Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Binamu yangu aliolewa mwezi Oktoba 2016. Aliolewa na kijana wa Bagamoyo huko mtoto wa Mganga. Baada ya ndoa wakaenda kuishi huko Bagamoyo nyumbani kwa wazazi wa mume wake.
Maisha yameendelea tu vizuri hadi siku ya Jana alipokuja kwetu usiku saa tano na begi kubwa la nguo.
Kumuuliza vipi umekuja na mzigo hivyo, kwema huko? Akasema si kwema hata kidogo! Baba Mkwe anataka amuoe yeye. Yaani baba wa mumewe amesema mwanae ampe talaka mkewe kisha amuoe yeye!
Sababu aliyotoa mzee ni kuwa yule binti ana nyota kali sana(nadhani kaiona kwenye ulimwengu wa kichawi huko) hivyo mwanae hatoiweza inaweza hata kumuua. Yeye kwakuwa mganga kwanza itamsaidia kwenye kazi zake na pia ataweza kuikabili kwa kutumia mizimu.
Mume wake hana usemi wowote, haoneshi upande wowote. Anasema tangu baba mkwe atamke maneno hayo mumewe kawa kama zoba, mpole kupitiliza na muda wote anawaza tu. Haongei kitu chochote hata akimuuliza. Hajui hata kama anakubaliana na mzee wake au la!
Sababu ya kuja kwetu na sio kwao (kwa mama yake) ni kwakuwa alipomwambia mama yake kwenye simu, akamwambia kama ndio walichoamua upande wa mumewe hatakiwi kupinga maana sasa yuko chini ya mumewe! Kumpigia mama mkubwa simu anasema " Labda ndo majaliwa yake hayo, hawezi kuepuka"
Mama kasema tukae nae hadi waje kumtafuta ili watueleze vizuri wana mpango gani na huyu binti.