Daah! Ila haya mambo

Daah! Ila haya mambo

Antennah

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2015
Posts
6,933
Reaction score
9,033
Basi bhana leo nimerudi nyumbani baada ya kupiga sana mzigo kwa mwezi mzima katika taasisi fulani.

Kabla sijafika nyumbani nikaona sio mbaya kama nikipitia maeneo fulani kupata moja moto moja baridi.

Kiukweli ilifika point nikawa sijielewi kabisaa basi hapo nikaamua tu niende nyumbani.

Baada ya kufika nyumbani inaonesha niliwapigia simu baadhi ya watu kadhaa kutoka kwenye phone book yangu, sasa shida ni kwamba

Kuna huyu mwanangu anaitwa tonny, mpaka dakika hii ananipigia zaidi ya mara ya nne anapiga simu kunishukuru sana, yani mpaka naona kabisa unyenyekevu mkubwa kwenye sauti yake, na ananiambia eti kesho atakuja nyumbani nimpe info kwa undani zaidi juu ya mchongo niliompatia ili aanze kuutekeleza.

Asichokijua ni kwamba mi sikumbuki lolote na sikumbuki kama kuna mchingo wowote nimeutoa kwa mtu yeyote, mi mwenyewe hapa natamani atokee mtu anipe mchongo, sasa sielewi imekuaje leo mimi ndo nimekua mtoa mchongo.

Ndugu zangu wale wa kula vitu, hebu nisaidieni, itakua nimemuahidi kumpa mchongo wa aina gani huyu janja.
 
Inakuaje unalewa unaongea ahadi fake na hukumbuki cc min -me Dr am 4 real PhD
Unajua pombe/ alcohol = kifutio / eraser Sasa ipo ""The higher the alcohol the higher the eraser"" & vise versa is True.

Kikubwa pombe huchochea confidence/ kujiamini na kubwa kuliko hata kwenye vikao vya harusi ili watu wa PLEDGE vizuri hupewa alcohol hivyo hakuna wa ku pledge kinyonge

Pombe for years imetumiwa na ma champion na washindi vile vile wafalme
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom