CUF Wanachekesha; Wanapendekeza mabadiliko ya muswada...!

Mimi nilishangaa kumwona myaa wakati mbungeni nilimsikia kwa masikio yangu anasema. Serikali imeleta mswada mzuri hauna matatizo, wapinzani wanapotosha, lisu amewatukana wanzanzibar. Akampongeza kikwete na serikali kwa mbwembwe zote. Jana namwona ikulu amepeleka mapendekezo. Sasa najiuliza hivi myaa amekuwaje au ndo bendera fuata upepo, ama kweli cuf ni ccm b na itakuwa vigumu kujinasua.

Mnyaa angekuwa na uwezo angeifuta Tanzania bara kwenye ramani ya dunia!
 
Kwa mtaji huu wa kualika vyama vya siasa Ikulu, basi JK ameshageuka tume ya kuksanya maoni ya katiba mpya, tusubiri bunge la katiba!:crutch:
 
Julius Mwenyewe naona hilo jina la kazi, ukimuangalia vizuri kwenye paji la uso ni kama vile huwa anaswali kwa kubong'oka.
Comment za baadhi ya wana JF siku hizi, zinatia kinyaa...napata mashaka sana na mustakabali wa nchi hii ikiwa watu wenye comment kama hizo(bolded) watapewa nafasi za kutuongoza.

Cha kushangaza ni kuwa wakati vyama vinajitahidi kuondokana na kansa hii japo kwa sura ya nje..washabiki ni tofauti kabisa...hivi ukitazama picha hii hapa chini unajifunza nini????

magwanda.jpg
 
Strategically CUF wamejiposition katika sehemu ambayo wataalam wa product life circle wanaita EXIT.

img_businesscycle.jpg

Maana waliisha fika katika stage ya maturity kwenye siasa za upinzani sasa wana exit. Japo ni dhahiri kuwa CUF wana agenda ya siri katika kuchukua SMZ kwa kujaribu kuwahakikishia wahafidhina wa CCM kule visiwani kuwa CUF si tishio kwao kama watatawala Zanzibar. Huu muungano wao na CCM ambao unawabana kuanza kuzalisha tension kati ya CUF na CCM katika kutawala si tu kwamba unaimaliza CUF bara na kuidhoofisha visiwani bali unaondoa umuhimu wa CUF katika siasa za Tanganyika.

CUF mwisho wao rasmi ni 2015 pale watakapotokwa mapovu na kulia na kusaga meno baada ya CCM kuwageuka na kuwanyima ushindi kwa ya tano mfululizo na hakutakuwa na wa ku-sympathise nao tena kwa unafiki huu wanaouonesha sasa, ambao strategically kama CUF ingesimama kama chama cha upinzani na kuungana na CDM katika kupigania katiba nzuri ya wananchi wangekuwa wamejijengea nafasi nzuri sana ya kutangazwa washindi wa urais kule Zanzibar mwaka 2015.

Kitendo cha Maalim Seif kutumiwa kuwaagiza wabunge wa CUF nini cha kufanya ili kuwamaliza nguvu CDM siyo tu inaimaliza nguvu CUF bali inauondoa kabisa umuhimu wa CUF kama chama cha upinzani katika bunge la Jmahuri. Sishangai kusikia kuwa kuna internal friction kati ya Maalim Seif na Hamad Rashid. Strategically CUF ingekuwa ingeweza kuidhibiti CDM kama tu ingeonesha kuwa inaungana na CDM dhidi ya CCM bungeni kitendo ambacho kingewafanya wafuasi wa CUF kuendelea kuiamini CUF bara, kwa sasa ni dhahiri kabisa kuwa wananchi wasioridhishwa na utendaji wa serikali ya CCM na huko nyuma kuona CUF ni chama mbadala watatafuta chama kingine mbadala na haiyumkiniki itakuwa ni CHADEMA.

Kila mtu anafahamu fika kuwa CUF ilikuwa inaungwa mkono zaidi na watu wengi ambao ni waumini wa dini ya kiislam na hata huko nyuma ilifikiwa kuwa chama hiki ni cha kiislam. Jitihada za kuitangaza CDM kama chama cha kikatoliki zinazofanywa na CCM wakishirikiana na CUF zinalengo la kuwafungia ndani wanachama wengi wa CUF ambao ILMU dunia yao ni ndogo wasikimbilie CDM, lakini wanshindwa kujua kuwa wananchi hao hao mbali na dini yao wanatakiwa kupata matumaini ya kuishi vizuri dunia kabla ya kwenda peponi k maana ni dhahiri hawawezi kuwenda CCM. Sasa basi ni dhahiri kuwa CUF itakuwa imewakatisha tamaa watu hawa na mwisho wa siku watapambazuka na kuona kuwa propaganda dhidi ya CDM ni muendelezo wa maisha yao duni kwani hakuna wa kuwatetea zaidi hapa duniani zaidi ya hao CHADEMA ambao siyo tu wanaonekana kutetea watanzania bila kuagalia imani zao bali pia wanashambuliwa na serikali nzima na CUF wakiwamo katika harakati zao hizo.

Kwa hoja hizi ni dhahiri kuwa CUF imekosa ushawishi bara na kwa hilo CCM na TISS wanagonga glass ila wakisikia neno CHADEMA glass zinawaponyoka.
Huo ndio ukweli mkuu. Hongera kwa uchambuzi wa kina
 
hata kabla ya hapo CUF na CHADEMA walikuwa wanachiana majimbo (kama CDM kina nguvu jimbo fulani CUF walikuwa wanawaachia; lakini), CUF lengo lake ilikuwa na vyama vyengine vipate nguvu; lakini hali haikuwa hivyo baada ya CHADEMA kupata nguvu imepata bipolar ddisorder (mania) ya kutaka kuonekana ndio chama kikuu cha upinzani, nafikiri ndio ilikuwa ndoto yao kubwa hio; sijui kama watakuwa na strategy nyengine za kuendelea mbele mazali wameshapata kua chama kikuu cha upinzani.
CHADEMA hawakupaswa kuvisaliti vyama vyengine hasa CUF; halafu wamegeuka CCM badala ya kusema wao kama ndio wamewatosa wenzao hawataki tena kuungana na vyama vya upinzani wamewatupia CUF kosa hilo la jinai.

