RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Katika hali isiyo ya kawaida na baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu dhidi ya kile kinachokiita “njama za makusudi dhidi yake”, sasa Chama cha Wananchi (CUF) kinasema hakitaweza tena kuvumilia vitendo vya kihuni na kihalifu wanavyotendewa viongozi na wafuasi wake visiwani Zanzibar, kwani wameshasukumwa hadi kwenye ukuta.
Akizungumza na wakaazi wa Dunga Kiembeni, wilaya ya Kati Unguja, hivi leo (Februari 25), Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Mazrui, amesema hujuma ambazo zimepangwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea kwenye kile kinachoitwa ‘uchaguzi mkuu wa marudio’, zinakusudia kuiingiza nchi kwenye machafuko.
Akitaja mifano kadhaa ya vitendo hivyo vya hujuma, Mazrui alisema kitendo cha kuharibiwa kwa baraza ya CUF ya Dunga kilichofanywa usiku wa kuamkia leo kitakuwa cha mwisho kwao kukivumilia.
Chanzo: zanzibardaima.net