Mimi nilipomaliza chuo nilikaa mwaka mmoja bila shughuli yeyote,
Baadaye nikaenda kwenye kakampuni nikawa natembeza vyombo, unauza bei ya juu, unakata pesa ndiyo mshahara wako, usipouza na wewehela huna, nilivumilia ili tu kukicha niwe na pa kwenda. Nilijifunza five steps to sell, Sijui eight steps to success lakini baada ya mwaka mmoja sikuona gain yeyote, nilikuwa napata hela ya kula tu halafu kazi ngumu kwrlikweli, unatembea mitaani hadi sole za viatu vinaisha, hujauza
Baada ya mwka mmoja niliacha, nikaenda kufundisha shule za kata, imagine, graduate unafundisha form one na form two physics na hesabu,mshahara elfu 70, nikawa nafundisha vishule viwilikwa wakati mmoja, Nikawa napata pesa ya nauli kwenye interviews mbalimbali,
Baadaye nikapa sehemu nzuri kutokana na elimu yangu, sasa hivi mambo safi.
Kwa hiyo unaweza kuona kuwa nilikaa almost miaka mitatu ndipo nikapata sehemu ya maana.
Kwa hiyo na wewe kama umesota kwa mmiaka miwili au mitatu usiogope, ndivyo ilivyo.