DADA YENU MAPENZI YAMENIKABA KOO

DADA YENU MAPENZI YAMENIKABA KOO

Pole sana.
Kwa maelezo yako tu inaonyesha mtu halisi wa kuja kukuoa bado hajatokea, hao wote uliojaribu ni wahuni wa kawaida sana. Hawakuwa na mpango wa kukuoa zaidi ya kutaka kula mzigo tu.

Ushauri wangu, kwa sasa wewe tulia tuli, usiwe na haraka wala papara. Msimamo wako ndio silaha yako, ng'ang'ania hapo hapo. Maana tupo wanaume tunaopenda kuoa wanawake wenye misimamo imara kama hiyo. Ipo siku tu, kama ipo ipo tu.

Kwa umri wako na msimamo wako viko sawa kabisa. Jambo moja tu ambalo silijui ni muonekano wako. Kwa leo naishia hapa.
 
Habari za weekend wanajamvi..

Mimi ni member mzoefu,nmeona nitumie ID mpya ili niwe huru zaidi kujielezea...nmefikwa kooni nahitaji ushauri

Mm ni mtu mwenye msimamo wa dini na nina misimamo yangu ya maisha,nashkuru Mungu nimesoma vzuri na nina kazi nzuri... (sio slay queen)..Anyways,,binafsi kwa mara ya kwanza kabisa nmeanza kujihusisha na mahusiano nilikua chuo mwaka 2 kuingia wa3...(field),,,Nilikutana na kijana na hapo ndio ilikua mwanzo wa mahusiano na mwanzo wa hata ku-kiss
Mahusiano yale yalidmu miezi kadhaa na nliyaacha baada ya kugundua yule mwanaume hakuwa wa dini yangu (alinidanganya dini)...na mm mtu wa hvo naona hatutafika mbali na mm sipendi kua na mahusiano yasio na future....uzuri ni kwamba sikusex nae

Sikujihusisha tena na mahusiano mpka nkamaliza chuo,nkawa kitaa nasaka ajira...nikakutana na mkaka wa makamo,,nikaona at least huyu age yake imeenda labda kweli anataka ku-settle down...
tulikaa kwenye mahusiano kwa muda wa miezi kama 7..huyu kaka nilimkuta na watoto wawili wa mama tofauti...mama wa mtoto wa kwanza alishaolewa,ana familia yake..mama wa mtoto wa pili walikua wameachana na huyu kaka alikataa mimba (kwamba hawakua na makubaliano ya yule dada kubeba mimba ila m.ke aliilengesha)...

Ukweli huu alinambia mwanzo kabisa akiwa ananitongoza,,basi me nkajua ntaweza yavumilia,,mahusiano yetu yalikua mazuri lakini likija swala la kuombwa mechi me nkawa nakaza..jamaa akawa ananiambia sasa tutakuaje kimahusiano kama kaka na dada?!,,,nkamwambia mm siwezi kulala na wewe... (siamini katika sex before ndoa)...akawa ananambia inabdi kwanza nizae au kama nikunioa basi niwe na mimba ila yeye hawezi uziwa mbuzi kwenye gunia...tuliendaaaaa ikafika point nkaona kabisa haya mahusiano nayalazimisha!,basi kila mtu akashika shughuli zake...

Akawa ananitafuta siku moja moja (hakutaka kuamini kweli naweza mkatalia kusex),basi tukionana hakuna jipya msimamo wangu ni ule ule..

Nkapata kazi nkapangiwa mkoa wa mbali na jamaa,,mawasiliano yetu yakaena yakawa yanafifia kabisaa..ila akawa kila akija mkoa niliopo ananitafuta (nature ya kazi yake anasafiri sana)..

Nkamwambia yaan wew siku zote huniuliziagi ila mpaka uje huku...anazuga na sababu zisizo za msingi..

