Dada anagoma kumpa Kaka mwanaye, waliyezaa naye

Dada anagoma kumpa Kaka mwanaye, waliyezaa naye

Akili yangu inagoma kabisa kukubaliana na hili andiko. Enewei, ni jukwaa huru hili
 
Katika mazingira fulani kaka na dada (mama zao mtu na mdogowe) wakajikuta wameanza mahusiano hatimaye kupata mtoto.

Dada alipoulizwa na wazazi wake kuhusu mimba akamsingizia mtu hewa, mtoto akazaliwa maisha yakaendelea, na huduma zinatolewa kwa usiri mkubwa sana mpaka sasa.

Wakati hayo yanafanyika Kaka mtu alikuwa tayari ana mke na mtoto mmoja mchanga.

Miaka 10 Sasa jamaa hajabahatika kupata mtoto mwingine kwa mkewe, pia kajaribu kutafuta nje ya ndoa imeshindikana kabisa, dada alishaolewa na amejaaliwa watoto wawili wengine.

Sasa Kaka anataka amchukue mwanaye aliyezaa na dada yake amlee kama mwanaye na awe sehemu ya urithi wake, lakini dada hataki kwasababu watu wanasema mtoto anafanana na Mjombaake (baba) Kwahiyo akimchukua siri itavuja,Kaka naye anatishia kutotoa msaada wowote endapo hatapewa mwanawe.

Kwenu wanaJF mnawaambia nini hawa wazazi mtu na dada yake.
Hao ni binamu sio kaka na dada. Watoto wa ndugu wawili wa kike au mmoja wa kiume na mwingine wa kike huwa wanaitana binamu. Ndugu ni watoto wa baba mkubwa na baba mdogo.

Pia makabila mengi bunamu wanaruhusiwa hata kuoana mfano kabila langu.
 
haya mambo bwana, huku wanataka kuchinjana kugombea mtoto, kule wanatupa watoto chooni,

kule wanachoropoa mimba, pale anakataa mtoto akidai bibie 'kajilengesha'
 
Hao ni binamu sio kaka na dada. Watoto wa ndugu wawili wa kike au mmoja wa kiume na mwingine wa kike huwa wanaitana binamu. Ndugu ni watoto wa baba mkubwa na baba mdogo.

Pia makabila mengi bunamu wanaruhusiwa hata kuoana mfano kabila langu.
Ni kweli,ila katika kabila lai binamu ni ndugu kabisa ni mwiko kumuoa,na hata ikitokea wakagundua mabinamu wametiana mimba lazima ichomolewe na yafanyike mambo ya kimila ili kuondoa nuksi.
 
Hao ni binamu sio kaka na dada. Watoto wa ndugu wawili wa kike au mmoja wa kiume na mwingine wa kike huwa wanaitana binamu. Ndugu ni watoto wa baba mkubwa na baba mdogo.

Pia makabila mengi bunamu wanaruhusiwa hata kuoana mfano kabila langu.
Mkuu hayo makabila yana jumuisha wazaramo ??
 
Hapana mkuu sio watu wa Pwani
Hapana mkuu, nilimquote jamaa mmoja hapo juu alisema kuhusu makabila yanayo ruhusu binamu kuoana nikauliza kama hayo makabila yana jumuisha wazaramo.
 
Umejiuliza nimejuaje?
Kuna vyanzo vingi vya information hivyo kujua wala sio hoja unaweza kujua taarifa za mtu fulani ambaye hata hamjawahi zungumza ni vyema ukajibu tu swali kama ilivyo

Amani iwe nawe
 
Mkuu hayo makabila yana jumuisha wazaramo ??
Kwa wazaramo sijui ila huko kanda ya ziwa wanaoana, mimi mwenyewe ilikuwa nioe binamu yangu ila ilishindikana sababu alikuwa anasoma bado nami muda wa kuoa ulifika ikabidi nisonge mbele na aliye tayari.
 
Kuna vyanzo vingi vya information hivyo kujua wala sio huja unaweza kujua taarifa za mtu fulani ambaye hata hamjawahi zungumza ni vyema ukajibu tu swali kama ilivyo

Amani iwe nawe
Sawa mkuu,amani iiwe nawe pia.
Mimi ni rafiki yake jamaa,baada ya mambo kuwa magumu jamaa akanitafuta na kunisimulia mkasa mzima,na tumeshawahi kukaa kikao cha faragha mimi ni wao lakini bahati mbaya sana kikao hakikuzaa matunda.
Mimi na huyu rafiki yangu makabila tofauti,kwa kabila langu mimi mtoto wa Shangazi mjomba Mama mkubwa ruksa kuoa.
 
Back
Top Bottom