Dada una sura nzurii.....

Dada una sura nzurii.....

Ngoja namimi nikusifie, maana ushasema angekuwa mkaka ungempa namba yako ya simu... We mdada unangozi nzuri, shingo ya kuvalia cheni, tabasam maashallah.. kweli Mungu kakuumba
 
Uwe makini na sifa kutoka kwa mwanamke mwenzako, wengine ni madume jike!
 
View attachment 702207 Kasie Mahaba.

Habari zenyuu,

Ndo naingia home hapa SA hooii,sasa nikiwa migration section pale airport iki nigongewe kuwa nimerudi nchini salama, nikamkabidhi passport yangu (aliyekuwa ananihudumia ni mdada).

Baada ya kuniuliza maswali kadhaa akaniambia niangalie camera, weka finger prints akagonga muhuri kwenye passport halafu akafungua ukurasa wenye taarifa zangu kuangalia mwaka wangu wa kuzaliwa na nilivyo..

Akanitazamaaa huku akiwa ameshikilia passport yangu kwa sekunde kadhaa. Aka tabasamu huku akisema.. Dada una sura nzuri. Sikutegemea usemi ule hasa kutoka kwa mdada. Nikajikuta natabasamu kuanzia pale nia nzima hadi home. Nikamwambia asante kisha nikachukua passport yangu huyo nikakamata Gautren hadi Sandton kisha nikachukua uber hadi home.

Njiani nikawa najiuliza..... kwani huyu dada kaniambia nina sura nzuri.....

Update:

Mara nyingi watu husema wadada ni ngumu sana kusifiana yaani huwa tunaoneana wivu. Lakini huyu dada kwa tabasamu alilotoa niliona alimaanisha kunisifia aidha kwa kulinganisha umri na sura akaona sura bado ina ahueni japo umri umeenda.

Najua wako ambao wanasifia kwa unafiki ile mtu anakwambia Umependeza wakati uko kama kituo. Kama kawaida yangu nilikuwa kawaida tuu sikuwa na makeup yoyote usoni zaidi ya lipstick na wanja. Huyu dada sifa yake haikuwa ya kinafiki tabasamu lake lilisema yote.

Kingine nikaona kuwa kweli wadada tunalewa sifa, wallah angekuwa mkaka ndo kanisifia ningempa namba yangu ya simu hehehehe.

Sio siri wadada tunasikia raha sana tukisifiwa hasa sifa ikiwa ya ukweli.... yaani hadi sasa kila nikiwaza natabasamu.

Kasie Kiuso hehehehehe.

Heeey, sijaweka huu uzi kujisifia bali nimeelezea kilichotokea. This pic below is real Kasie ..... nimeipiga lini jibu kwenye mabano hehehehhe

View attachment 702209

Kasie Mahaba.


Pengine huyo dada ana matatizo yake tu binafsi, mi nakuona ni wa kawaida sana wala sioni uzuri wako.
 
So pretty!!
0758c962542d10090724e8981fe3f6db.jpg
 
Nataka nikiwa mkubwa niwe kama wewe, wewe ni mzuri shemeji anafaidi wallahi
 
Pengine huyo dada ana matatizo yake tu binafsi, mi nakuona ni wa kawaida sana wala sioni uzuri wako.
Acha bhana!
Mwanamke mtu mzima anaelekea kwenye 50' zake, kuwa na babyface namna hiyo ni majaaliwa yakhe.
Wengi wenye umri wake, sura zao zilikwishakuchuma kunde tayari.
Huyo anajitunza, anafanya mazoezi na hana matumizi mabaya ya mwili wake zaidi ya sex, diet na love kwa raha na afya.
Kwanini akongoroke!
Wenziyo zaidi ya wawili ukisikia wakisifia kwamba fulani ni mzuri,waunge mkono kwa kusema 'ndiyo afande', maana saazingine jicho lako laweza kuwa na husda, linakunyima ushirikiano kwa kuuona uzuri (urembo) wa huyo dada mtu mzima.
 
Kumbe ndiyo maana nasikia Wazaramo wakiona mnyamwezi hukosa pumzi na kuwa wapole ghafla sana.
Pamoja na pyepyepye na tantarila zao, lakini kwa Mnyamwezi ni kiboko chake na huwa anaufyata na kuwa mdogo kama tembe la pilton.
Sasa sielewi undani wa simulizi hii unatokana na mishepu ya Kinyamwezi, ana nini hasa!
Embu Kasie tupe hint kidogo kuhusu hilo.
 
Ngoja namimi nikusifie, maana ushasema angekuwa mkaka ungempa namba yako ya simu... We mdada unangozi nzuri, shingo ya kuvalia cheni, tabasam maashallah.. kweli Mungu kakuumba

Hahahahhaa looh usijali ntakutumia namba yangu.
 
Pengine huyo dada ana matatizo yake tu binafsi, mi nakuona ni wa kawaida sana wala sioni uzuri wako.

Uko sawa kabisa, macho yake si yako. Mke mwenyewe alinishangaza ila kwa kuwa wadada huwa tunasikia raha kusifiwa..... basi alinipa tabasamu mwanana usoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom