CV ya Dr Slaa From Certificate to PhD

CV ya Dr Slaa From Certificate to PhD

Status
Not open for further replies.
Wewe unafuatilia PHD halali za watu wakati sisi tunahangaika na waliomteka Dr Ulimboka na wanaotaka kuwauwa viongozi wetu watetezi wa haki.

Akili zingine za ajabu kweli????

Mtu akitembea huangaza pande zote ili kulinda usalama wake!
 
Jana katika kijiwe kimoja maarufu maeneo ya msamvu moeogoro nilishudia vijana wakirushiana maneno makali na mwisho kupigana.
Chanzo walikuwa wakibishania slaa kuitwa Dr. na wengine wakipinga kwa madau eti huwezi kuwa na PhD bila bachelor na masters, ili kuamua ugomvi huo tulilazimika kuingia kwenye mitandao na kupata source mbalimbali lkn wote kukaafikiana kuitumia ile ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.tulikuta.naomba nawe uyaputie tujiulize je?hii ndio cv sahihi ya slaa katika nyanja ya kitaaluma?

School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993 1993 CERTIFICATE
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985 1985 CERTIFICATE
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural
Development 1980 1981 ADV
DIPLOMA
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977 1981 PHD
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974 1977 CERTIFICATE
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972 1973 CERTIFICATE
Itaga Seminary School A-Level Education 1970 1971 HIGH
SCHOOL
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966 1969 SECONDARY
Karatu Primary School Primary Education 1962 1965 PRIMARY
Daudi Primary School Primary Education 1961 1961 PRIMARY
Kwermusl Primary School(Mbulu) Primary Education 1958 1960 PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992 1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985 1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982 1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982 1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977 1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic
Church Padre 1977 1991
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
CHADEMA Secretary General 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu
Constituency) 1995 Todate
CHADEMA Member of National Executive
Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch(Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
 
mkuu haieleweki, hapo hakuna LL.B wala LLM , ila naona phd Laws , sielewi, haha, imekaa kisiasa zaidi..
 
Ndy maana anatabia ya kupinga hata jambo lenye ukweli.
 
Mmmmmh mmmmmh... Dr gani hii jamani hata base haina? kweli siasa kuna tulio zaliwa nayo na kuna walio ikurupukia. Sasa huyu babu haoni kama ana jidhalilisha na CV ya namna hii?

Ila kuna msemo una sema, ukiwa "CHONGO" kwenye nchi ya vipofu, basi wewe ndio unakuwa mfalme. CHADEMA na jumuiya zake zote hakuna mtu wa kupepelusha CV yake ndani ya CCM.
 
Wewe unafuatilia PHD halali za watu wakati sisi tunahangaika na waliomteka Dr Ulimboka na wanaotaka kuwauwa viongozi wetu watetezi wa haki.

Akili zingine za ajabu kweli????

Mkuu!

Ndio tatizo la KUBINAFSISHA AKILI. Kila analo ambiwa na BWANA wake inakuwa NDIYOOOOO!!!!!!!!!! Kama kile kibwagizo chao kule Bungeni!
 
mbona kuna wenye phd za kusomea miezi mitatu tu........................! nadhani waliomtunuku waliona anastahili, mbona huhoji kusoma certificate ya miaka mitatu kwa mtu aliyetoka form six?
 
Tatizo la kuto kujitanua na kujua mambo kote duniani sawa na Tanzania, mitaala ya elimu imetofautia nchi na nchi ko usidhani kama duniani kote mtaala unao tumika sawa na Tanzania, alafu chuo kilicho mtunuku hiyo DR kina vigezo vyake vya kudahili ko kwa mana hiyo Dr Slaa alikidhi vigezo vyote. Kwa msaada ukiendelea na akili ya kukalili mambo itakutesa sana hebu jitanue unatia aibu
 
Msiopitia elimu kubwa mna matatizo sana. Advance diploma (AD) inapewa hadhi sawa na degree moja, that's why mtu mwenye AD anakwenda moja kwa moja Masters. Swali lako laweza kuwa kwa nini Dr Slaa hakupitia Masters? Jibu ni kwamba zipo Thesis za Masters zinazopewa hadhi ya PhD na hivyo mhusika kupewa PhD moja kwa moja. Hata hapo UD , kule SUA na vyuo vikubwa duniani wapo watu wa aina hiyo. Muulize Slaa vizuri pengine thesis yake ya masters ilipasishwa kumfanya apate PhD. Lakini pia zamani kuna vyuo ambavyo vilikuwa vinatoa certificate zenye hadi ya advance diploma. Kumbuka mabadiliko ya elimu yametokea hivi karibuni. Zamani mtu angeweza kuwa profesa bila kuwa na PhD lakini kwa sasa hivi haiwezekani. Nakushauri uliyeleta mada hii upitie kwanza mifumo ya Elimu ya miaka aliyosoma Dr Slaa, kisha upitie chuo na chuo uone standards za kila chuo ndio utoe lawama.
 
