Hii ndiyo CWT niijuayo

Mkyamise

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
454
555
Mimi ni mwanachama kwa zaidi ya miaka 15.

Miaka michache iliyopita CWT ilitangaza nafasi 12 za makatibu wa wilaya. Nikajaribu kuomba. Mchakato ulikuwa ni kama ifuatavyo:

1. Unaandika barua ya maombi kwa katibu mtendaji Taifa, ukiambatanisha nakala za vyeti, salary slip, kitambulisho cha uanachama, n.k.

2. Maombi yako unapeleka kwa katibu wa CWT wilaya ulipo. Hapa kuna makorokocho mengi sana. Kuna fomu wanatakiwa kukujazia ili upate marks/alama kulingana na sifa zako. Mfano kama una diploma huwezi kupata alama/marks zinazolingana na mwenye shahada, kama umewahi kuwa kiongozi wa tawi/wilaya huwezi kuwa na alama sawa na ambaye haja wahi kuwa kiongozi wa tawi/wilaya. Kifupi nilijiona nina sifa zote kabisa.

Orodha ya waliopata sifa za kuendelea baada ya mchujo hapa wilani sijawahi kuiona au kuipata. Mwishowe nikaja kugundua walipeana sifa wanaofanya kazi pale ofisi ya CWT wilaya. Nikaambiwa maombi yote ya wenye sifa na wasiokuwa na sifa yatapelekwa mkoani kwa ajili ya kupitiwa tena.

Nikajitutumua mpaka ofisi za CWT mkoa kuonana na katibu mkoa. Akanionyesha rundo la maombi akaniambia ameyapokea kutoka wilaya zote za mkoa na anafunga safari kwenda Dodoma kuyapeleka kwa ajili ya mchujo. Katibu hakuniruhusu kuyapekua kuona kama maombi yangu yapo au kujua kama jina langu lipo. Maana aliniambia ni siri. Hapa pia waliopata au kukosa sifa hakuna anayejua.

Huyu katibu mkoa alinieleza mengi sana yanayohusu chama pamoja na ufisadi mkubwa. Mfano alinionyesha gari (Prado) iliyokuwa imepaki nje ambayo ni ya katibu mkoa. Ilionekana ni mbovu hata tairi haina. Kwa maelezo ya katibu huyo aliniambia kuna spare moja ilichomolewa kwenye hilo gari kisha ikaenda kuhifadhiwa nyumbani kwa katibu aliyekuwapo kabla yake. Lengo la kufanya hivyo ni ili viongozi waipige mnada kwa bei nafuu na wainunue wao wenyewe kisha wakachukue hiyo spare ndani waifunge gari inakaa vyema.

Baadaye wakatoa orodha ya majina 100 na ushee kwenye magazeti kwa ajili ya nafasi hizo 12 na waliitwa Dodoma kwa ajili ya usaili. Katika orodha hiyo nikaona jina la jamaa yangu tuliokuwa college mate. Nikampigia kumuomba anipe ABC za mchakato mzima. Akanieleza kuwa ni mchakato mrefu mno. Na yeye mpaka kufikia hatua hiyo yeye alikuwa pro-Seif (Katibu aliyepita). Wakati katibu huyo anagombea hiyo nafasi huyu jamaa yangu alikuwa mmojawapo wa wapiga kampeni. Mpaka sasa huyo jamaa yangu ni katibu wa wilaya X.

Kuna watu wanaitwa KUT (KAMATI YA UTENDAJI TAIFA). Hawa kiufupi ndio wanaosaili watumishi wa CWT na kuwaajiri. Ila katibu mkuu ndio Boss. Akisema yes hakuna wa kupinga. Kila mkoa una KUT mmoja. Sasa wako MaKUT walio upande wa katibu Mkuu na wengine wako against. Hapa unapotokea usaili katibu anakuwa ameshawasuka KUT walio upande wake wanapiga kura kupata waajiriwa wapya. Kwa hiyo katibu mkuu anakuwa na kazi ndogo sana wakati wa kampeni maana ana network (makatibu wilaya waliopata nafasi zao kupitia mwamvuli wake)

Wakati wa uchaguzi ngazi ya wilaya bila rushwa hutoboi. Yupo jamaa yangu alijaribu kugombea nafasi ya uenyekiti wilaya. Hakufika popote kwani hakuwa na pesa ya kulisha watu na kugawa mlungula.

Kwa yanayoendelea sasa ndani ya CWT ni dhahiri kuwa wanachama tumechoka kulaghaiwa. Ikiwezekana tuifute CWT tuanze upya.

Kiukweli CWT ni kama dude lenye mizizi mirefu isiyoyumbishwa na yoyote. Kuanzia ngazi ya wilaya mpaka Taifa. Mambo mengi ni siri sana kuyajua.

Haya niliyoandika hapa ni baadhi tu ya niliyopata wakati najaribu bahati yangu na pia mahojiano niliyofanya na KUT wa mkoa wangu, katibu wa mkoa na huyu jamaa yangu ambaye ni katibu wa wilaya X.
 
Back
Top Bottom