Cv za wake za watu!

Maana yake anamtaka boss

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
We si umeseha huonyeshi jinsia ..??? nakunukuu sehemu ya post yako # 44 ... CV yangu haina Jinsia, Umri, marital status wala dini ...... mwisho wa nukuu. Ndo nikakupa mfano huo... ACHA UBISHI USIO NA MAANA


Haya mkuu, ila haibadilishi ukweli kwamba CV yangu haina hivyo vitu! mwisho wa siku unaweza kuifanyia nini kampuni/mwajiri.
 
Mkuu, kuna watu wao ni ubishi....wanawekewa link za ushahidi wa kinachosemwa bado wanabisha tuuu.... JAMANI KAMA HUNA DATA USISEME CHOCHOTE MAANA UTAKUWA UNASAMBAZA UONGO TU

Hivi hayo makampuni yakisema yanataka watuma maombi wa Kisukuma tu tena Wakristo, ni sawa?
 

Tena hata hizo habari binafsi zenyewe wakati mwingine inabidi uangalie jinsi gani zinahusiana na kazi unayotaka kuiomba na ikibidi uondoe zisizo na ulazima sana au hazina uhusiano wa moja kwa moja na kazi unayoomba.
 
Tukirudi kwenye uzi, kama mwanamke kaandika hivyo kwenye CV yake huenda ikawa anaishi na mtu bila cheti cha ndoa, akiandika ameolewa watataka alete cheti cha ndoa. Ili kuepusha matatizo anaamua kuandika single.
 
Hivi hayo makampuni yakisema yanataka watuma maombi wa Kisukuma tu tena Wakristo, ni sawa?
KUNA VITU VIKO OBVIOUS HATA KAMA HAWASEMI... HIVI UNADHANI MTUNZA HAZINA WA MSIKITI ATAKUWA MKRISTU..?? AU MTUNZA HAZINA WA PAROKIA AU KANISA ANAWEZA AKAWA MUISLAMU..???? au MKALIMANI WA KIINGEREZA KWENDA KISUKUMA SI ANATAKIWA ANAYEJUWA HICHO KISUKUMA...??? Acha bana.... hivi tunavyobishana hapa, Kuna watu wanaiandika biblia kwa kingoni... niambie atakayetakiwa hapo ni nani...

 
Tukirudi kwenye uzi, kama mwanamke kaandika hivyo kwenye CV yake huenda ikawa anaishi na mtu bila cheti cha ndoa, akiandika ameolewa watataka alete cheti cha ndoa. Ili kuepusha matatizo anaamua kuandika single.
Sawa, ila ategemee lolote baada ya mumewe asiye na cheti naye cha ndo kugundua hilo.... YAANI HUYO HANA TOFAUTI NA ASIYEKUTAMBULISHA KWA YEYOTE KAMA WEWE NI MUMEWE/MKEWE
 

Atatakiwa yule ambaye yuko fluent katika Kingoni bila kujalisha sana hayo mengine. Mambo ya kama kaoa au la hayahusiki kabisa hapo. Kinachohusika ni kujua Kingoni kwa ufasaha wa kutosha na kumridhisha mwajiri. Mambo ya ana watoto wangapi hayahusiki kabisa. Mambo ya kama yeye ni shoga au la hayahusiki.
 

Kuna tangazo la kazi niliona ambatanisha cheti cha kuzaliwa
 
Mbona hilo na mtunza hazina hujibu..??? Mr Nyani Ngabu umeshakonwa hapo
 

Mwanasheria utamjua tu!
 
Halafu nyie watu mmefundishwa wapi kuandika hizo resumes ambazo mnaweka marital au relationship status zenu?

That's just so unprofessional.
Kiranga come see this foolishness.
si bora hiyo wengine ni mwendo wa
''married with two children!aged 11 and 6yrs!''
khee!
 

Kikawaida unapoandika tangazo la nafasi za kazi basi unaweka na qualifications. Kama nafasi ya kazi ni mweka/mtunza hazina wa msikiti basi unaweka wazi sifa unazozitaka - mfano, applicant lazima awe na elimu ya uhasibu, tajiriba ya miaka kadhaa katika fani husika, pia unaweza ukaweka unapendelea Muislamu lakini hata wa dini zingine nao wanakaribishwa kutuma maombi na dini zao hazitatumika kuwanyima hiyo fursa endapo watakuwa na sifa zote zinazokidhi mahitaji ya hiyo nafasi.