Slaa ni mtu wa dili na mambo rahisi rahisi tangu zamani, si kwenye elimu hadi kwenye ndoa...
 
Hamjui PhD inavyopataika kwa mtu Adv Dip?ameungasha Master ndani ya hiyo PhD.
 
Kuna Maswali mengi sana ya kujiuliza kwenye hii elimu, siitofautishi na ile degree ya mrema ya miezi 6
 
Yeye Dr.Slaa kaipata kwa kusoma,baba yako Jei Kei ya kwake kapataje?wewe mwenyewe elimu yako unaikumbuka ulivyochakachua?
 
Msiopitia elimu kubwa mna matatizo sana. Advance diploma (AD) inapewa hadhi sawa na degree moja, that's why mtu mwenye AD anakwenda moja kwa moja Masters. Swali lako laweza kuwa kwa nini Dr Slaa hakupitia Masters? Jibu ni kwamba zipo Thesis za Masters zinazopewa hadhi ya PhD na hivyo mhusika kupewa PhD moja kwa moja. Hata hapo UD , kule SUA na vyuo vikubwa duniani wapo watu wa aina hiyo. Muulize Slaa vizuri pengine thesis yake ya masters ilipasishwa kumfanya apate PhD. Lakini pia zamani kuna vyuo ambavyo vilikuwa vinatoa certificate zenye hadi ya advance diploma. Kumbuka mabadiliko ya elimu yametokea hivi karibuni. Zamani mtu angeweza kuwa profesa bila kuwa na PhD lakini kwa sasa hivi haiwezekani. Nakushauri uliyeleta mada hii upitie kwanza mifumo ya Elimu ya miaka aliyosoma Dr Slaa, kisha upitie chuo na chuo uone standards za kila chuo ndio utoe lawama.
Unatetea ufisadi wa elimu kwa kuwa umefanywa na mtu umpendaye?????????
 
Ndahani,
Ni haki Yao kujadili. Msiwapuuze wala kuwakatisha tamaa kujadili. Inawezekana kweli wapo ambao kwa nia njema hawajui mfumo wa Elimu wa Kanisa Katoliki ambao tok a Seminary Ndogo ( Form 1-V1) nimepitia Dungunyi Seminary and Itaga Seminary of which am very proud na ninatoa shukrani za dhati kabisa kwa waalimu wangu wote si tu kwa kunipa elimu bora, Bali pia kwa kunipa misingi imara ya malezi( formation) kwani elimu bora ni zaidi ya vyeti.

Aidha si wengi wanaojua Philosophia hasa wanafundisha nini. Kwa bahati mbaya kuna watu wanadhani wameelimika na kuwa mavuvuzela kumbe hawajui kitu, ndio maana ya msemo " nusu elimu ni hatari sana". Kuna watu Leo ukiwaambia kuwa masomo ya philosophia( falsafa) yanahusu subjects muhimu Kama 1) Ethics 2) Logic 3)Epistemology 4) Cosmology 5) Metaphysics 6) Psychology na philosophy yenyewe yaani misingi ya philosophy hawaelewi unazungumzia nini na si kosa lao. Kuhoji is not an issue, issue ni je anayehoji anahitaji kujifunza au anahoji kwa ushabiki tu! This is the issue at stake!

Wako watu wanafikiria Seminary Kuu unajifunza Theolojia ( Tauhidi). Hawajui kabisa kuwa miaka 5 ya masomo ya Theolojia ni pamoja na complete course on Sociology, Anthropology, Oratory,miezi Sita ya mwisho nilipata complete course ya ukunga kwa kuwa ukiwaambia Padre vijijini wewe pia ni ambalance, hivyo lazima ujue basics za kumhudumia mama mjamzito unayemkimbiza hospital ini na kadhalika. Msomi yeyote, kabla ya kuhukumu anaanza kwa kutafuta ukweli juu ya jambo na kufanya utafiti. Prospectus ya Seminary Kuu ambazo ziko affiliated kwa vyuo vikuu mbalimbali duniani zinapatikana, hivyo hakuna msingi wa mtu kufanya guess work, labda awe tu na sababu zake na au agenda yake ambayo nintofauti na lengo la elimu ambayo ni kutafuta "full truth" ambayo nayo ni msingi wa Somo la Epistemology katika masomo ya Philosophy(Falsafa).

