kama yepi ?
kukubali vyama viwili kuunda umoja na kuviona vyengine kwa kua na uwakilishi mdogo si wapinzani ?
chadema mtulie muache makeke
ngoma yataka matao
Ni sawa wao si ni chama tawala wakishirikiana na CCM.ALIYEKUWA kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge lililopita, Hamad Rashid Mohamed amewashambulia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.
Hamad amewatuhumu Chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na Chama Cha Wananchi (CUF) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.
Mbunge huyo wa Wawi (CUF) alimewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, wao (CUF) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.
Amewataka viongozi wa Chadema wawe matured na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa Hamad, CUF wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo Chadema wajifunze kwao (CUF).
Alisema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na CUF kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge hilo.
Hamad amesema, alikataa wazo la Mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.
Mwanasiasa huyo amesema, CUF wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, Chadema hawataki.
Hamad amesema, viongozi wa Chadema wamemkwaza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.
Source: Basil Msongo,HabariLeo ,Dodoma; Tarehe: 18th November 2010
ALIYEKUWA kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge lililopita, Hamad Rashid Mohamed amewashambulia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.
Hamad amewatuhumu Chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na Chama Cha Wananchi (CUF) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.
Mbunge huyo wa Wawi (CUF) alimewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, wao (CUF) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.
Amewataka viongozi wa Chadema wawe matured na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa Hamad, CUF wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo Chadema wajifunze kwao (CUF).
Alisema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na CUF kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge hilo.
Hamad amesema, alikataa wazo la Mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.
Mwanasiasa huyo amesema, CUF wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, Chadema hawataki.
Hamad amesema, viongozi wa Chadema wamemkwaza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.
Source: Basil Msongo,HabariLeo ,Dodoma; Tarehe: 18th November 2010
Mkuu tukiangalia hivyo na tukienda down that road utaanza kuona kwamba wote wana makosa. Maana CUF wanaonekana ni Waislamu na Chadema Wakatoliki/Wachaga. Udini upo na ukabila upo sikatai. Hata katika hali ya kawaida mtu ukiwa na nafasi uka kutana na mtu wa kabila lako au dini yako una kuta ni rahisi zaidi kuwasaidia ila haimaanishi wewe ni mkabila au mdini.
Ila mkuu hamna haja ya mimi na wewe kubishana. Unaweza kuwa sahihi kusema udini umechangia nami nasema muafaka nao kwa kiasi kikubwa umechangia. Mbona wakati CUF ndiyo wameunda baraza kivuli bunge lililo pita wali washirikisha Chadema? Wakati huo udini haukuepo? Kwa mantiki hilo swala la kwanza linalo kuja kichwani mwangu ni kwamba it's not a matter of "udini" per se bali inferiority complex inayo izuia CUF kuwa chini ya Chadema kwenye baraza kivuli ndani ya Bunge.
na la mwisho ambalo hata na mm ningependa kujua kua Chadema imewakwaza viongozi wakuu wa NCCR na CUF kivipi ?
Nimecheka sana, Yaani sasa malengo ya CUF yanaanza kuwa crystal clear. Yaani CUF ndo wanawaonya Chadema kuwa kuna madhara ya kutomtambua rais aliyetangazwa na tume? CUF ambao wamemkataa karume kule Zanzibar hadi juzi juzi tu baada ya kurushiwa peremende? Sasa CUF wanaanza rasmi kuifanya kazi ya CCM ya kuishauri Chadema imtambue rais!!
Sasa iwe wazi, kwa wale wote waliokuwa wakiamini kuwa CUF inaweza ikawa mpinzani bara wakati Zanzibar wako serikalini, kuwa hilo halipo. Na anayesema CUF na Chadema wanaweza kuunda kambi ya upinzani haitakii mema kambi hiyo na pengine haoni haja ya kuwa na kambi ya upinzani. Na kusema kweli ni CCM pekee anayeweza kuona hilo la CUF kuungana na Chadema kwenye kambi ya upinzani ni jambo jema.
CUF walikuwa wanashirikishwa. Sasa huo usemaji wa vyama vingine CUF wamepewa lini? Yaani CUF wanaambiwa karibuni tuunde kambi ya upinzani, lakini wao wanasema ili sisi tuje inabidi na NCCR, UDP na TLP wawemo!! Si TLP, UDP wala NCCR waliokwishasema kuwa wanataka kuingia kwenye hiyo kambi. Sasa CUF wamepataje hiyo 'authority' ya kuvisemea hivyo vyama vingine??
CUF ni moja na CCM ni moja, kule Zanzibar na huku bara pia! Ni kujilisha upepo kuamini kuwa CUF na CCM sasa hivi watatofautiana kwa lolote, nasema ni kujilisha upepo. Sasa hivi wao, lao moja, nalo ni kuona kuwa ajenda za serikali zao zinapita bila kupigiwa kelele na yeyote.
aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni katika bunge lililopita, hamad rashid mohamed amewashambulia viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.
Hamad amewatuhumu chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na chama cha wananchi (cuf) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.
Mbunge huyo wa wawi (cuf) alimewaeleza waandishi wa habari mjini dodoma kuwa, wao (cuf) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.
Amewataka viongozi wa chadema wawe matured na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua rais jakaya kikwete.
Kwa mujibu wa hamad, cuf wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo chadema wajifunze kwao (cuf).
Alisema, mwenyekiti wa chadema, freeman mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na cuf kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika bunge hilo.
Hamad amesema, alikataa wazo la mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.
Mwanasiasa huyo amesema, cuf wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, chadema hawataki.
Hamad amesema, viongozi wa chadema wamemkwaza mwenyekiti wa nccr mageuzi, james mbatia na mwenyekiti wa cuf, profesa ibrahim lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.
Source: Basil msongo,habarileo ,dodoma; tarehe: 18th november 2010
Jamani kama CUF sio wabinafsi ilikuwaje wakafanya mwafaka bila kushirikisha wapinzani wengine?
Kwanini ni wao tu wanajiona wako sahihi kila siku, ile hali wao wamekubali kuungana na CCM zanzibar vyama vingine vikawapongeza ikiwemo chadema.
Kwanini leo wao wanataka kuipangia chadema chama cha kushirikiana nacho, Hii ni aibu kwa chadema.
Hicho hasa ndiyo chenyewe. CUF waeleze wazi kuwa siyo wapinzani tena. Watuambie wanampinga nani maana kule Zanzibar wameungana na CCM na pengine huu mwafaka unahusu Serikali ya Muungano.
Kama CUF si wabinafsi mbona zanzibar hawakushirikisha chama hata kimoja.
Mimi nafikiri tumeichagua Chadema kwa zaidi ya kura mil. 2 kwahiyo wanahaki ya kujipangia mambo yao kwa maslahi ya wananch na si kwa maslahi ya CUF kama ambavyo CUF inataka.
Kwanza CUF ni Chama cha Zanzibar kwahiyo huku bara hatuitambui hata kidogo, na Wabunge wengi wa CUF ni mamluki wanaotumwa na CCM hatuna imani nao.
Peoples Power