Dada mtu anamtafutia wifi yake bwana

green rajab

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
11,305
35,852
Katika hali isiyoendana na maadili yetu ya Kiafrika Best angu kaja kunipa story kua mke wake alienda kumsalimia wifi yake ambaye dada wa best angu dukani kwake katika mazungumzo yao wifi akaanza kuelezea maisha yake ya ndoa na mumewe ambaye wameoana muda tu na wajaaliwa kupata watoto wa 3 ila kaamua aanze kuishi maisha ya kuchepuka na mabwana wa pembeni makusudi ili apate tulizo la moyo.

Ndipo alipoanza kumshawishi mke wa jamaa nae atafute bwana wa pembeni hatapata stress yoyote ya mapenzi.

Jamaa baada kuambiwa hatua aliyochokua ni kuondoa ushirikiano wa aina baina yake na dada yake na amempiga marufuku mke wake kukanyaga tena huko. Hizi familia zingine kwa kweli ndugu hawapendani kabisa.

mchepu.jpg

Mtu hawezi kuibuka tuu kukupa ushauri wa kutafuta mchepuko wa kukutuliza moyo kama hajui moyo wako haujatulia?! Hao ni mashosti na lazima wanajuana na wanajua jinsi ya kukukama

green rajab Inawezekana kabisa huyo mke wenu anachepuka haswa sasa anahitaji kujisafisha

Poleni mwayego
 
Huyu mke wetu anasema yeye alimuambia amekuta meseji za wanawake kwenye simu ya best angu sasa akawa anamdisia wifi yake ndio akakutana na ushauri huo wa kubomoa
 
Huyo mwanamke Ni mchonganishi. Katunga uongo ili awagombanishe mtu na dada yake. Jamaa ameingia kwenye ulaghai.
Hayo mambo yapo sana siku hizi wala sishangai. Nimeshashuhudia Mama Mkwe anamtafutia mabwana Mwali wake ambae ni Mke wa Mtoto wake wa Kiume.
 
Huyu mke wetu anasema yeye alimuambia amekuta meseji za wanawake kwenye simu ya best angu sasa akawa anamdisia wifi yake ndio akakutana na ushauri huo wa kubomoa

Hahahaaa siku atakayofuata huo ushauri hatokaa akuambie, ila ipo siku... Anayeweza kutuelewa wanawake ni Mungu tuu😃😃😃
 
Kiufupi huyo mwanamke ni mjanja sana, anatengeneza trust ili akachepuke vizuri huko atakakoenda kuchepuka.

Niggar angalia kama mali yako ni inalika ,,,wewe kula" mengine atajua yeye mwenyewe milwaji.
 
Nawaza akifwata huo ushauri wa wifi alafu siku kiumane, hatoamini kama ni wifi ndie aliekua kuwadi . ila vitu vinavyocross kwenye akili za watu wakati mwingine vinashangaza
 
Back
Top Bottom