CUF yatangaza kutoshiriki uchaguzi wa Arumeru Mashariki

Hizi chaguzi kila siku zinatugharimu Watz. mamilioni kama sio matrilioni ya shilingi. Ni bora jimbo libaki wazi mpaka uchaguzi mkuu na fedha hizo zitumike kwenye mambo mengine ya muhimu zaidi. Tunao zaidi ya wabunge 300 wakuhangaikia posho zao tu!
 
...uamuzi wao umezingatia ukweli kuwa hawajafanya jitihada yoyote kuweka mizizi Arusha.
Tunawaomba wafanye hivyo pia ktk uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2015.
 
Naibu katibu mkuu wa CUF Mtatiro ameongea na waandishi na kutangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa Arumeru mashari kwa sababu kwamba wanautaratibu wa kutoshiriki uchaguzi mdogo ambapo walikuwa namba tatu uchaguzi mkuu uliopita.Hata hivyo Mtatiro ametangaza kuwa CUF itaunga mkono chama cha chochote cha upinzani chenye nia ya dhati ya kumsadia mtanzania wa Arumeru.
Arumeru kule hakuna vikofia kwa mujibu wa Ismail Jusa
 
...uamuzi wao umezingatia ukweli kuwa hawajafanya jitihada yoyote kuweka mizizi Arusha.
Tunawaomba wafanye hivyo pia ktk uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2015.
mizizi yao ni pale kwenye vikofia ndipo wanapowekeza hii.ni kwa mujibu wa Isamil Jusa
 
CCM B imeona iachie CCM A kushiriki uchaguzi huo.....................hii ni aibu kwa chama kinachoanza kuchagua sehemu za kugombea je ni lini wataieneza CUF?
 
CUF Dar es salaam walilalamika kwamba CUF wanawekeza fedha zaidi kwenye chaguzi za zanzibar japo bara majimbo yake ndio makubwa ni moja ya maeneo wanayomalalamikia maalim Seif kuweka nguvu nyingi Pemba kuliko Unguja na bara.
 
Hizi chaguzi kila siku zinatugharimu Watz. mamilioni kama sio matrilioni ya shilingi. Ni bora jimbo libaki wazi mpaka uchaguzi mkuu na fedha hizo zitumike kwenye mambo mengine ya muhimu zaidi. Tunao zaidi ya wabunge 300 wakuhangaikia posho zao tu!

safari za jk za nje kwenda kuomba vyandarua na gloves ni gharama kuliko chaguzi ndogo.
 
Kushiriki uchaguzi si laziama ushinde nifursa ya kukitangaza chama kuonekana kipo hai.
 
hao wanazama baharini, na maneneo ya mwisho ya kuatapatapa,haya tunatuma boti ya CHADEMA kuja kuwaokoeni
 
Naibu katibu mkuu wa CUF Mtatiro ameongea na waandishi na kutangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa Arumeru mashari kwa sababu kwamba wanautaratibu wa kutoshiriki uchaguzi mdogo ambapo walikuwa namba tatu uchaguzi mkuu uliopita.Hata hivyo Mtatiro ametangaza kuwa CUF itaunga mkono chama cha chochote cha upinzani chenye nia ya dhati ya kumsadia mtanzania wa Arumeru.

Jusa alisema wao hawashindi penye wakristo wengi labda ndo sababu

Viva chadema tumeweza kuotesha miti hadi jangwani huo ndio ujasiri mkuu unaopaswa kupigiwa mfano na vyama kama cuf!!
 
Igunga na uzini ni chaguzi kubwa?hapo ndio sielewi

Igunga walishika nafasi ya pili mwaka 2010!Pia uzini walishika nafasi ya pili (Kumbuka kuwa nafasi ya uwakilishi CHADEMA haikushiriki mwaka 2010 ilishiriki ubunge wa JMT)!
 
Back
Top Bottom