Dada ang'u anataka kumuua mwanae!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Habarini wana JF, Majuma kama matatu yaliyopita dadaangu ambaye ni mtoto wa rafiki mkubwa wa mama yangu mzazi alifanya jaribio la kumuua mtoto wake wa kumzaa. Tatizo ni kwamba alipata ujauzito baada ya Kubakwa na kijana fulani (Ametoroka yasemekana anaonekana mkoani Arusha ni dereva tax kwa sasa), huyo dadaangu ni mwalimu na huyo mtoto ana miaka mitatu. Ilibidi itumike mbinu isiyo rasmi kuwapoza Polisi. Hata hivyo baada ya kuhojiwa na watu wa karibu anasema kuwa huwa anasikia hasira sana kila anapomuona yule mtoto na anamchukia kutoka moyoni Kwani amefanana sana na baba mbakaji. Kikubwa kingine kinachomfanya amchukie ni kuwa uchumba wake ulivunjika baada ya kupata mimba hiyo iliyotokana na kubakwa. Mchumaake alikuwa masomoni South Africa aliporudi na kulikuta hilo akaghairi
YUKO SAHIHI KUMCHUKIA MWANAE KWA KUWA ALIPATIKANA BAADA YA KUBAKWA?
 
haina maana kutafuta usahihi wa yeye kuua mtoto ama kutokumuua. ameathiika kisaikolojia kutokana na madhali yaliyompata. wakati mnafanya mipango ya kumsaidia apae matibabu ya kiakili, mnaweza kumsaidia kwa kumchukua mwanae na kukaa nae ili mumpatie mapenzi ya kindugu na kumuepusha nae kuathirika kisaikolojia. poleni sana,kwa kweli wabakaji wote wanastahili adhabu duniani, na kisha ahera!
 
Mtoto hana hatia..sema kwa kweli jamaa alimfanyia kitendo cha unyama.
 
Hayuko sahihi, ila tatizo lake linataka sana councelling ya hali ya juu. Anamwona kama mtoto kamuharibia maisha, halafu watoto wa hivo huwa wanakuja kuwa na akili sana
 
Habarini wana JF, Majuma kama matatu yaliyopita dadaangu ambaye ni mtoto wa rafiki mkubwa wa mama yangu mzazi alifanya jaribio la kumuua mtoto wake wa kumzaa. Tatizo ni kwamba alipata ujauzito baada ya Kubakwa na kijana fulani (Ametoroka yasemekana anaonekana mkoani Arusha ni dereva tax kwa sasa), huyo dadaangu ni mwalimu na huyo mtoto ana miaka mitatu. Ilibidi itumike mbinu isiyo rasmi kuwapoza Polisi. Hata hivyo baada ya kuhojiwa na watu wa karibu anasema kuwa huwa anasikia hasira sana kila anapomuona yule mtoto na anamchukia kutoka moyoni Kwani amefanana sana na baba mbakaji. Kikubwa kingine kinachomfanya amchukie ni kuwa uchumba wake ulivunjika baada ya kupata mimba hiyo iliyotokana na kubakwa. Mchumaake alikuwa masomoni South Africa aliporudi na kulikuta hilo akaghairi YUKO SAHIHI KUMCHUKIA MWANAE KWA KUWA ALIPATIKANA BAADA YA KUBAKWA?
Huyo DADA NI MWALIMU, HUYO MUME NI DEREVA TAXI... Hajabakwa hata kdogo, 100% mdada tamaa zmemzd, atajiju! Tena huyu inabd afungwe kwa jarbio la kuua.... Dhambi znapatkana hapa dunian, msaliti mkubwa wa mapenzi huyo!
 
haina maana kutafuta usahihi wa yeye kuua mtoto ama kutokumuua. ameathiika kisaikolojia kutokana na madhali yaliyompata. wakati mnafanya mipango ya kumsaidia apae matibabu ya kiakili, mnaweza kumsaidia kwa kumchukua mwanae na kukaa nae ili mumpatie mapenzi ya kindugu na kumuepusha nae kuathirika kisaikolojia. poleni sana,kwa kweli wabakaji wote wanastahili adhabu duniani, na kisha ahera!
Mkuu fateni ushauri huo wa king'asti haraka sana.Kila la kheri.
 
Anaitaji counselling haraka sana

Kuna mdau anamtukana hapo juu wewe halijakukuta ndio maana unaongea eti kajitakia
 
huyo dada ni mwalimu, huyo mume ni dereva taxi... Hajabakwa hata kdogo, 100% mdada tamaa zmemzd, atajiju! Tena huyu inabd afungwe kwa jarbio la kuua.... Dhambi znapatkana hapa dunian, msaliti mkubwa wa mapenzi huyo!
mkuu,taratibu kidooogo!! Mh! Usikimbilie kumuhukumu wakati hujui undani wa kitu.
 
Pole sana dada, fuateni ushauri mzuri mliopewa hapo juu.
 
