Dada zangu nawapenda lakini mnakera sana

Twin_Kids

JF-Expert Member
Feb 25, 2016
3,451
5,370
Sisemi kwamba watu ambao hawajaenda shule au kukaa kwenye society ya watu wengi tofauti tofauti siyo watu, lakini ni wazi watu ambao hawajaishi maisha hayo wana taabu sana.

Japo na wanaume wapo, mtu akikuchekea, akaonyesha wewe ni mtu kama wengine, humjui vizuri, una tatizo amekusaidia, unaanzaje kumsema kwa watu kwamba anakutaka kimapenzi?

Badilikeni, bila kuishi na watu kwa ukarimu maisha hayajaenda. Kwa hiyo si kila anaekuongelesha anakutamani
 
Hivi kwa nini siku hizi watu wengi hawajui wapi pa kuweka "l" na wapi pa kuweka "r".

"Mnatukera" wanaandika "mnatukela" kama wote watoto wa Magufuli?

Mimi hawa wananikera pia.

cc FaizaFoxy

Mkuu,hongera sana kwa kunikosoa,lakini pia kumbuka JF imekuwa mzazi wa mataifa mengi siyo Tanzania tu! Nadhani umenielewa sasa
 
Mkuu,hongera sana kwa kunikosoa,lakini pia kumbuka JF imekuwa mzazi wa mataifa mengi siyo Tanzania tu! Nadhani umenielewa sasa
JF imezaaje mataifa? Na mataifa hayo iliyoyazaa JF yanaitwaje?

Na nani kasema Watanzania hawana hili tatizo?
 
inategemea na ukaribu ulioonyesha... yaan hata kama ni friends tu kuna mambo mengine ukifanya lazima mtu ashtuke... BTW wengi ambao minara yao ya kichwan haijakaa sawa ndo wanatangaza!!!!
 
inategemea na ukaribu ulioonyesha... yaan hata kama ni friends tu kuna mambo mengine ukifanya lazima mtu ashtuke... BTW wengi ambao minara yao ya kichwan haijakaa sawa ndo wanatangaza!!!!

Mkuu, hasa wale ambao hawajaishi kwenye makundi makubwa ya watu ndo wana katabia hako.Ndo aina ya watu wakiona mwanaume kaingia kwa mwanamke,bila kujali wana uhusiano gani,taarifa zitasambaa mtaa mzima kuwa furani kagegedwa.
Ila kwa msemo wako wengine minara ya kichwani haijakaa sawa
 
mkuu unajua wengine wanakuwa wanatamani hiyo nafasi sasa akiona unachelewa na tayari kuna ka'ukaribu anaona bora yeye alianzishe kwa style hiyo..!!!!
 
mkuu unajua wengine wanakuwa wanatamani hiyo nafasi sasa akiona unachelewa na tayari kuna ka'ukaribu anaona bora yeye alianzishe kwa style hiyo..!!!!

Mtu unakaa nae mji mmoja(wapangaji),unajua umeoa, umewasha ki Vtz chako,anaomba lift, kakaa anaomba elfu mbili tu! Kiato cha walinzi unakijua,umempa, af umeuchuna maana hata kama ni kuchepuka nadhani siyo kila mwanmke unaweza chepuka nae! Badae taarifa mtaano kwamba ulimtaka akakataa! Aibu jamani!
 
duuuh.. huyo alitaka kukuharibia tu...!!!!
kuna rafik yangu alikuwa anachatishwa na demuflan hv kitaa... yaan demu anamwingizia swaga za kimapenzi kwa sms.. mwisho yuke demu akachukua zile sms zote aka'foward kwa mke wa yule rafik yangu... kilinuka nakwambia.. nikamwambia shem kuna mademu shida yao kuharibu tu nyie potezeeni !!!!
 
Umesema kweli mkuu! Inatokea sana kwa wadada... Mkaka akiwa mkarimu au mwema kwako unaanza kufikiria au ata kutangaza kua anamtaka kimapenzi!
Mimi nadhani sababu ni kwamba experience inaonesha asilimia kubwa ya wanaume wanafanya hivyo kwa lengo hilo...
Mda mwingine mdada nae anakua too desperate kutaka mapenzi au anajistukia tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom