Kwani anayedai kuwa koloni ni mtanganyika au mzanzibar? Tunasema hivi kama mnahisi mumeonewa sana na hakika mnahisia hizo, tamkeni mbele ya tume kuwa hamtaki muungano.
Mnaposema tuwe na mkataba kama wa Swiss(mwasheria wa unguja) kwi kwi! semeni mambo gani mnataka yawe ya mkataba?
Huyo aliyesema iwepo Tanganyika, nashangaa maana Tanganyika ikirudi hapo mtapoteza hata kidogo mlicho nacho.
Mkisema mkataba wa EU tunauliza wa mambo gani?
Sasa hivi Zbar ikijiunga na EAC kama nchi pekee itapoteza mambo mengi sana! hakuna nchi itakayokubali ubaguzi mnaowafanyia Watanganyika.
Tunachotaka kusema hapa ni kuwa tume hiyoo! sasa wekeni madumu ya mafuta na petroli pembeni Ongeeni hoja! ZNZ haitaki muungano, huku kumung'unya maneno ya mkataba wa Uswiss(mwanasheria wa BLW) ni upuuzi!
Tanganyika ikirudi kama alivyosema Mkandara muungano umekufa na ZNZ haitapata makataba wa Uswiss, Uchina, EU n.k
Lakini pia wanaotakiwa kudai Tanganyika wapo kimya! ninyi koloni mnawataka wadai wakati wao wana koloni!
Kelele zote sasa kimyaa! ukweli unadhihiri
LET ZNZ GO!
Hapana, hesabu zao ni kuwa Tanganyika ikirudi watakuwa na mambo yao na yale yanayowashinda watayaleta katika muungano. Hawana sababu ya kukataa muungano kama wanataka.Hapo kwnye red ndio kwenye mtego wa Wazenji kwa Tanganyiaka ili wapate sababu ya kuuvunja muunagano kabisa.
Hapana, hesabu zao ni kuwa Tanganyika ikirudi watakuwa na mambo yao na yale yanayowashinda watayaleta katika muungano. Hawana sababu ya kukataa muungano kama wanataka.
Ukitaka kujua hilo, hakuna hata mmoja anayesema vunja muungano. Wanajua wazi kuwa;
-Asilimia 7 ya pato la taifa wanalopata bure halitakuwepo.
-Wanajua kuwa soko lao la biashara na ajira ni Tanganyika wala si Kenya, Uganda n.k.
-Wanajua kuwa ukaribu wao na Zambia, Malawi, Rwanda n.k ni kwa vile wapo ndani ya Tanzania
-Wanajua kuwa mzigo wa elimu ya juu utakuwa wao
-Wanajua kuwa bajeti ya ulinzi na usalama itakuwa yao
-Wanajua ugumu wa kuwekeza kama si Watanzania
-Wanajua tatizo la ardhi leo na siku zijazo linalowakabili
Na kwa kukuthibitishia hili, hata siku moja hutasikia wakidai Passport zao kwasababu wanajua uwepo wa Passport ni kikwazo kwao. Ndiyo maana wanahangaika kutafuta njia za kubaki wakiwa wamejibanza kwa Watanganyika
- Mara wanataka uhusiano maalumu, ukiwauliza wa nini na kwanini isiwe SADC hawana jibu
- Wanataka uhusiano wa EU, ukiwauliza kwanini isiwe EAC hawana jibu
-Wanataka mkataba, ukiwauliza wa mambo gani, hawana jibu
-Sasa wamekuja na kiroja cha mwanasheria wa BLW kuwa tuwe na ushirikiano wa Swiss! kwi kwi! mwanasheria!!
Wao wanachotakiwa ni kupaza sauti katika tume kama walivyokuwa wanapaza katika mikutano ya UAMSHO.
Wasidai Tanganyika wadai ZNZ kwasababu wakiipata ZNZ ya neema automatically Tanganyika itakuwepo
LET THEM GO, LET ZNZ GO ASAP!
Joka kuu, ndio maana kila nikimtaja naweka kwiki za kicheko. Nadhani mimi kama wewe kuna kitu hatukielewi.
Ni jambo jema tukawaalika wanajamvi wote watusaidie. Hapa jamvini kahawa ilizunguka lolote linazungumzwa.
Hapa kwenye busati nimewaona hawa wafuatao wakiwa na kashata, na waje basi 'tuhangaike nao'
Wote kwa pamoja Wakuu;
Nonda, Takashi,Baru baru, Mwiba,Mkataba, Abdulsahaf,Toical, Jasusi, Ngongo, Jmushi1, Mzee Mwanakijiji, Mkandara, Kichuguu, sweke34, Pasco, Ben saanane, miss Judith, Mshikachuma,Ngambo ngali, Kimbunga, Nyani Ngabu, Ritz, Ogah, Mwita Maranya,chama nk
Wala hakuna doubt na elites wanavyowadanganya walalahoi. Utasikia mtu anasema mkataba, muulize uweje hana jibu. Fikiria hapa tumewauliza akina Baru baru, Nonda, Takashi n.k. hakuna anayekuja na kitu 'tangible'Nguruvi3,
..ingependeza kama AG wa Zanzibar na wenzake wangeweka details katika mapendekezo wanayotoa.
..naona kila mara wanakuja na jipya. hata suala la "muungano wa mkataba" mtu wa kwanza kumsikia akipendekeza ni huyu AG wa Zanzibar. sasa labda wangekwenda mbali na kuwaeleza wananchi ni nini kitakuwepo ktk huo "mkataba."
..nadhani hawa Zanzibari elites wanawadanganya walalahoi wa mitaani. hawawaelezi ukweli kwamba basically madaraka waliyonayo Zanzibar/SMZ ni very close to the maximum u can get in any form of union/federation/confederation.
Mkuu unajua wasema maneno mazito sana hapa.. Sasa inakuwaje tume hiyoo inakusanya maoni ya wananchi wao wanakuja na kusema tuunde serikali tatu, mara tuunde jumuiya kama ya Ulaya ya nini yote haya wakati jibu ni moja tu.. Wazanzibar hatuutaki Muungano - kwisha!. Vunja muungano - Toeni wote jibu moja tu sio kuitaka katiba iwe hivi ama vile wakati katiba hutengenezwa baada ya nchi kuwa huru. Hamuutaki muungano hii katiba mpya ya nini kwenu?..Kadhi kaingia mjini mnaitaka talaka humuitaki?.. semeni!Kwani anayedai kuwa koloni ni mtanganyika au mzanzibar? Tunasema hivi kama mnahisi mumeonewa sana na hakika mnahisia hizo, tamkeni mbele ya tume kuwa hamtaki muungano.
Mnaposema tuwe na mkataba kama wa Swiss(mwasheria wa unguja) kwi kwi! semeni mambo gani mnataka yawe ya mkataba?
Huyo aliyesema iwepo Tanganyika, nashangaa maana Tanganyika ikirudi hapo mtapoteza hata kidogo mlicho nacho.
Mkisema mkataba wa EU tunauliza wa mambo gani?
Sasa hivi Zbar ikijiunga na EAC kama nchi pekee itapoteza mambo mengi sana! hakuna nchi itakayokubali ubaguzi mnaowafanyia Watanganyika.
Tunachotaka kusema hapa ni kuwa tume hiyoo! sasa wekeni madumu ya mafuta na petroli pembeni Ongeeni hoja! ZNZ haitaki muungano, huku kumung'unya maneno ya mkataba wa Uswiss(mwanasheria wa BLW) ni upuuzi!
Tanganyika ikirudi kama alivyosema Mkandara muungano umekufa na ZNZ haitapata makataba wa Uswiss, Uchina, EU n.k
Lakini pia wanaotakiwa kudai Tanganyika wapo kimya! ninyi koloni mnawataka wadai wakati wao wana koloni!
Kelele zote sasa kimyaa! ukweli unadhihiri
LET ZNZ GO!