Habarini wana JF, Majuma kama matatu yaliyopita dadaangu ambaye ni mtoto wa rafiki mkubwa wa mama yangu mzazi alifanya jaribio la kumuua mtoto wake wa kumzaa. Tatizo ni kwamba alipata ujauzito baada ya Kubakwa na kijana fulani (Ametoroka yasemekana anaonekana mkoani Arusha ni dereva tax kwa sasa), huyo dadaangu ni mwalimu na huyo mtoto ana miaka mitatu. Ilibidi itumike mbinu isiyo rasmi kuwapoza Polisi. Hata hivyo baada ya kuhojiwa na watu wa karibu anasema kuwa huwa anasikia hasira sana kila anapomuona yule mtoto na anamchukia kutoka moyoni Kwani amefanana sana na baba mbakaji. Kikubwa kingine kinachomfanya amchukie ni kuwa uchumba wake ulivunjika baada ya kupata mimba hiyo iliyotokana na kubakwa. Mchumaake alikuwa masomoni South Africa aliporudi na kulikuta hilo akaghairi
YUKO SAHIHI KUMCHUKIA MWANAE KWA KUWA ALIPATIKANA BAADA YA KUBAKWA?

Nikiangalia muda sioni kama ni tatizo la kubakwa..kama angekuwa na hasira basi angetoa mimba (abortion)..lakini amebeba ujauzito miezi 9 akijua ana mpenzi, amelea miaka mitatu...Kuna tatizo kubwa sana nyuma ya huyo dada..kwa haraka haraka ni tatizo la kiuchumi..nadhani ameona amefulia na mtoto anamletea "kauzibe"..

Sisi binadamu tumejaliwa uwezo wa kusahau kadri ya siku zinavyoenda... Pia mioyo yetu imeumbwa na uchungu tukuangalia macho ya watoto..Fanya utafiti huu.. tafuta rafiki au ndugu unayemchukia sana...halafu nenda nyumbani kwake wakati yeye hayupo ila wapo watoto wake tu..halafu ongea nao uone dhamira yako itavyokusuta...

Dawa ya huyo dada ni kumweka chini ya ulinzi na kumpa kibano cha nguvu mpaka aseme ni nani anamsumbua..naweza kuhisi kuna jamaa ana hela kidogo anamdanganya atamuoa lakini hataki kulea mtoto asiye wake..kama sababu siyo hiyo basi asaidiwe kuwekwa sawa kiuchumi ili asitegee wanaume..hakijiamini atampenda huyo mtoto.. Watoto ni malaika jamani..
 
Nyie kama ndugu wa dada huyo, chukua mtoto mkae naye, na huyo Mdada mmtafutie mshauri nasaha ili ashuriwe na kujengwa kisaikolojia, ni kweli anajisikia vibaya maana kila akimwona huyo mtoto inamkumbusha jinsi tukio lote la kubakwa lilivyotokea na kusababisha kuachwa na mchumba wake. Kuweni makini naye, maana maana kama hamtachukua hatua haraka, akishindwa kumuua mtoto anaweza kujiua mwenyewe.
 
Habarini wana JF, Majuma kama matatu yaliyopita dadaangu ambaye ni mtoto wa rafiki mkubwa wa mama yangu mzazi alifanya jaribio la kumuua mtoto wake wa kumzaa. Tatizo ni kwamba alipata ujauzito baada ya Kubakwa na kijana fulani (Ametoroka yasemekana anaonekana mkoani Arusha ni dereva tax kwa sasa), huyo dadaangu ni mwalimu na huyo mtoto ana miaka mitatu. Ilibidi itumike mbinu isiyo rasmi kuwapoza Polisi. Hata hivyo baada ya kuhojiwa na watu wa karibu anasema kuwa huwa anasikia hasira sana kila anapomuona yule mtoto na anamchukia kutoka moyoni Kwani amefanana sana na baba mbakaji. Kikubwa kingine kinachomfanya amchukie ni kuwa uchumba wake ulivunjika baada ya kupata mimba hiyo iliyotokana na kubakwa. Mchumaake alikuwa masomoni South Africa aliporudi na kulikuta hilo akaghairi
YUKO SAHIHI KUMCHUKIA MWANAE KWA KUWA ALIPATIKANA BAADA YA KUBAKWA?

my friend, nyie ni watu wabaya sana... yani mtu anataka kuua halafu mnawapoza polisi???

mpelekeni msimbazi au vtuo vya yatima kuliko kutetea muuaji, th baby is innocent na kuna watu wanaomba usiku na mchana kupata mtoto

umeniudhi sana kusema ati mlipoza polisi... ulitakiwa uripoti polisi na sio JF
 
Pole sana,
Muweke mtoto mbali na mama yake then mshugulikie mama yake sio mzima, hayupo sahihi kumuua mwanae make mtoto ni malaika siku zote hana kosa mwenye kosa ni baba yake
 
Kwa sis tunaoamini imani za dini mathalani dini ya kristo tunaamini kila ki...kuwepo duniani, mshaurini sana dada aikubali hali hiyo mana hajui mpango wa Mungu juu ya huyo kijana, yawezekana huyo mchumba wake aliyekuwa anamtegemea asingemfaa kama ambavyo huyo kijana atakavyomfaa, haya maisha ni makaratasi bwana kila kalamu inaandika, swala la mwandiko mzuri inategemea na ushukaji wa kalamu na mkono wa mwandishi...haina haja ya kulaumu kalamu! Ni hayo tu Brah!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom