Da kweli walimu wanasafari ndefu

kwamba hela ni ndogo au vipi mkuu ebu njoo na habari kamili kwani aijakamilika.

Sikia mkuu, 'biashara' ya semina na warsha inalipa sana kwetu ma-afisa elimu na wakaguzi- malipo halali ya semina ile aka padiem ni kama elfu hamsini kwa mwalimu, kukodi ukumbi, steshenali, chakula nk. Sasa tulichofanya ni kukata michango ya mafuta ya mwenge, pia tumebana matumizi kidogo upande wa ukumbi ambapo tulipanga semina ifanyike pale Ngurudoto lakini tumeamua kutumia chumba cha darasa, teh,teh!kweeeeee!

Mchawi wa Watanganyika yumo vichwani mwetu, serious ukiona mchanganuo wa pesa za semina hiyo ni utazimia. Viva mama Ghasia!
 
Walimu yatupasa kuwa na msimamo hawa maafisa elimu ndo maadui zetu wakwanza kabla ya hata serikali. Mkiweza kuondoka wote they will learn a lesson. Tupambane na huu udhalimu.
 
Hapana! hawapaswi kuadhibiwa, mwalimu, wajua mimi mwenyewe ni mwalimu by professional nimekaa huko kwa 6 years lakini tatizo kubwa la walimu walio wengi hawajitambui, waoga katika kusimamia maslahi yao... mimi nilishindwa kuwa muoga nikaamua bora niepushe balaa mapema.

Ila najisifu kuwa mwalimu, na napenda kufundisha hasa....

Hii ndio serikali sikivu inayo wajali wananchi wake. Mbunge anaye sinzia kwenye kikao kwa sababu alikunywa bia na wanawake mpaka usiku alipwe 200,000/= -kwa siku mwalimu anaye hangaika na watoto 600 form one hadi form four mwalimu wa sayansi ni mmoja anapo jengewa uwezo wa kufundisha alipwe sh. 15,000/= Baada ya wanafunzi kufeli tutaunda tume ya kuchunguza. Ninahisi kila mtu anatuona tumebeba maboga juu ya shingo zetu tunayaita vichwa
 
kwamba hela ni ndogo au vipi mkuu ebu njoo na habari kamili kwani aijakamilika.

kama hujui kaa kimya mwaliku wa sekondari ni Afisa Elimu kwa cheo chake anatakiwa kulipwa nihgt allowence ya tsh 65000 hii ni kwa mujibu wa waraka wa utumishi kwanini unauliza swali la kipuuzi?
 
Hii ndo serikali sikivu na inayo wajali wananchi wake.Mbunge anaye sinzia kwenye vikao kwa sababu alikunywa bia jana yake akachelewa kulala alipwe Tsh 200,000/= posho kwa siku Lakini mwalimu wa sayansi anayefundisha watoto 600 kutoka kidato cha kwanza mpaka cha nee akiwa mwalimu pekee wa sayansi anapo jengewa uwezo wa kuhangaika na watoto wate shule nzima peke yake alipwe Tsh. 15,000/= na baadae wanafunzi wakifeli tutaunda tume ya kuchunguza matokeo mabaya. Ninahisi watu wanao tuangalia wanatuona tumebeba maboga juu ya shingo zetu na tunaita vichwa.
 
Back
Top Bottom