CUF yatangaza kutoshiriki uchaguzi wa Arumeru Mashariki

Kwa hili cuf nawapeni pongezi hamna haja ya kuingia gharama kubwa wakati kushinda ni ngumu
 
Uwezo mdodo wa uelewa! Hawana utaratibu wa kushiriki uchaguzi mdogo waliokuwa 3 katika uchagui mkuu!
wewe utakuwa miongoni mwa 90% ya matokeo ya form iv mwaka huu
 
Kwa hili cuf nawapeni pongezi hamna haja ya kuingia gharama kubwa wakati kushinda ni ngumu
Kama uchaguzi ni gharama kwanini usiwashauri CUF wavunje chama wasiwe wanahangaika na gharama hizi.
 
Ah! mm sioni kuwa sababu ya mtatiro kama ina mashiko yeyote Jussa amesema hata uchaguzi wa Uzini walitokea watatu katika uchaguzi mkuu, leo hatushiriki kwa sababu tulitokea watatu yupi mkweli? mm nafikiri sababu ndio ile ile Arumeru wako wakiristo wengi na watu wa bara.
 
Chama cha wananchi CUF kupitia naibu katibu mkuu wake Julius Mtatiro wametangaza kutokushiriki kugombea kiti cha ubunge jimbo la Arumeru,hii ni baada ya kugundua kwamba hakuna uwezekano wa kushinda kutokana na historia yake kwenye chaguzi zilizopita.
 
watailaumu ccm sana mwaka huu na hivi imeweka wagonjwa karibu majimbo hamsini watakoma.

chaguzi ndogo zipo nyingi tu na bado miaka minne,ccm walifurahia kupigia kampeni watu waliostahili kuwa icu walitegemea nini?
nashauri watafute wafadhili wa kugharamia chaguzi ndogo kwani serikali iko ukingoni ki fedha.

haki sawa?..............................
 
Oh Yeah ni Chama Cha Mrengo Mmoja... sio Chama cha Tanganyika...

Sasa watakisema nini CHADEMA, angalau CHADEMA walishriki uchaguzi UZINI na kushidwa walipata kura 540 kwahiyo kuna Wana Chadema 540 Uzini...

Wataacha kuimba kuwa Chadema Chama Cha Wachagga Sasa??? wao Wamekimbia Arumeru....
 
Hawa jamaa huwa siwaelewi kabisa. Na huyu Mtatiro hajui kuitumia ile sauti yake nzito. Angekuwa anasema "peopleeeeez"
 
Ni uamuzi mzuri na wa busara,maana hii aibu ya sasa ingekuwa ni aibu ya kufungua mwaka...kama kwenye ngome yake kuu kule Zenji wameshindwa kuhimili vishindo,sasa kwenye eneo kama Arumeru huyo mgombea wao asingepata hata kura moja,namaanisha hata yeye mwenyewe asingejipigia kura.
 
CUF imetagaza kutosimamisha mgombea wa kiti cha ubunge arumeru kwa sababu kadhaa kwanza ni kuwa na historia ya kutosimamisha mgombea katika maeneo iliyokuwa ya tatu katika uchaguzi uliopita na pia kukiongezea nguvu chama pinzani chenye nguvu zaidi katika mapambano dhidi ya kukiondosha chama cha mapinduzi. Huu ni mfano wa kuigwa kama kweli watanzania tuna mpango wa kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani.
 
Rip kafu, with you it was unpleasant, without you it's even better
 
wamesoma alama za nyakati. Hongereni sana cuf kwa kuliona hili kwa jicho la tatu!
 
CUF imetagaza kutosimamisha mgombea wa kiti cha ubunge arumeru kwa sababu kadhaa kwanza ni kuwa na historia ya kutosimamisha mgombea katika maeneo iliyokuwa ya tatu katika uchaguzi uliopita na pia kukiongezea nguvu chama pinzani chenye nguvu zaidi katika mapambano dhidi ya kukiondosha chama cha mapinduzi. Huu ni mfano wa kuigwa kama kweli watanzania tuna mpango wa kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani.

Kama sio wanafiki watamke wazi tunaiunga mkono CDM
 
Madai ya CUF kujitoa uchaguzi wa Ingunga hayana msingi kabisa.. Kama wangejitoa kutokana na kutokuwa na imani na NEC chombo ambacho sii Huru ningewaelewa tena hata vyombo vya kimataifa wangeweza kuwapa support na pengine vyama kama Chadema TLP na vinginevyo vingepata nguvu wao pia kutoshiriki (kususia)..lakini kwa sababu ati walikuwa wa Tatu, sijui wanakata matumizi - haya maneno unawaambia wananchi wa Arumeru halafu kesho uje kuomba kura zao watakuelewa kweli?...Hivi CUF wamejiuliza mwananchi wa Arumeru mpiga kura ataielewa vipi statement kama hiyo?
 
Back
Top Bottom