Daftari la Wapiga Kura Arusha Lachakachuliwa

Daftari la Wapiga Kura Arusha Lachakachuliwa

Thats why kuna thread nilimuuliza Mungi wanayo taaarifa na mipango ovu inayoendelea Arusha?!!
kuna mipango mibovu kati ya ccm,tume ya uchaguzi na Polisi kwa ajili ya kuhujumu uchaguzi wa Arusha
na polisi watakaosimamia wameagizwa wasithubutu kusema au kufanya lolote siku hiyo kwa watakachoona'
 
Waheshimiwa wanajamvi kwa sasa ninaweka habari hii hapa kama tetesi kwa malengo mawili:
1. Kuwafanya wahusika wajue kuwa hila zao zimeshajulikana.
2. Kufuatilia zaidi nyendo za wahusika na hatimaye tulete updates hapa hapa jukwaani.

Jana nilipata habari kutoka kwa chanzo muhimu cha ndani kabisa kwa,ba maofisa wa tume ya uchaguzi wameelekea jijini Arusha kwa lengo la kwenda kurekebisha daftari la kudumu la wapiga kura kwa kata nne zenye uchaguzi.

Maofisa hao ni pamoja na makarani wa kupiga picha na wajuzi wa IT. Imepangwa wafanye kazi hiyo hadi Jumanne tarehe 2/7/2013. Kama mpango wao huo ukifanikiwa Tume inaamini kwamba kwa kila kata kutakuwa na rekebisho la walau 38%. Hili rekebisho litakuwa kura za msingi za kuipa CCM ushindi kwa kata zote nne.

Nikiwa bado natafuta habari zaidi naomba nitoe kwa muhtasari maeneo yatakayorekebishwa.
1. Watu wote walioondoka Arusha ama kwa kufariki, kusafiri au kuhama mapengo yao yatazibwa na wapiga kura maalum watakaopewa shahada kwa ajili yao.
2. Wapiga kura wanaojulikana wazi kuwa wa CDM watafuatwa kwa malengo ya kuombwa wauze shahada zao, wengine zitaibiwa na wale wagumu kabisa watawekwa rumande siku za kuelekea uchaguzi mdogo.

Wakubwa serikalini na ndani ya CCM wanahitaji ushindi Arusha mjini kwa udi na uvumba hivyo kama wakigundua mbinu zao za ushindi zimegundulika ama kwamba zitagonga mwamba wataahirisha tena uchaguzi kwa kisingizio cha usalama.

Hadi sasa jeshi la polisi linapangwa kwa ajili ya kupelekwa Arusha kwa lengo la kusaidia utekelezaji wa mbinu hizi za kihuni za CCM kwa kisingizio cha kuimarisha usalama.

Stay tuned!!


Kwa haya yanayoendelea kwa sasa katika nchi hii yenye Utawala tumekuwa tukitawaliwa muda mrefu sana.Inawezekana pia hata mkuu wa nchi hii anaetawala hakuchaguliwa kihalali kama tunavyoaminishwa na Tume ya Uchaguzi ya Tanzania.Ninawaomba viongozi wa Chadema mmpeleke nguvu kubwa sana Arusha bila kujisahahu msisahau pia kuchukukua tahadhari sababu Polisi watatumika sana katika kufanya hujuma.Nnasisitizia tena CCM kama Serikali italitumia sana jeshi la polisi kufanya hujuma katika uchaguzi huu,sababu katika kitabu cha mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali kimeainisha upotevu wa bilion of money katika manispaa ya Arusha.
 
Mbeya Mjini walijalibu kufanya kitu kama hiki ktk kata ya Iyela
Tulichofanya ni kuutangazia umma, kua ambaye c mkazi wa Iyela asithubutu kupiga kura.

Mawakala wote wa Cdm wa lipewa daftari la mwaka 2010.kila aliyeingia aliangaliwa ktkt daftari lile.iliangsliwa jina,namba ya kitsmbulisho na picha.Kama mtu alikosa kimoja kati ya hivyo HAKURUUSIWA KUPIGA KURA.
 
Hukunielewa tu ndugu,soma post yangu vzr,HILO LA WIZI WA KURA NDILO WANALOLITEGEMEA MAGAMBA NA CUF NA KWA KUJIFANYA HAWAUONI UPEPO UNAVYOVUMA wanadanganyana eti CHADEMA hawana chao.
samahani mkuu,unajua hawa jamaa wa magamba wanatia hasira sana, wana macho lakini wanajifanya hawaoni,wanamasikio lakini wajifanya hawasikii. tuko pamaja kamanda
 
vijana wa lumumba project wakiongozwa na hammy d,simiyu and the like wameitana lumumba kuona wacounter vipi hili bandiko

Hawana nafasi leo wameshavalishwa mashati mapya tayari kwenda kulamba viatu vya mgeni!Subiri pilika zikiisha utawaona mbio kama wametoka kujisaidia kichakani!
 
safi sana mkuu kwa hizi habari zimulikwe mapema kujua wananchotaka ni nini hasa .
 
Kimsingi tusipuuze ujumbe alioleta mdau,pamoja na wadau kuendelea kwenye key board tuwe na njia mbadala kwenye ground maana kupata tetesi kama hii na kutoifanyia kazi ikitucost itakuwa uzembe mkubwa sana.jambo jingine wakazi wa Arusha watambue siku ya uchaguzi yanaweza kutengenezwa mazingira yasiyo rafiki kiuchaguzi mfano-uwepo askari wengi kupita kiasi na silaha ili watu waogope kujitokeza kupiga kura.Jitokezeni kwa wingi na pigeni kura.
 
samahani mkuu,unajua hawa jamaa wa magamba wanatia hasira sana, wana macho lakini wanajifanya hawaoni,wanamasikio lakini wajifanya hawasikii. tuko pamaja kamanda

Wataelewa tu siku yao ipo,pamoja tutafika.
 
Back
Top Bottom