CWT taifa tunaomba ufafanuzi

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
9,732
10,813
Kuna tangazo la nafasi za ukatibu cwt wilaya,mmetoa majina ya walimu walioomba nafasi hizo kwa usaili tarehe 11th Novemba.
Kuna walioomba ambao majina yao hayapo kwenye hiyo list yenu.
Kuna mchujo ulifanyika kwenye ngazi ya wilaya/Mkoa?
Msaada katibu cwt Taifa.
 
Ata mimi niliomba nimekula za uso bila sababu hata sijui walikuwa wanangalia kama ni mzee sana au vigezo vimetumika
 
Hicho chama tumeshaskia kikilalamikiwa mara kadhaa na wanachama wake! Hakina msaada tena hata walimu wakandamizwe vipi! Ni bora kama tartibu zinaruhusu wanachama kujitoa, nashauri walimu jitoeni muache kupoteza michango yenu bure!
 
Umesema vema kabisa,hiyo option ya kujitoa ndio suluhu pekee kuondokana na adha ya chama ambacho hakitendi haki kwa wanachama wake
 
Kuna tangazo la nafasi za ukatibu cwt wilaya,mmetoa majina ya walimu walioomba nafasi hizo kwa usaili tarehe 11th Novemba.
Kuna walioomba ambao majina yao hayapo kwenye hiyo list yenu.
Kuna mchujo ulifanyika kwenye ngazi ya wilaya/Mkoa?
Msaada katibu cwt Taifa.
Huna kadi ya CCM wewe kaa pembeni.
 
Shida walimu wanatumiwa sana na CCM.
Wanao pata vyeo CWT ni malukuki wa CCM. Hapo unategemea nini?

CWT ni chama kilicho kosa maamuzi juu ya changamoto zinazo wakabili wanachama wake.

CWT kimetumika kuwakandamiza wanachama wake.

Ukiangali CWT imekosa majibu juu ya
1. Walimu wanao nyanyaswa na wanasiasa kv. DC,RC, maafisa elimu wenyeviti na viongozi wa ccm

2. Walimu kutozwa michango isiyo na mantiki mf. Mwenge n.k
NB. Walimu tambueni Taluma na siasa haviwezi kukaa pamoja.
 
Mimi ni mmojawapo wa waliojitokeza kuomba. Utaratibu uliokuwepo ni kwamba unapeleka barua kwa katibu wa wilaya. Kuna form maalum za kuangalia vigezo na unapewa alama(marks) mfano uliwahi kuwa mwakilishi wa tawi au kiongozi wa wilaya unapewa alama, una diploma, digrii au cheti unapewa alama. Baadaye form hizo zinachambuliwa kuonyesha waliopata alama za juu. Zinapelekwa mkoani zote(waliopata alama za juu na za chini). Mkoani nao wanazipitia kuangalia kwanini huyu amepata alama za juu au za chini. Nao wanafanya mchakato huo huo. Kisha zinapelekwa Taifani na katibu wa mkoa. Kule kuna watu wanaitwa KUT (kamati ya utendaji ya taifa) ndio wanaofanya short listing na baadaye interview. Ukipenya hapo unakula shavu.
NB:
Mfumo huu unawabeba zaidi viongozi kuliko walimu wa kawaida. Hii ni kwasababu wanapata alama nyingi zaidi kuliko blackboard teacher. Huu ndio uelewa wangu. Naomba kuwasilisha.
 
Kuna tangazo la nafasi za ukatibu cwt wilaya,mmetoa majina ya walimu walioomba nafasi hizo kwa usaili tarehe 11th Novemba.
Kuna walioomba ambao majina yao hayapo kwenye hiyo list yenu.
Kuna mchujo ulifanyika kwenye ngazi ya wilaya/Mkoa?
Msaada katibu cwt Taifa.
Hukuona only short listed will be contacted? Sisi hatutaki interview ifanyike uwanja wa Mkapa, nafasi zenyewe chacheee
 
Mimi ni mmojawapo wa waliojitokeza kuomba. Utaratibu uliokuwepo ni kwamba unapeleka barua kwa katibu wa wilaya. Kuna form maalum za kuangalia vigezo na unapewa alama(marks) mfano uliwahi kuwa mwakilishi wa tawi au kiongozi wa wilaya unapewa alama, una diploma, digrii au cheti unapewa alama. Baadaye form hizo zinachambuliwa kuonyesha waliopata alama za juu. Zinapelekwa mkoani zote(waliopata alama za juu na za chini). Mkoani nao wanazipitia kuangalia kwanini huyu amepata alama za juu au za chini. Nao wanafanya mchakato huo huo. Kisha zinapelekwa Taifani na katibu wa mkoa. Kule kuna watu wanaitwa KUT (kamati ya utendaji ya taifa) ndio wanaofanya short listing na baadaye interview. Ukipenya hapo unakula shavu.
NB:
Mfumo huu unawabeba zaidi viongozi kuliko walimu wa kawaida. Hii ni kwasababu wanapata alama nyingi zaidi kuliko blackboard teacher. Huu ndio uelewa wangu. Naomba kuwasilisha.
Hao wa wilayani wameweka kapuni maombi ya walimu wao wakajijazia alama za juu wenyewe.Haiwezekani M/kiti wa wilaya na mweka hazina ndio waonekane wanasifa wawe shortlisted.na walimu wengine wapungukiwe sifa.
 
Back
Top Bottom