Katika Vyuo vikuu, ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Urbaniana ( Roma) nilikosoma Mimi, pamoja na miaka 7 ya Seminary Kuu nilizosoma (Kibosho Major Seminary/ Moshi na Kipalapala Major Seminary ambazo zilikuwa affiliated kwa Kwa Makerere University na Ndiyo maana vyetu vyangu ni vya Makerere University na Urbaniana Pontifical University Rome, 1) Nilianza na Bacclaureate ( equivalent ya BA) na kuandika Paper baada ya Course Work, na Licentiate ( Masters) nayo nikaiandikia Paper na kufaulu, ndipo nikaruhusiwa kuendelea na JCD).
2) Napennda pia kuwafahamisha kuwa wengi kwa kutokuelewa wanafikiria kuwa JCD inafundisha tu Canon Law. Pamoja na Canon Law masomo mengine ni 1) Civic Law ( ambayo ni msingi wa sheria zote inayotokana na Roman Law), 2) Family Law( ikumbukwe Kanisa Katoliki ina mfumo kamili wa ki mahakama kuanzia Courts of First Instance hadi court of Appeal ( Sacred Rota) na Supreme Court ( signature Apostolica). Huu ni mfumo kamili wa ki mahakama, kwa kawaida ukijishughulisha na maswala yote ya ndoa,na Patrimony. 3) Jurisprudence 4) comparative Law French, Commonwealth, American, Russian kwa maana nyingine all major Legal Systems worldwide. 5) International Law na branches zake zote. 6) Principles of criminal Law ( elements ambazo haiku kwenye Comparative Law na Civic Law.

Ili kufanya Desertation yangu, nilipaswa kujifunza Lugha 5 ( nje ya Kiingereza ambayo kwa wanafunzi wa English Speaking Countries inahesabiwa kuwa Mother Tongue, Latin ambayo kwa aliyetoka Seminary Kama nilivyopitia Mimi inahesabiwa Kama original language, na Hebrew ambayo pia kwa mtu aliyepitia Seminary it was taken as on Original language, japo Mimi sikuwahi kujifunza Hebrew Seminarini). Hivyo nikachagua a)Ki Italiano ambayo pia ndiyo ilikuwa Mwdium of Instruction yaani lugha ya kufundishia,b) Kijerumani c)French d) Spanish na e) Portuguese. Hata hivyo focus yangu ilikuwa kwa Italian na German na mengine matte nilijifunza kuweza kufanya research yangu, na kuniwezesha kusoma lakini Siko fluent katika kuzungumza.Hii pia ni kutokana na muda mfupi. Nilipata course ya Wiki 3 tu ya kujifunza Lugha kabla sijaingia darasani kwa masomo proper.

Nimeyaweka kwa uwazi, na ninadhani wako wanaofahamu mfumo wa masomo katika vyuo vya Kanisa Katoliki wanaweza kujazia. Wako ambao tumesoma nao was mapadre katika Pontifical Universities za Rome, Leo wanashika nafasi kubwa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au nafasi zinging mbalimbali kwenye Taasisi mbalimbali. Kwa kuwa nilienda Roma nikiwa tayari Mkurugenzi wa Maendeleo Jimbo Katoliki la Mbulu, nikawa Nina shuttle Kati ya Pontifical University ya Urbaniana na Pontifical University ya St. Thomas Aquinas, Rome ambako nilisomea Advance Diploma ya Rural Development.
Nadhani sasa mnaweza kupima kwa vigezo hivi hoja za mleta thread hii. Mnaweza kupima nini ni puma na nini ni mchele. Mnaweza pia objectively kuangalia depth ya masomo kwa kulinganisha na propaganda nyingi zinazopigwa kwa malengo tu ya upotoshwaji na au Propaganda. Vyuo vikuu Biko kwenye mitandao, mleta thread na wengine wa aina yake wakijisumbua kidogo tu kuingia kwenye Google watapata ukweli bila kutafuniwa na mtu. Tuweke uvivu wa kufikiri pembeni tunapojadili mambo makubwa na mazito. Nafasi ya kila mmoja kujipatia Elimu bora ipo Kama watu tutakubali kujisumbua na kuacha uvivu wa kufikiri. Nchi haitaendelea kwa propaganda na otoshwaji, Taifa halitaendelea kwa wivu....shika Kitabu. Soma. Jichimbie utavuna lakini Kama utakesha kwenye mitandao kufanya Propaganda badala ya kuchota elimu bora tena ya bure kwenye mitandao utaachwa unajiozea! Nawahimiza wote wenye kupenda Taifa lao kujichimbia. Innovation ni msingi wa maendelo na Innovation haipatikani kwa majungu na umbeya inapatikana kwa wanaochimbia vichwa vyao kwenye utafiti, kujisomea na kujiendeleza. Tupende Taifa letu, uzalendo uwe kwa matendo na sio Maneno matupu.




Nadhani sasa mnaweza kupima hoja ya mleta thread hii kwa vigezo nilivyoweka hap,



Basi tumvue udokta ili udokta pekee utakaobakia utakuwa ni ule wa kupewa kwa kutumia kura ya veto na sio kukaa darasani. What difference does it make? You can be a doctor and yet you deliver nothing!
 
usitumie muda wako mwaingi kushindana na hawa Gambaz brother,jibu liko wazi,Slaa yeye kaipata kwa kubukua,baba yake huyu kiumbe(Jei Kei)yeye hizo phd zake zi zile za akina Kikula na mshahara aliopewa alipopeleka ujumbe wa Bush kule Kenya?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom