Bullying ipo sana NN na Kongosho msikatae.....
Mimi sijakataa kwamba bullying ipo (hivi kwa Kiswahili inaitwaje?). Ninachokataa ni kuchanganya trolling na bullying.
Mtu hunijui utaanzaje kuni-bully? Tunakutana humu kwa utambulisho usio halisia, hujawahi hata kunitia machoni na wala haitotokea unitie machoni hata siku moja, hujui nilipo, hujui nikoje - mrefu, mfupi, mnene, mwembamba, n.k., hujui nina kiwango changu cha elimu, hujui maishani najishughulisha na nini.....
Sasa huna habari zangu zozote zile ambazo ni za ukweli na ambazo unaweza kweli ukazithibitisha, utaanzia wapi kuni-bully?
Ndiyo, unaweza ukanitukana vijitusi ambavyo wala si vipya, utaniita vijina hapa na pale, utarudia uzushi ule ule wa kusadikika, but that is only as far as you can go.
Huna ammo zozote zile za ukweli ambazo unaweza ukaziweka humu na kuanza kuninyanyasa.
Uje humu uanze kusema sijui NN ni punga au sijui NN ana miaka 70....really?
We mwenyewe unayesema hivyo huenda hata huamini unayoyasema ila unayasema tu kwa sababu unataka kunikera.
Kwa hiyo kwangu madongo yarushwayo humu mengi huwa ni trolling na si bullying.