BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,102
Kama hili ni kweli, basi hawa CUF wanataka kutuletea balaa kubwa sana
CUF watishia kujilipua
na Mwandishi Wetu, Pemba
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
MWENENDO wa mambo visiwani Zanzibar unazidi kuwa wa mashaka, baada ya wafuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF) kutangaza kuwa wataanza kujivisha mabomu ya kujitoa muhanga kama njia ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kusaini makubaliano ya mazungumzo ya muafaka.
Sambamba na hatua hiyo ya kutisha, pia wamewataka wafanyabiashara kutoka kisiwani Pemba kutosafirisha mazao ya chakula kwenda katika Kisiwa cha Unguja.
Hatua hiyo ni tishio kwa wakazi wa Unguja wanaotegemea chakula kutoka Pemba na iwapo itatekelezwa, itasababisha maelfu ya wakazi wa kisiwa hicho kukabiliwa na baa la njaa.
Wito wa kujitoa muhanga kwa wana CUF kama njia ya kukabiliana na manyanyaso waliyodai kuyapata kutoka Serikali ya Mapinduzi, ulitolewa na mwimbaji wa utenzi, Saidi Hamad, mbele ya viongozi wakuu wa chama hicho.
Huku akishangiliwa na umati wa wanachama hicho wakati akisoma utenzi baada ya kumalizika kwa maandamano ya amani ya kuishinikiza CCM kusaini makubaliano ya muafaka, Hamad alisema wana CUF wako tayari kujivika mabomu ya kujitoa muhanga kutokana na manyanyaso na maumivu ya ubaguzi wanayofanyiwa na serikali.
Baada ya Hamad kumaliza kusoma utenzi huo, Mbunge wa Viti Maalumu wa CUF, Rizik Omar, ambaye alisoma risala mbele ya viongozi wa CUF, alisema Wapemba wote wanapaswa kususia kupeleka chakula Unguja.
Katika risala hiyo, wanachama wa CUF wanawaonya wakazi wote wa Pemba kuwa, atakayekwenda kinyume cha uamuzi huo wa kutopeleka chakula Unguja, atatengwa kwa vile atadhihirisha kuwa hana umoja na wenzake na hajali maovu wanayofanyiwa Wapemba na SMZ.
Hatua hiyo iwapo itatekelezwa, inaweza kuwa madhara makubwa zaidi, kwa kuwa Kisiwa cha Unguja kinategemea sehemu kubwa ya mazao na matunda kutoka Pemba.
Sambamba na hilo, wafuasi wa CUF pia wametakiwa kutotumia meli za serikali za mv Mapinduzi na mv Maendeleo katika safari wanazozifanya kati ya visiwa vya Unguja na Pemba.
Ilidaiwa na msoma risala huyo kuwa, Wapemba wanapaswa kugoma kutumia usafiri wa meli hizo kwa sababu zimekodishwa kwa mama wa kiongozi mmoja wa SMZ na mkataba wake ni wa kutatanisha.
Madai mengine ya kuwepo kwa migomo hiyo yaliyosomwa katika risala hiyo, ni Wapemba kutengwa katika nafasi za ajira serikalini na kwenye taasisi za umma pamoja na kutopatiwa nafasi za masomo na uongozi kama vile wao si sehemu ya Zanzibar au Jamhuri ya Muungano.
Akizungumza katika mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis, alisema anaunga mkono uamuzi wa wananchi wa Pemba ingawa atakuwa mmoja wa waathirika wa mgomo huo.
Alisema mgomo huo ni hatua nzuri kwa vile ni moja ya njia za mapambano ya kupigania haki na kukataa kudhulumiwa.
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alisema chama hicho kimefunga mlango wa mjadala na CCM juu ya suala la muafaka na kutangaza masharti yanayopaswa kutekelezwa kabla ya kurejea katika meza ya mazungumzo.
Aliyataja masharti hayo kuwa ni Rais Jakaya Kikwete kuwakutanisha na Rais Amani Abeid Karume, kama alivyofanya kwa Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, wakati aliposhiriki mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa wa Kenya.
Alisema kumkubali Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ni kupoteza muda na kuendeleza fani ya usanii ya CCM kwa sababu Makamba hana kauli wala uamuzi katika chama hicho ambacho kila siku kinabadili kauli zake.
Alisema iwapo Rais Kikwete atashindwa kutimiza sharti la kwanza, basi anapaswa kuhakikisha makubaliano ya pande mbili zilizokuwa zikishiriki mazungumzo ya muafaka yanatekelezwa kwa kusainiwa na wahusika na utekelezaji wake kuanza mara moja.
Kwamba njia hizo ndizo pekee zinazoweza kuinusuru Zanzibar isitumbukie kwenye matatizo makubwa zaidi.
Kwa upande wake, Prof. Ibrahim Lipumba aliuambia umati wa waandamanaji hao kuwa, amesikitishwa na kitendo cha viongozi wa serikali waliolazimika kuachia madarakani kwa tuhuma za kukiuka maadili ya uongozi kupokelewa kwa mbwembwe majimboni kwao mfano wa mashujaa.
Alisema viongozi wa serikali na CCM wilaya, kumpokea aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, kwa karamu nono za nyama choma na pombe ni kuwakebehi Watanzania walioiweka serikali ya CCM madarakani.
Lipumba alisema katika nchi inayozingatia misingi ya utawala bora, viongozi wanaokabiliwa na shutuma za aina yoyote hawapaswi kurandaranda mitaani, bali wanapaswa kuwa chini ya uchunguzi na wanapothibitika kutenda kosa huwa wanafikishwa mahakamani mara moja.
Alimkumbusha Rais Kikwete kutekeleza ahadi aliyoitoa bungeni ya kuwashughulikia mafisadi na kuinusuru nchi na watu wenye nia ya kuhujumu rasilimali za nchi kwa kuweka mbele tamaa zao.
Wakati CUF wakiendelea kulia na CCM, Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, Yusuph Makamba leo anatarajia kukutana na waandishi wa habari kuzungumzia maendeleo ya mazungumzo yao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara), George Mkuchika ilieleza mkutano huo ni muhimu kwa mustakabali wa Zanzibar na nchi kwa ujumla.
Wakati CCM wakitarajia kutoa maendeleo ya mazungumzo hayo, CUF wao walishaweka wazi msimamo wao kuwa hawatakubali kufanya mazungumzo na CCM kwani hatua waliyofikia ilipaswa iheshimiwe.
CUF walisema katika mazungumzo yaliyomalizika hivi karibuni walikubaliana namna ya kumaliza tatizo hilo, lakini kikao cha CCM kilichoketi Butiama kiligoma kukubali mapendekezo hayo.
CCM katika kikao chake iliweka wazi msimamo wake kuwa suala la muafaka au serikali ya mseto linapaswa kujadiliwa na wananchi wote na wala si chama au kundi la watu fulani.
Msimamo huo uliwakera zaidi CUF kiasi cha wabunge wao kuamua kutoka nje katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge mjini Dodoma kwa lengo la kushinikiza CCM kukubali mazungumzo waliyokubaliana katika mkutano wa muafaka.
Aidha, CUF iliamua kufanya maandamano nchi nzima kupinga uamuzi wa Butiama na kuwataka wananchi washirikiane nao kama ishara ya kukuza demokrasia hapa nchini.
Zanzibar imekuwa na mgogoro wa kisiasa tangu kufanyika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 na makubaliano mawili ya muafaka ya hapo awali kukwama, huku watu kadhaa wakipoteza maisha katika machafuko yaliyowahusisha wafuasi wa CUF na vyombo vya dola