Nawaombea wananchi wa taifa hili amani na demokrasia ya kweli na sio ukahaba wa kisiasa.
 
Chadema iko Tanganyika tu

Wakati CUF iko Tanganyika na Zanzibar (pemba na Unguja)

Wabunge wa kuchaguliwa na wananchi ..

CUF inawakilisha Tanzania nzima while Chadema inawakilisha Tanganyika tu..
Siku hizi Tanzania nzima ni Lindi na Pemba pekee?
 
hata kabla ya hapo CUF na CHADEMA walikuwa wanachiana majimbo (kama CDM kina nguvu jimbo fulani CUF walikuwa wanawaachia; lakini), CUF lengo lake ilikuwa na vyama vyengine vipate nguvu; lakini hali haikuwa hivyo baada ya CHADEMA kupata nguvu imepata bipolar ddisorder (mania) ya kutaka kuonekana ndio chama kikuu cha upinzani, nafikiri ndio ilikuwa ndoto yao kubwa hio; sijui kama watakuwa na strategy nyengine za kuendelea mbele mazali wameshapata kua chama kikuu cha upinzani.
CHADEMA hawakupaswa kuvisaliti vyama vyengine hasa CUF; halafu wamegeuka CCM badala ya kusema wao kama ndio wamewatosa wenzao hawataki tena kuungana na vyama vya upinzani wamewatupia CUF kosa hilo la jinai.

Nawaombea wananchi wa taifa hili amani na demokrasia ya kweli na sio ukahaba wa kisiasa.
CUF ndo ilianza sarakasi kwanza iliungana na ccm na vyama vingine kuichafua CHADEMA kuwa wamemuua Chacha Wangwe, pili mahali ambapo hata mtoto mdogo anajua kuwa CUF haina nguvu wao waliomba waachiwe kugombea ubunge mbeya vijijini wakati wakijua kuwa Mbeya hamna CUF, kwahiyo wao ndo walianza kuionea wivu chadema.
 
Cuf wanaimalisha ndoa. Nawashauri saaana kama hawijui ccm watawadanganya halafu watashtukia chama kimekufa. Angalia maalim seif baada ya kuula amekisahau chama kabisa. Wakumbuke wanagawana madaraka kwa kuwa walishinda! Wakishindwa 2015 hawapati kitu. Ccm ni nyoka!
 
hapana mkuu,sina udini kabisa.Nilikuwa nachambua tu majina ya waliohudhuria

Unapozungumzia masuala ya dini hapo ndipo mnaponipa wasiwasi wafuasi wa CDM. Mnajidanganya kama nyie pekee yenu mnaweza mkataka mtu fulani akaingia ikulu. Bora CCM waendeleee kutunyonya hivi hivi mpaka tutie adabu
 
....Maalim Seif alishapata alichokuwa anapigania, sasa hivi umebaki mchezo wa kuigiza tu ndani ya CUF
 
Unapozungumzia masuala ya dini hapo ndipo mnaponipa wasiwasi wafuasi wa CDM. Mnajidanganya kama nyie pekee yenu mnaweza mkataka mtu fulani akaingia ikulu. Bora CCM waendeleee kutunyonya hivi hivi mpaka tutie adabu

ningeshangaa kama mfuasi wa cuf usingesema haya.Ndoa tamu bana!
 
Julius Mwenyewe naona hilo jina la kazi, ukimuangalia vizuri kwenye paji la uso ni kama vile huwa anaswali kwa kubong'oka.
" Wale wanaoswali kwa kubong'oka ndio wanomuogopa Mungu" ila wale wanaopiga magoti au kukaa kwenye mabenchi huku wakiburudishwa na mapambio ya warembo, wao wanamkejeli Mungu na hawamuogopi. Kwanza Mungu mwenyewe anafanana na wao !
 
musidanganyike na porojo za chadema. Chadema na CCM ni baba mmoja mama mmoja kwa kweli chadema ni backup ya ccm wote hawa wanatumikia kanisa siku kanisa litakapoona CCM haina maislahi tena na kanisa basi nchi hii atapewa Chadema.
 
Acha porojo. Waweza kuthibitisha?
 
" Wale wanaoswali kwa kubong'oka ndio wanomuogopa Mungu" ila wale wanaopiga magoti au kukaa kwenye mabenchi huku wakiburudishwa na mapambio ya warembo, wao wanamkejeli Mungu na hawamuogopi. Kwanza Mungu mwenyewe anafanana na wao !
Mbona hueleweki wewe?Mungu anafanana na wapi ktk hao uliowataja?Au Bange imeanza kufanya kazi nini?
 
Mbona hueleweki wewe?Mungu anafanana na wapi ktk hao uliowataja?Au Bange imeanza kufanya kazi nini?
Bange unazo wewe unaejifanya 'hamnazo' kwani hujui Mungu wenu 'nyie' ambao ham'bong'oki mnakaa kwenye mabenchi ya kuwa, ana macho, ana miguu, ana mikono, ana masikio, ana shikwa na njaa, ana shikwa usingizi na alikufa ! Yaani anafanana na ninyi kabisa !
 
Back
Top Bottom