Kilimanjaro: Mama adaiwa kumuua mwanae wa miaka mitatu kwa kumchapa fimbo

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
421
1,048
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linamshikilia mwanamke mwenye miaka 27, Mkazi wa Kibosho Kirima Juu, Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua mwanae mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita kwa kumchapa na fimbo.

Akithibitisha hilo mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, ACP Simon Maigwa amesema tukio hilo limetokea Jumapili Julai 31, 2022 majira ya saa moja asubuhi.

Kamanda Maigwa amesema Mama huyo alimchapa na fimbo mwanae katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku chanzo kikidaiwa kuwa mtoto huyo alifungulia bomba na kuchezea maji ya baridi yaliyokuwa yakitiririka.

" Baada ya kuona hali ya mwanae imezidi kuwa mbaya mama huyo alijaribu kutoroka ila wananchi walimdhibiti na Jeshi la Polisi tulifanikiwa kumchukia kwa taratibu za kisheria" Amesema Kamanda Maigwa.

Aidha Kamanda Maigwa ametoa wito kwa wazazi kutumia busara katika kuwaadhibu watoto wao pale wanapofanya kosa na sio kuchukua hatua kali hali inayopelekea kuhatarisha maisha.

"Kitendo cha kuchapa sio suluhisho kumfanya mtoto awe mtiifu, wazazi tumieni njia za busara, huyu mtoto alikuwa na miaka mitatu na miezi sita bado ni malaika haelewi chochote," amesisitiza Kamanda Maigwa.

Chanzo: Langolahabari
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linamshikilia mwanamke mwenye miaka 27, Mkazi wa Kibosho Kirima Juu, Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua mwanae mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita kwa kumchapa na fimbo...
Wamama wengi hasira za wanaume zao huzimalizia kwa watoto.. RIP little angel..may your soul rest in eternal peace
 
Ninapoishi kuna dada mmoja ana mtoto miaka mitatu na mwingine nadhani hajafikisha mwaka.

Huyu dada anaonekana ana stress sana maana huwa ni wakushinda home tu na kazalishwa na mume wa mtu ndio anamlipia kodi na kumtunza.

Huwa anakapiga hako katoto ka 3years na kukatukana vibaya sana yani katoto kanapewa kazi ya kumlelea mdogo wake na mtoto akilia tu dogo anatukanwa matusi ya nguoni utafikiri sio mama yake na anachezea mikanda balaa.

Mimi huwa najisemea tu siku akiua. Mimi nakimbia naenda bar kula zangu beer sitaki ushahidi.

Stress zimejaa kwenye hii nchi serikali iangalie namna ya kufariji raia wake.
 
Inasikitisha sana

Ila pia mazingira hayaoneshi kama kulikuwa na dhamira ya kuua.
Miaka mitatu anampiga mpaka anakufa ina maana alikuwa anapiga kila sehemu ya mwili bila kwa hasira. Kama alivyosema Mshana Jr mara nyingi baadhi ya wanawake wanapokuwa na visirani na waume zao, humalizia hasira kwa watoto. Kuna tukio moja lilitokea zamani kidogo.

Hili lilikuwa ni baba alimpiga mtoto mwenye miaka saba hivi akafa. Walipoona amekufa wakachukuwa sumu ya kupulizia wadudu wakamwagia kwenye mdomo jalafu wakasema alikunywa sumu.
 
Miaka mitatu anampiga mpaka anakufa ina maana alikuwa anapiga kila sehemu ya mwili bila kwa hasira. Kama alivyosema Mshana Jr mara nyingi baadhi ya wanawake wanapokuwa na visirani na waume zao, humalizia hasira kwa watoto. Kuna tukio moja lilitokea zamani kidogo. Hili lilikuwa ni baba alimpiga mtoto mwenye miaka saba hivi akafa. Walipoona amekufa wakachukuwa sumu ya kupulizia wadudu wakamwagia kwenye mdomo jalafu wakasema alikunywa sumu.
baba alimpiga mtoto mwenye miaka saba hivi akafa. Walipoona amekufa wakachukuwa sumu ya kupulizia wadudu wakamwagia kwenye mdomo jalafu wakasema alikunywa sumu.

Ushetani mkubwa sana huu
 
baba alimpiga mtoto mwenye miaka saba hivi akafa. Walipoona amekufa wakachukuwa sumu ya kupulizia wadudu wakamwagia kwenye mdomo jalafu wakasema alikunywa sumu.

Ushetani mkubwa sana huu
Kweli kabisa. Ila mazingira ambayo huyo baba alikuja fariki nayo yalikuwa kama karma imechukuwa mkondo. Alikuwa ni mnywa gongo, basi siku moja akaifakamia kumbe ilichanganywa na spirit na ikamharibu tumboni. Alianza kukonda na kushindwa kula vizuri ahuku akiteseka kama mwaka hivi ndiyo akafariki.
 
Ninapoishi kuna dada mmoja ana mtoto miaka mitatu na mwingine nadhani hajafikisha mwaka.

Huyu dada anaonekana ana stress sana maana huwa ni wakushinda home tu na kazalishwa na mume wa mtu ndio anamlipia kodi na kumtunza. Huwa anakapiga hako katoto kwa 3years na kukatukana vibaya sana yani katoto kanapewa kazi ya kumlelea mdogo wake na mtoto akilia tu dogo anatukanwa matusi ya nguoni utafikiri sio mama yake na anachezea mikanda balaa.

Mimi huwa najisemea tu siku akiua. Mimi nakimbia naenda bar kula zangu beer sitaki ushahidi.

Stress zimejaa kwenye hii nchi serikali iangalie namna ya kufariji raia wake.
Nilishagombana na dada mmoja vibaya mno kwa ajili hiyo, mtoto mdogo anapigwa kwa makosa madogo kisha akilia anapigwa tena, nikamtamkia kama mtoto amemshinda ampeleke vituo vya yatima tu.. alikuwa na stress za kuzalishwa na kuachwa pia
 
Mimi personally ni sio muongeaji na sipendi kuingilia mambo ya watu. Huwaga sina maneno salamu tu napita zangu mbele. Sijawahi kumuambia chochote.
 
Kweli kabisa. Ila mazingira ambayo huyo baba alikuja fariki nayo yalikuwa kama karma imechukuwa mkondo. Alikuwa ni mnywa gongo, basi siku moja akaifakamia kumbe ilichanganywa na spirit na ikamharibu tumboni. Alianza kukonda na kushindwa kula vizuri ahuku akiteseka kama mwaka hivi ndiyo akafariki.
Safi sana.. Karma is bitch ..!
 
Kweli kabisa. Ila mazingira ambayo huyo baba alikuja fariki nayo yalikuwa kama karma imechukuwa mkondo. Alikuwa ni mnywa gongo, basi siku moja akaifakamia kumbe ilichanganywa na spirit na ikamharibu tumboni. Alianza kukonda na kushindwa kula vizuri ahuku akiteseka kama mwaka hivi ndiyo akafariki.
Aisre hii ilikuwa karma kwelii...
 
Back
Top Bottom