CUF YAING'ANG'ANIA CHADEMA Kuhusu USHOGA

CUF YAING'ANG'ANIA CHADEMA Kuhusu USHOGA

habariyamujini

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Posts
3,094
Reaction score
457
[h=2]CUF yaing’ang’ania Chadema kuhusu ushoga[/h]JUMAPILI, JUNI 02, 2013 07:51 NA MWANDISHI WETU

LICHA ya vyama vikubwa viwili vya upinzani, CUF na Chadema kuombana radhi kutokana na mvutano ulioibuka kuhusu suala la ushoga na kusababisha kuvunjika mara mbili kwa kikao cha Bunge hivi karibuni, CUF bado kimeonakana kutoridhika na hatua hiyo, MTANZANIA Jumapili linaripoti. Jana CUF ilisambaza taarifa yake kwenye vyombo vya habari ikidai kuwa kitendo cha Chadema kukihusisha chama hicho na ushoga kwa sababu tu ya kufuata sera za kiliberali na hatua ya kuomba radhi kwake ni kujifariji kuwa ujumbe wao tayari umefika na umesikika kwa Watanzania kama walivyokusudia.

Kabla ya kuombana radhi juzi, vyama hivyo viliingia kwenye mvutano mkali bungeni, baada ya Mbunge wa CUF kuomba mwongozo wakimtaka Msemaji wa kambi ya upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Hezekiah Wenje, aondoe maneno ya kukidhalilisha chama hicho.

Mvutano uliibuka wakati Wenje akielezea kuhusu itakadi ya vyama rafiki vya CCM, CUF na Chadema, ambapo alisema kuwa itikadi ya CUF ni ile ya kiliberali, inayounga mkono ushoga, usagaji na ndoa za jinsia moja.

Katika taarifa yake hiyo iliyotolewa jana na kusainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma, Abdul Kambaya, CUF ilidai kuwa kitendo hicho cha Chadema ni kiburi kinachofanywa na wabunge wa chama hicho ndani ya Bunge na kuendeleza matusi na ufedhuli, hali ambayo imedhihirisha kwamba adhabu zinazotolewa na na chombo hicho ni dhaifu.

“Pamoja na Mkuu wao wa Kambi rasmi, Freeman Mbowe kuonyesha kulazimika kuomba radhi, lakini sisi CUF tunaamini hili si la Hezekia Wenje pekee, bali ni mpango maalum wa Kambi inayojiita rasmi na kwa kauli nyingine, lilikuwa tamko la Chadema, kwani ndio wanaunda kambi hiyo peke yao, kwa hiyo kuomba radhi kwake ni kujifariji kuwa ujumbe wao tayari umefika na umesikika kwa Watanzania kama walivyokusudia,” ilisomeka sehemu ya taarifa.

Aidha CUF kilikishutumu Chadema kuwa ni chama cha wahafidhina kama kilivyo Chama cha Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon cha Conservative, ambao nao wanaunga mkono ushoga na ndoa za jinsia moja.

“Chama hicho pia kilisema International Democratic Union ni asasi ya vyama vya kihafidhina wenye mrengo wa kulia, hivyo Chadema hakina itikadi bali ni uhuni na ‘opportunism’.

“Vitendo vyao vinadhihirisha hawafai hata kidogo kuaminiwa na Watanzania. Chadema hawana itikadi, bali wanaangukia kokote ambako hela ziko. Majuzi walikuwa Kenya waliipigania ODM, ODM ni liberal party.

“Wakati wao wanasema liberal parties zinasimamia ushoga, at the same time wao wanakwenda kuwapigia debe liberals. Sasa kwa sababu ODM nao ni mashoga sielewi Chadema walipokwenda juzi ndo walikwenda fungate ya jinsia moja na ODM au la! Chadema wanapaswa kuileza jamii ili wapate kujibainisha juu ya itikadi sahihi wanayoiamini,” ilieleza taarifa hiyo ya CUF.

Chama hicho kilidai kuwa sera zao ziko wazi na hakuna tamko la viongozi au andiko lolote ambalo limetaja, limependekeza au kuunga mkono ndoa ya jinsia moja na kwamba inachokifanya Chadema ni siasa za kihuni na kitoto.

CUF pia kilihoji hatua ya Rais wa Marekani, Barrack Obama, kuja nchini kama atashutumiwa, kwani kabla ya uchaguzi wa 2012 aliunga mkono ndoa za jinsia moja.

Kilisema kuwa nchi ina matatizo ambayo vyama vya upinzani vilipaswa kujenga hoja kuikosoa serikali iliyoko madarakani na si kufanya siasa za kihuni na kitoto.

Mbali na kukituhumu Chadema, pia chama hicho kilisema Bunge na Serikali yake vimeshindwa kuwaadabisha Chadema, kutokana na hali iliyotokea hivyo kinawakabidhi kwa wanachama wao kwa nia ya kukilinda.
 
CCM imeshindwa kumridhisha CUF ? Toto la Kipemba lenye mivuto ya Kiliberali haliliridhiki na bwana mmoja. Aende huko Narea kwa wenzake, na asitukaribie kabisa Chademahatutaki michezo michafu
 
CCM imeshindwa kumridhisha CUF ? Toto la Kipemba lenye mivuto ya Kiliberali limemtamani Chadema.

Kwi kwi kwi kwiiiiiiiiiiii acha atani CHADEMA hatutaki kabisa huo mchezo ndiyosababu tukawapa MAKAVU LIVE
 
Asante sana kamanda Wenje, mwanzo sikujua maana ya Hakisawa kwa ote, kumbe ndo manayakeeee!
 
Back
Top Bottom