapi akili zetu?inauma sana na si ajabu utashangaa anajitokeza mtu na kumtetea ndugai au mtu anampinga mtu anayemkosoa huyu pimbi!!inamaana viongozi wetu wamefikia katika kupambana kuwa ni nani anakula zaidi badala ya kusema nani anawajibika zaidi katika kuwaletea wananchi maendeleo!!!??

  kidini wanasema kila serikali inawekwa na mungu!!lakini hapa ndipo napochanganyikiwa kumwelewa huyu mungu,mbona ametutenga kiasi hiki??ni kosa gani kubwa tulilofanya watanzania mpaka atuadhibu kiasi hiki ?watu hawajitambui!!mambo ya wazi watu hawaoni!! (kumbuka wana wa israeli walikuwa wanapata mapigo kwa kujitenga mbali na mungu) naomba nisije nikakufuru ila lililo kweli ni kwamba sasa ni wakati wa mungu kutupa hekima kufanya maamuzi sahihi,sasa kauli za kipumbavu toka kwenye viongozi wetu limekuwa jambo la kawaida kwa sasa!!!,wanapambana kutoa kauli utafikiri kuna tuzo wanazogombania,tunakwenda wapi watanzania!!!??

  Kwa sasa kuna kamsemo kamoja kameibuka kutetea wizi ambapo mtu ukihoji ubadhilifu unaambiwa hayo ni majungu au wivu na unaambiwa toa kauli za maendeleo si hizo!!hivi kweli unaweza kupata maendeleo wakati pesa za kuleta maendeleo zinateketezwa kwa namna hii!!ni mwendawazimu tu ambaye anaweza kuendelea kusomba maji kwenye mtungi wakati ukiwa umetoboka
   
 14. z

  zamlock JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  nimemshanga sana na inaonyesha upuuzi huu wanaufanya kwa makusdi ajui hata anachokizungumza unajua kuna siku kaka yangu aliniambia hata jobndugai kawa mbunge tena naibu speaker nikasema kwan vp akanijibu basi kumbe hata mimi naweza kuwa kiongozi safi kama kweli huyu bwana amekuwa kiongozi tena mkubwa nikabaki nimeduwaa sasa leo ndo nimeamini huyu ndugai uwezo wake ni mdogo sana wa kujenga hoja
   
 15. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Hili suala ni la kuangaliwa katika ngazi zote na busara ni kupunguza posho sio kuwaongezea kundi moja lifanane na jingine.

  halafu anasema wafanyakazi wa bunge hawazidi 350, majaji wapo wangapi kwani au hadi 'mahakimu' wa huku kwetu mahakama za mwanzo wanapata hizo posho?

  Kwanza wabunge ni wawakilishi wetu na hakuna mtu anayelazimishwa kugombea, wenzao ni watu na fani zao walizosomea na wametumika sana mpaka kupata hivyo vyeo.
   
 16. k

  kiche JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati ulifika nikataka kukichukia kipindi hiki kwa vile kilionyesha kama vile ni jukwaa la viongozi kutetea upuuzi,sasa nimeanza kuelewa umuhimu wake kumbe ni kweli kabisa ukitaka kujua upumbavu wa mtu mpe nafasi aongee,naamini tutashuhudia mengi.
   
 17. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Very dissapointed!!!
   
 18. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Magamba Matatu(3) na Wana JF,
  Hii ndio tatizo la Wabunge wa Chama Tawala kuwa wengi na kupitisha kila kitu hata kama kibaya, kuna haja ya kuwa na Wabunge wengi wa Upinzani watakaoleta Ushindani wa Hoja. Huu ni Uoga wa hali ya juu, Mh Ndugai kwanza ni mzoefu wa miaka mingi, anajua kinachoendelea ana cheo cha Unaibu Spika, sasa atashindwaje kukemea na kubadilisha mambo yote yasiyokuwa na tija na Taifa letu, au analinda kibarua chake ?? Anataka kujisafisha kuwa wao Wabunge wanalipwa kidogo kuliko mihimili mingine yaani Serikali na Mahakama ?? Tuacheni Siasa za kinafiki, tujenge Nchi yetu.
  My Take: Tunamtaka Mh Ndugai atuambie Mahakama na Serikali Viongozi wao wanalipwa Posho Tshs ngapi ?? Ili wananchi ambao ndio wenye Nchi tuamue !!! otherwise Samaki mmoja akioza wote wameoza. Sipo Upande wowote haya ni Maoni na Mawazo yangu tu
  Nawakilisha
   
 19. C

  CHIEF MGALULA JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 782
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 80
  mungu aailaze mahala pema regia mtema,ninakukumbuka wakati leo tunakuaga mpendwa wetu huyu mgogo Bw.Ndugai anatuzidishia majonzi
   
 20. Rumishaeli

  Rumishaeli JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 225
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mungu aturehemu!
   
Loading...