FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 733
Swala hili ni very sensitive. I don't support hawa jamaa kujilipua kwani hawezi solve tatizo. Bali nashangaa kwa nini JK anaweza kuwa kinyonga na kugeuka maamuzi ya Mkamba na Seif?
Nimepata siki more than 95% ya wabunge wa pemba ni CUF, sasa najiuliza jee ni haki kwa chama chenye wabunge zaidi 95% ndani ya pemba kutokuwa na wawakilishi ndani ya serikali? Wakati JK and CCM plays politic Wapemba wanashindwa kupata matibabu, wanashindwa kupeleka watoto wao kwenye shule bura sababu tuu walichagua CUF kwenye general election.
Pemba hata Umeme ni tabu, mafuta ni tabu, na pemba ndio wakulima wakuu wa visiwani kule.
I support swala zima la kutokutuma chakula unguja, however i condem swala la kujilipua mabomu.
Jarida hili linapotosha.
1. Wapi hapo inaonyesha 'wafuasi' wamesema hivyo zaidi ya mfuasi mmoja, muimba tenzi?
2. Huyo mwimbaji ana nguvu ya kutoa tamko la CUF au kutumbuiza?
3. Waandishi waliwauliza wasemaji wa CUF kuhusu hilo, au wameliachia achia jambo linaning'inia hewani ili waje kutudanganya 'CUF wametoa tamko?'
4. Pia, nipe nukuu ya hata sentensi moja ya maneno yake mwenyewe. Usinitafsirie peke yake. Tafadhali ndugu muhariri.
Jamani hawa waandishi ni waongo, wachovu. Hawana hiyo taaluma hata kama wameenda shule za uandishi. Mimi sio CUF lakini nataka ukweli kwanza, kabla sijajadili lolote. Bongo hakuna Media!
Hii habari ina nia ya kuuza gazti tu kwani alotoa rai ni tu mmoja na imeshakuwa CUF na kuonyehsa kuwa ni uchochezi walitumia jina la pili la huyo msoma utenzi ambaye jina lake ni Hamad ili kupotosha, mwandishi makini anayetaka ujumbe uwafikie wasomaji wake angetumia jina lake la kwanza ili kutafautisha baina ya Seif na huyo jamaa.
Ama katika hoja ya kutokupeleka mazao Unguja ni moja ya mikakati ya kudai haki na kama hoja ni kuathirika kwa wananchi wa kawaida ni sawa kwani ni wao wanaoshabikia kutokupatikana kwa Muafaka , ni wao na si viongozi waliokuwa wakipita katika magari na kukejeli wenzao. Kwa hivo wacha wasome kwa vitendo kuwa likiingia janga na wao wataathirika na kuhusu CUF walioko Unguja watavumilia au watazifata hizo bidhaa huko Pemba.
Lazima hatua zichukuliwe bila hivyo CCM watakuwa kila siku wanafanya watakalo wakijua kuwa kuna mazumbukuku wachache wanawashabikia.
Mimi naungana na waliopendekeza kuwa heading ya hii thread ibadilishwe!
Hivi kweli haya maneno wamesema CUF kweli?
hayo ndio mambo ya akili kweli? hawa ndio tuwaachie nchi watawale?
sasa jee watawaambia pia wahame unguja warudi pemba?
maana wanachekesha sana hawa watu na wavae mabomu na vifaru
warudi kwenye mazungumzo wazungumze sio vitisho na upuuzi
Umaskini uliokithiri wa ndugu zetu wa Pemba utakwamisha utekelezaji wa maamuzi haya ya kisiasa. Soko kuu la mazao yao ni Unguja na yeyote anayewakataza wasipeleke mazao yao huko hawatakii mema, anataka kuwaona wakifa njaa. Wenzetu waarabu wanajilipua lakini familia zao zinabaki kwenye mazingira mazuri, I dont think this will be the case kwa hawa ndugu zetu, viongozi waache kuwajaza wananchi ujinga wa kisiasa, there must be lots of other more meaningful and realistic options. Labda tunaweza kuwasaidia viongozi wa CUF kufikiri ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa hapa kabla mambo hayajawa mabaya kwa ndugu zetu.
MKANDARA
naomba kukuliza
How good is your knowledge of ZANZIBAR POLITICS?
Tafadhali naomba utujulishe hilo
siasa za vitisho hazijatatua matatizo; leo hii israel na palestina licha kulipuana na kuuana wamefikia karibu kwenye suluhisho la mgogoro wao kwa kiasi gani?
Kuna mambo mengine ni mazuri kutia hamasa lakini haya manufaa yoyote yale.