Siku moja nkaona amepost picha ya mtoto (nikajua ni yule mtoto aliemkataaga),,kama vile wameelewana na yule mzazi mwenzie...basii siku aliokuja mkoa niliopo,,nkamuuliza akasema mm nmefata mtoto ila yule mwanamke sijarudiana nae...lakn yule mwanamke anacoment kabisa kwenye picha zake mara mume,mpenzi,kiboko yangu n.k....ikifika birthday ya m.ume mdada atajishughulisha cake na mazawadi kedekede...

anakuja huku nilipo anakataa hawajarudiana ila inta unaona yule mwanamke na the guy wameenda trip zanzbr na mtoto...hio siku nikanyanyua mikono juu nkasema hapa sina hata matumaini..nkawa mkali kwa jamaa nkamwambia tafadhali naomba ukija huku nilipo fanya yaliyokuleta usepe...nkawa mkali...nkafuta namba zake...akawa hata akinitext whatsapp simjibu!

sasa nkakaa kama miezi 8 au 9..nkajaribu mahusiano mengine...nafs yangu inakua ngumu kumuamini mwanaume tena!,naona uongo umezidi kiasi kwamba huyu mwanaume akanambia mm sionyeshi kumpenda na sina feelings nae (kilichoni dissapoint kwa huyu kaka ni na yeye ana watoto na hakuniambia before...)na mm nkapunguza mawasiliano na last week tukaachana kabisa..baada ya kujua ana watoto mzuka ule wa mahusiano ukafa..sitaki baby mama dramas

Nafsi yangu kusema ukweli ilimpenda sana sana sanaa huyu kaka mwengine ambae amaerudiana na baby mama wake (na hawaezi oana dini mbalimbali kabisaaaa),,...ila mwanamke sa hvi ni mjamzito anazaa mtoto mwingine baada ya miaka 8

Nafsi yangu ina maumivu makali sana jaman,nifanyaje nisahau na niweze move on?,!,yaan nmeshalia sana sana kwa Mungu wangu,kumuomba aniwezeshe nisahau jaman...

Nisaidieni wanajamvi..ni kweli kabisa siwezi pata mwanaume atakaekubali mvumilia mwanamke mpka amuoe?!,, Nahisi subira yangu ya kujitunza uanamke wangu inanishinda (Im 26 now)...,

Na pili huyu mwanaume namtoaje akilini jaman?!...

NB::: comments ntazisoma kupitia account yangu ya kawaida hapa nimemaliza...nmetumia hii ili nijimwae mwae...
So Dada wa jf huja sex mpka sasa kwa sababu bado hujaolewa ?


Halafu tafuteni normal guys like ME huwa ndo wana settle down
 
Njoo PM Kuna kitu nataka kuhakikisha kutoka kwako...Hakika huto jutia maamuzi yako ya kunifuata Pm
 
Nikuambie tu ukweli kwa jinsi unavyocomplicate mshusiono kwa kulazimisha ndoa na kugoma kutoa nyapu jiandae tu kuwa single maza maana hakuna namna nyingine
 
shida yako hutaki kutoa mechi ukitoa mechi hutojuta tena anyway njoo dm tuyajenge
 
Hiyo kitu ya kuwa na mahusiano bila kuonjana asee dada yangu endelea kusali.
Ila kwa sisi wanaume ni ngumu sana. Yani kirahisi rahisi naona Mwanamke bila kumvua pichu.!!?
 
HUWEZ OELEWA WEW,Mara nying madem kama nyinyi mwisho Wa sku uolewa na wahuni(walevi,wavuta bangi,jobless)
 
Kuna jamaa mmoja yupo Twitter,anajiita kigogo.anatumia Avatar kama yako,,,hivo nikiiona hyo Avatar yako najua ni yeye
Yap,nafahamu hiyo account Mkuu, na hii Avatar niliichukua kwake baada ya kuipenda!
 
We mshamba,,,ila samahan kwa kukwambia neno hilo...utawezaje kukaa na bikra miaka yote hiyo....narudia huo ni USHAMBA...kama sio ushamba basi utakuwa Matatizo kweny mwili wako si bure...
 
Kuzaaa na mtu mara nyingi hutokea unplanned. Cha msingi ni msimamo wa mpenzi wako. Na kukubaliana nae.
Kumsahau its just maamuzi na kuitune mind yako kusahau itasahau. Ndio utamkumbuka but jitaidi kutomtext,kumpigia wala kumtafuta
 
Back
Top Bottom