Nana brain
JF-Expert Member
- Jan 3, 2017
- 488
- 367
Majuma kadhaa yalopita, The Bold aliweza kuandika Thread inayomhusu D.B.Cooper,jamaa ambae aliweza kuiteka ndege ya Boeing mnamo mwaka 1971 na kisha kuomba apewe dollar lak 2 ambazo alipewa na baada ya hapo alifanikiwa kuruka kutoka ndani ya ndege kwa kutumia parachuti pasipo kujulikana ni wapi alienda na alikuwa ni nani hasa na isijulikane yupo wapi mpaka leo hii
Baada ya kitendawili hicho kushindwa kuteguliwa, mnamo mwaka 2016 mwezi June FBI waliamua kuifunga rasmi kesi hiyo ambayo waliona walikuwa wakipoteza pesa ambazo huenda zingesaidia katika sekta zingine za maendeleo na sio kuchunguza kesi ya mtu aliyeshindwa kujulikana kwa muda wa miaka 45.
Lakini kuna kundi la wanasayansi wa kujitegemea wanaohusika na uchunguzi wa matukio ya uhalifu waliamua kuichunguza kesi hiyo kuanzia miaka mitatu iliyopita pasipo kutegemea pesa kutoka Serikalini
Kwa miongo mine ya tukio kumekuwa na wakisiwa zaidi ya 1000 ambao walidaiwa kuwa wanaweza kuwa ndio D B Cooper mwenyewe, wakisiwa ambao walikataliwa kuwa si D.B. Cooper kwa kulinganisha muonekano wa nje kama ulifanana na maelezo yaliyotolewa kuhusu mwonekano wa D B Cooper, Uwezo na uzoefu wa kutumia parachuti, DNA test kwa kutumia tai iliyoachwa na D B Cooper ndani ya ndege baada ya kuruka, DNA ambayo ilidhihirisha kuwa wakisiwa hawakuwa D.B.Cooper mwenyewe
Mwandishi Ross Richardson kutokea Michigan aliweka mbele nadharia ya kumfananisha na kuamini kuwa D.B. Cooper lazima atakuwa Baba( aliyeitwa Richard Lepsy) mwenye mke na watoto wanne alieishi Grayling Michigan ambae alipotea mwaka 69 na kuacha mke na watoto bila kujulikana ni wapi alienda, kufananishwa huko ni baada ya picha ya mchoro wa D.B.Cooper kuoneshwa kwenye TV na watoto wote kutazamana na kusema ' huyo ni baba' kwani mchoro ulifanana sana na baba huyo.
Lakini mwaka 2011,mwanamke aliyeitwa Marla Cooper alikuja na Ushahidi ambao FBI walisema kuwa ulikuwa ni Ushahidi tosha kwa wao kufunga rasmi file la kesi ile.
Marla Cooper aliiambia FBI kuwa alikuwa na mjomba wake ambae alikuwa ni Mvamizi sugu wa ndege. Mwanamke huyo aliiambia FBI kuwa amekuwa na siri ya familia ya miaka arobaini kwa ajili ya kumlinda mjomba wake ambae aliitwa Lynn Doyle Cooper
Mwanamke anasema kuwa alikuwa na umri wa miaka minane ambapo mjomba wake ambae yeye alizoea kumwita LD Cooper alikuja nyumbani kwa ajili ya siku ya thanksgiving akiwa amejeruhika vibaya ambapo ilikuwa ni siku moja baada ya tukio la utekaji wa ndege kufanyika, alipoulizwa kuumia huko alisema kuwa amepata ajali ya gari lakini baadae wazazi wa mwanamke huyu walikuja kuamini kuwa mjomba wake L D Cooper ndie alikuwa mtekaji wa ndege hiyo. Anasema tangu siku hiyo hakuwahi kumwona tena mjomba wake mpaka aliposikia kuwa amefariki mwaka 99. Ushahidi huo ndio ulikuwa Ushahidi wa kuridhisha mpaka FBI wakaamua kuifunga kesi hiyo mwaka 2016
Pamoja na hivyo, kundi la wanasayansi wa kujitegemea wa uchunguzi wa matukio ya uhalifu wakiongozwa na Tom Kaye walijitolea kuendelea na utafiti wa D.B.Cooper
Ambapo kwa kutumia tai iliyoachwa na D.B.Cooper ndani ya ndege wamefanikiwa kuichunguza na tarehe 15.1.2017 wamejitokeza kutoa ushahidi wa majibu ya uchunguzi wao
JE INAWEZEKANA KUWA D. B. COOPER ALIKUWA NI MFANYAKAZI WA BOEING?
Uchunguzi wao unaonesha kuwa kwa namna moja au nyingine lazima D.B Cooper alikuwa ni mfanyakazi wa ndege ya Boeing.
Wanasayansi hao kwa kutumia microscope wamegundua chembe chembe za elementi tofauti tofauti katika tai ya D.B.Cooper, chembechembe hizo ambazo katika tai hiyo haziwezi kuonekana kwa macho bali kwa kutumia microscope ni chembechembe za element ambazo hupatikana mahali pachache sana na mahali flani flani Duniani humu, element hizo hutumika kwa matumizi maalumu tu na Kipindi hicho cha mwaka 71 zilikuwa zikitumika na kampuni ya Boeing katika kutengenezea ndege yao ya usafirishaji.Wanasayansi wanasema kuwa ni lazima D.B.Cooper alienda na tai ile kwenye maeneo Yale ya uzalishaji hivyo alikuwa ni Engeneer au manager kwenye moja ya plant za uzalishaji ambapo miaka ile ni mameneja na maingineer pekee ndio walivaa tai zile
Lakini matokeo ya uchunguzi huo yanazidi kuongeza makisio yasiyothibitishika na kuongeza utata katika kesi hiyo isiyotatulika .
Ni kuwa;
1. Hakuna Ushahidi wa kuweza kuthibitisha kuwa tai ile ilikuwa ni ya D B Cooper - hakuna uchunguzi uliofanywa wa kuweza kuaminisha kuwa tai ile ilimilikiwa na Cooper, Lakini wanasayansi hao wanasema kuwa wanaashumu kuwa tai ile ni ya Cooper kama step ya kwanza ya uchunguzi wao kwa sababu chembechembe walizoikuta nayo zinaelezea story ya Cooper
2. Tai ingeweza kuwa imevaliwa na Engineer yeyote au manager yeyote yule wa plant - kutokana na kwamba Uzalishaji wa ndege ulikuwa ni wa kampuni hiyo ya Boeing, inawezekana mmoja kati ya maengineer au mameneja alienda kupumzika ndani ya ndege ile na kuweza kusahau ile tai na hivyo kutoweza kuwa ya Cooper na hivyo kuwa hakufanya kazi kampuni ile
3. Baadhi ya chembechembe zilizo kwenye tai zilitumika sana kwenye viwanda wa kemikali, viwanda vya kufulia vyuma na viwanda vya kubadili vyuma chakavu katika mwaka huo 71 na hivyo uchunguzi mpya unatakiwa uanze kufanywa katika maeneo hayo.
Hivyo kwa matokeo hayo, Tom Kaye na wanasayansi wenzake wameomba msaada kwa wataalamu wa aerospace engineering ili kuchunguza zaidi kiundani na kuweza kuleta matokeo mengine
Hivi wewe unahisi kuwa kuna siku ambayo D.B Cooper atakuja kujulikana kuwa ni nani?