Daah Ajira ngumu aisee!

Nimekufurahisha nini??..kuhangaika kwangu ama?..sijakuelewa
 
tatizo lenu vijana siku hizi mmekariri tu kuwa mkimaliza chuo tu basi ofisi inakusubiri wapewa funguo tu....jamani vijana amkeni tufikirie na mpango mwingine (plan B) kama kujiajiri au kuunda vikundi na kutafuta kitu cha kufanya na kwa njia ya vikundi mikopo inakuwa inapatikana...katika maisha kaka ni lazima ukiwa na ishu yako unataka kuifanya jaribu kuwa na alternatives ili hii ikikwama basi unaswitch kwa nyingine...ni marufuku kukariri!!!!!!!!!!!!!!! pia ujue kuwa hizo kazi ulizokosa hazikuwa rizki yako na kwamba rizki yako ipo njiani na utakuja kufanikiwa...haya yanayokukuta kwa hivi sasa ni kwamba unatengeneza history ya maisha yako na wakati umefanikiwa utakuwa unakumbuka tu kama history....kumbuka pia 'likuepukalo lina kheri na wewe'...kwa hiyo usife moyo endelea kuhangaika huku ukiwa na alternatives zako pia...kila la kheri ndugu yangu, mambo yatakuwa mazuri tu kwa wakati wa Mwenyezi Mungu...inshaallah!!
 
Asante kwa ushauri ndugu.
 

Pole sana Mkuu!!Usikate tamaa kwa jitihada zako soon utapata kazi......la msingi Omba Sana Mungu uku ukijibidiisha kutafuta kuna mahali anakupeleka,we all don't knw whr?I am sure next tym utaleta ushuhuda humu JF wa kazi uliyoipata.
 

Mjuni umenikumbusha, dah nimeshauza vyombo kwa jampuni pale Morocco(by far 2000) nliuza wiki 2 nkakimbia. Kweli maisha safari ndefu jamani, ninaimani ipo siku utafanikiwa bwa mdogo, tumepita wote ktk hizo challenge but saiv aagh shwari tu

Mimi naamini kuwa pa1 na kuwa na background mbaya ya familia bado ukitulia unaeza fanikiwa.
 

Mmh so sad, dah naomba isinitokee maana mchana ntakuwa na usaili
 
Nashukuru kwa kunipa moyo jombaa. Much love
 

Naomba nisaidie hizo recruitment agency za Tanzania mkuu, walau 3 tu nina shida nazo
 
Unazikumbuka zile, Introduction,short story, presentation,close na reharsh?
Au ulikimbia kabla ya kujua five steps to sell?
 
PESA YA PHOTOCOPY,BAHASHA,STAMPS NA MUDA NI MTAJI TOSHA kwako.
Ok mi nikupe ushaur huu: pls achana kbs na mawazo ya kuajiriwa maana ajira zimekuwa magumashi sana cku hzi..,mi nilipomaliza digrii yangu ya uhasibu moja kwa moja nilirudi kijijin nikiwa na laki tatu na sitini elfu(360000) nkaanza mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa kufuata ushaur na maelezo yalipo humu humu jf.,amini usiamin saiz siwaz kutafuta ajira ila nina vijana watatu nimewapa ajira tunasaidiana kulea kuku hao ambao wananiingia NET PROFIT ya 9M kwa mwaka,najenga sasa,nakausafir kangu,mtoto anasoma english medium na sasa nashauriana na wife aache kazi yake ya ualim tupige mzigo huu. Yan hyo pesa ya photocopy,stamp,bahasha na muda huo ulikuwa mtaji tosha.
 
Asante kwa mawazo mazuri.
 
Asante kwa link hiho mkuu.
 
Usihangaike piga 0719836781 au 0765666390 mwambie matatizo yako atakusafishia nyota nakuambia hutachuku mwezi unakitengo.serious mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…