Wala hakuna doubt na elites wanavyowadanganya walalahoi. Utasikia mtu anasema mkataba, muulize uweje hana jibu. Fikiria hapa tumewauliza akina Baru baru, Nonda, Takashi n.k. hakuna anayekuja na kitu 'tangible'
Ahmed Rajabu kila siku anazunguka mbuyu, mara EU, mara Mkataba na matokeo yake sasa AG ameibuka na kituko kutoka Geneva. Ipo siku tutasikia muungano kama wa California na New York (mungu saidia na epusha njozi hizi batili).
Naunga mkono hoja yako kuwa sasa ni wakati WZNZ waweke details na specifics wanataka nini hasa.
Hivi utaongleaje mkataba kama huna japo 'frame work' yake
Hivi utaongeleaje serikali 3 kama hujui zita operate vipi!
Hapa WZN wana mawili
1. Sema muungano basi, tuvunje jahazi na Tanganyika ichukue mbao zake, ZNZ irudishe sarafu na passport
2. Sema YES muungano, weka details una propose nini
Nilisoma makala ya Zitto, japo sikubaliani naye katika baadhi ya hoja lakini nakubaliana naye kuwa alikuwa na details na specifics za muungano uweje.
Sikubaliani na AG wa Unguja kwasababu anabwaga neno swiss kama dumu la maji lisilo na mwanzo au mwisho
Sikubaliani na Ahmed Rajabu kwasababu hajawahi kutoa details za anachokihubiri zaidi ya kusema ZNZ itakuwa kama Dubai, watu watagawiwa pilau kila siku, makaimati yatagawanywa na mashekha kila asubuhi na uwezekano wa bomba la maziwa na asali kutoka Oman upo kama wznz watakuwa kitu kimoja!
Mkuu,..pia wa-ZNZ waelewe kwamba "UHURU" wanaoutaka hautapatikana hata ktk "muungano wa mkataba" unaofanana na EU.
Mwiba,
..EAC inaiga mambo ya European Union na wanapata msaada na ushauri toka huko.
..pia hujasikia wa-ZNZ wanapendekeza "muungano wa mkataba" ambao utafanana na EU??
..suala kubwa ambalo Tanzania haijakubaliana nalo ktk EAC ni ardhi, mengine tumekubali.
..pia wa-ZNZ waelewe kwamba "UHURU" wanaoutaka hautapatikana hata ktk "muungano wa mkataba" unaofanana na EU.
..hebu chukulia suala kama la SARAFU ambalo ni prominent ktk "muungano wa kimkataba" wa EU. Tanganyika inaweza kuamua ku-devalue sarafu halafu ZNZ mkaingia ktk mtikisiko mkubwa wa kibajeti na kiuchumi.
..serikali 3 is not the answer.
..huyo aliyependekeza serikali 3 hajui implications za hicho anachopendekeza.
..kukiwa na serikali ya muungano itakayosimamia serikali za TGK na ZNZ kutapelekea raisi wa muungano kuwa na madaraka juu ya maraisi wa TGK na ZNZ.
..pia tukumbuke kwamba ZNZ tayari ina serikali, ni TGK ambayo haina serikali. katika mfumo wa serikali 3 kitakachoongezeka, au kubadilika, ni TGK kuwa na serikali yake yenye mamlaka na majukumu kama iliyonayo serikali ya ZNZ iliyoko sasa hivi. kwa upande wa serikali ya ZNZ sidhani kama kuna kitakachoongezeka.
..kwa mtizamo wangu, serikali 3 does not solve matatizo ya muungano wetu. zaidi haitakidhi matamanio waliyonayo wa-ZNZ ya kuwa na mamlaka kamili ya kisiasa,kiuchumi,kijamii, na kiutamaduni.
..hatutaki serikali 3, hatutaki mkataba, LET ZANZIBAR GO!!!
NB:
..kuhusu baraza la mitihani, ZNZ wawe makini.
..muelekeo uliopo sasa hivi ni kuwa na mfumo mmoja wa elimu kwa nchi za AFRIKA MASHARIKI.
..kwa msingi huo sylabus, pamoja na baraza la mitihani, vitakuwa chini ya EAC.
Mbona hizi habari hatuzisikii kutoka upande wa tanganyika ,Za zanzibar zinatangazwa kama mpira ama kweli zumari ikipulizwa Zanzibar walio maziwa makuu huhemkwa !