hili ndio tatizo letu hatuangalii wapi lipo tatizo, unapoanguka usitizame ulipoangukia tafuta nini kilikufanya kuanguka,
Kwani ndio hao tu wanaofanya hiyo biashara walao wao wanafanya kwa malipo ya pao hapo kula Dodoma kulikuwa na kashfa ya wake wa wabunge kulalamika waume zao wana nyumba ndogo mbona hatukuona picha zao hapa?
Hii sio tabia nzuri na aibu hata kwa hao dada poa ndio unawaona wakifunika sura zao kwa aibu lakini hawana namna ya kipato kwa hapa mjini isipokuwa hiyo wameshindwa na njia nyengine,
Kule vijijini tunawaharibia njia zote za mapato ikiwa pamoja na serikali kushindwa kuekeza mitaji na elimu ya kusaidia maendeleo yao
Tumeona gesi inatolewa Mtwara na kuletwa mjini DSM jee kula Mtwara tumewasaidia nini? na rasilimali ya kule tunaileta huku? Madini yote yametaifishwa hata wale wachimbaji wadogo walio wakaazi wa vijiji vinavyotoka madini yale wametimuliwa maeneo yao, wao wakale wapi?
Huo ni udhalilishaji wa raia wa kawaida walioshindwa na maisha na kutafuta njia mbadala iliyongumu kueza kujikimu na maisha,
Kama serikali inawajali hao watu basi iwape elimu na msaada wa maarifa na mitaji ya miradi kueza kujikimu na wimbi la kupanda kwa maisha vyenginevyo ni kuwaonea