Na mkalimani wa Kiingereza kwenda Kisukuma unaweza ukasema unahitaji mtu mwenye kuongea na kuandika kwa ufasaha lugha zote mbili bila kujali kama mtu huyo ni Msukuma ama Mwingereza, kabila lingine, au hata utaifa mwingine. Halafu chini unamalizia kwa kusema wewe ni mwajiri unayezingatia fursa sawa kwa wote bila kujali rangi, dini, kabila, umbile, mwelekeo wa kijinsia, asili, wala hali ya kindoa.

Haya nimekujibu sasa.
 

ngoja nitume cv yangu asee

Neene:ngati mwenyee dadii aniitili kadala
Mau:kachiki
Daadi:kadoda
mngana:si mwenye yule pasiko wa pale kumfaranyaki
lihengu:mtumishi lejio maria
uzoefu:ngati kila dominika nihudumiii kweeli ku misa,kuimba kweeeli nyimbo za Mama
shule:ku perahamiho kula kwa baba buruda wenyee mwaka nikosiwi neene
cc Fixed Point, Mzee tupatupa kipipi moto2012 na wengine wooote wenye mapenzi mema
bila kumsahau my gal Kaunga
 
Last edited by a moderator:

Hizo takwimu unazoziongelea zipo wapi?
SABABU INAYOWEZA KUFANYA WATU WADANGANYE KUHUSU MARTIAL STATUS ZAO
1.Ukishaolewa maana yake utazaa,ukizaa utakuwa na uwezo wa kuwepo kazini kama mwali wa kawaida kwasababu utakuwa na majukumu mengi,mara martenity leave,mara mtoto anaumwa,so ili kuhakikisha wafanya kazi watakokuwepo kazini wakati mwingi wanapewa kipaumbele wale wasio majukumu mengi na pia isitoshe yule ambaye hajaolewa anaweza kuenda anytime anapohitajika sio kama aliye kwenye ndoa au mwenye watoto.
Kama mke wangu ameandika single kwenye CV yake nitamuuliza kwanini amefanya hivo ili nizisikie sababu zake!
 

In real world, wanaozaa wengi wao wanazaa nje ya ndoa maana yake hawajaolewa na hawaishi na baba watoto zao nyumba moja. Tena ni bora aliyeolewa kwa sababu mume anaweza ku take care some other inconveniences.

Na asiye na watoto anaweza akawa mtegaji wa kazini kwa sababu hakuna kitu kinachomsukuma kwenda kazini, mwenye watoto lazima ajitume kulisha watoto.

Kuweka jinsia kwa mbali naweza kukubaliana nayo kwa sababu inategemea na aina ya kazi. Kama nataka kuanzisha bar/danguro then nitaweka masharti applicant anatakiwa awe msichana labda 18-24yrs old, au kama nataka kuajiri watu wa kushusha na kupandisha injini za magari manually hapo nitasema lazima applicant awe mwanaume wa miraba kadhaa.
Hiyo ni mifano tu unaweza ukapata mifano mizuri zaidi ya hiyo.

Kuweka marital status kwangu mimi bado ni upumbavu sioni ina faida ipi kwenye kazi. Ndio maana kwenye nchi za dunia ya kwanza kwenye kujaza form za kuajiriwa (sio kwenye CV/resume) kuna sehemu wanauliza labda " can you relocate?" hapo unaweza ukasema yes au no kulingana na situation yako.
 
Nakubaliana na wewe 100% hakuna umuhimu wala haja ya kuweka martial status kwenye CV kwasababu haihusiani kivyovyote na utendaji wako wa kazi!
 
Jamiiforums ni darasa tosha, Nyani Ngabu nakubaliana na wewe kabisa hakuna ulazima wala mantiki ya kuweka Jinsia, sex orientation, dini, kabila au marital status kwa sababu hazina uhusioano wa moja kwa moja na utendaji wa kazi. Ila umri nadhani ni muhimu kumwezesha mwajiri kujipanga muda alionao kukunyonya baasi!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…