Ni mbunge aliepotoka! Hajiulizi kwanini mpaka leo Jamii forums bado ipo na inazidi kuboreshwa, nilidhani watu kama yeye ndio wangekuwa mstari wa mbele kushauri mambo gani yafanyike ili kuendelea kuimarisha uhuru wa habari ndani ya nchi yetu.......lakini bure kabisa huyu bwana!
Kuna members ambao ni wabunge humu, tafadhali nendeni mkampe taarifa kwamba asione kwa vile yeye ana platform ya kusemea(Bunge) ndo keshamaliza kila kitu, sisi wananchi wa kawaida tupo na tutaendelea kuwepo uraiani hata pale yeye atakapomaliza term yake pale mjengoni.