CUF: SMZ ya Karume ina Ukaburu

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
CUF: SMZ ya Karume ina Ukaburu
Mwandishi Wetu Aprili 30, 2008



KUNA madai ya kitakwimu, ambayo yanaonyesha kuwa kuna ubaguzi wa dhahiri dhidi ya Wazanzibari wenye asili ya Pemba, unaodaiwa kufanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ).

Takwimu zilizotolewa juzi Jumatatu na Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)katika Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Ismail Jussa Ladhu, zinaonyesha kuwa kuna upendeleo wa dhahiri kwa Wazanzibari wenye asili ya Unguja, huku Wapemba wakibaguliwa katika nafasi mbali mbali za uongozi na maendeleo.

“Tulipokuwa tukijadili agenda ya tatu ya mazungumzo iliyohusu Masuala ya Utawala wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tulionyesha pamoja na vielelezo vyenye ushahidi kamili, jinsi Serikali ya Awamu ya Sita ya Zanzibar, chini ya Amani Karume, inavyowabagua, kuwanyanyasa na kuwakandamiza wananchi wanaotoka kisiwa cha Pemba,” anasema Jussa, ambaye pia ni katibu wa timu ya Muafaka na Chama cha Mapinduzi (CCM) ya CUF katika mahojiano maalumu yaliyochapishwa katika kurasa za 12 na 13 za toleo hili.

Anasema anakumbuka hata walipowasilisha takwimu hizo kwenye mazungumzo ya muafaka na CCM, hata Mwenyekiti Mwenza wa Timu ya CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru, alielemewa na akawaambia wajumbe wenzake wa CCM kuwa “hivi kwa ushahidi huu, tunataka kubishana kitu gani hapa?“

“Sijui ni wangapi kati ya Watanzania wanaelewa kwamba kati ya mawaziri 15 wa Zanzibar, ni mmoja tu anayetoka Pemba. Kati ya naibu mawaziri sita, ni mmoja tu anayetoka Pemba, kati ya wawakilishi sita walioteuliwa na Rais, ni mmoja tu anayetoka Pemba. Kati ya makatibu wakuu 15, ni wawili tu wanaotoka Pemba. Kati ya manaibu makatibu wakuu 12, hakuna hata mmoja anayetoka Pemba.

“Kati ya wakurugenzi, mameneja wakuu na makamishna 102 waliopo, ni 17 tu wanaotoka Pemba. Kati ya Wakuu wa Vikosi vya SMZ, ambao ni watatu kwa kila kikosi cha Valantia, KMKM (Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo), JKU (Jeshi la Kujenga Uchumi), Mafunzo na Zimamoto, hakuna hata mmoja anayetoka Pemba.

“Na hata katika Jeshi la Polisi, kati ya maofisa wakuu 18 waliopo Zanzibar, ambao ni pamoja na Kamishna, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Mkuu wa Utawala kwa Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa 5 na Wakuu wa Polisi wa Wilaya 10, hakuna hata mmoja anayetokea Pemba.

“Kwa ujumla, utaona asilimia 83 ya viongozi na watendaji wa ngazi za juu serikalini wanatoka Unguja na ni asilimia 17 tu ndiyo wanaotoka Pemba.”

Jussa, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, anasema kwamba uendeshaji wa utawala wa SMZ kwa misingi ya ubaguzi pia unaonekana katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kwamba miradi kadhaa ya maendeleo imeonekana kukusanyika katika kisiwa cha Unguja na kukitenga kisiwa cha Pemba katika kiwango kinachoondoa kabisa uwiano wa maendeleo baina ya visiwa hivi katika sekta takriban zote.

“Matokeo ya hali hii, Pemba imekuwa iko nyuma sana kwa takriban kila sekta, jambo ambalo limechangia sana katika kuwalazimisha watu wa Pemba kuhama kisiwani huko na kukimbilia Unguja na maeneo mengine nje ya Zanzibar.

“Angalia, kwa mfano, ujenzi wa barabara. Hivi sasa Zanzibar kuna wakandarasi watano wanaojenga barabara nane zenye urefu wa kilometa 145. Miradi hiyo ya barabara inafadhiliwa na Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) pamoja na mchango wa SMZ. Katika ujenzi huo, hakuna hata kilometa mmoja ambayo inajengwa Pemba kwa muda huu,” anasema Jussa.

Kwa mujibu wa Jussa, katika miaka saba sasa ya utawala wa Amani Karume, barabara za Unguja zimetengewa na kutumia asilimia 83 ya fedha zote za bajeti, zilizopangwa kutumika katika ujenzi wa barabara na kwamba bajeti ya barabara za Pemba ni asilimia 17 iliyobaki.

Kwamba, fedha hizo za Pemba ni asilimia iliyotengwa tu na si kiwango halisi kilichotumika kutengeneza barabara za huko na kuwa mgao huo usio na uwiano umeiweka Pemba hadi hivi sasa kuwa na mahitaji ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 320, wakati mahitaji ya Kisiwa cha Unguja ni kilometa 87 tu.

“Chukua mfano pia wa ujenzi wa viwanja vya ndege. Utaona kiasi cha sh. bilioni 12 zimetengwa na kutumiwa kwa matengenezo ya Uwanja wa Ndege wa Unguja. Hakuna kiwango kilichotengwa wala kutumika kwa kazi kama hizo katika Kiwanja cha Ndege cha Karume, Pemba.

“Hali katika matengenezo ya bandari ni hivyo hivyo. Jumla ya sh. bilioni 67 zimetengwa na kutumika katika kazi mbali mbali za matengenezo ya Bandari ya Malindi, Unguja. Pemba imetengewa sh. milioni 590 sawa na asilimia 0.88 ya kiasi kilichotengwa na kutumika kwa ajili ya Unguja. Nyingi kati ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya Pemba bado hazijatolewa hadi leo,“ anasema.

Jussa anasema kwamba kuna Mradi wa Maji Mijini, ambao unafadhiliwa na Serikali ya Japan, na kwamba awali katika upangaji na uandishi (project write-up) wa mradi huo, miji yote ya Unguja na Pemba (Zanzibar Mjini, Wete, Chake na Mkoani) ilijumuishwa.

Kwamba miradi ya maji iliyofadhiliwa na Shirika la Misaada la Finland (FINIDA) wakati wa kuanzishwa kwa mpango huu miaka ya 80 ilizingatia hilo, lakini awamu ya sasa ya Mradi wa Maji Mijini chini ya Utawala wa Rais Amani Karume, ambayo inafadhiliwa na Japan kupitia Shirika la Misaada la Japan (JICA), imeifuta miji yote ya Pemba katika maombi ya mradi.

“Athari ya kutopelekwa miradi kisiwani Pemba imechangia sana kuongeza umasikini Pemba. Sote tunaelewa kuwa kuwepo kwa miradi ya maendeleo katika eneo inakoelekezwa humaanisha pia kupatikana kwa ajira rasmi na zisizo rasmi kwa wananchi na wakazi wa eneo hilo na hivyo kusaidia pia kupunguza umasikini.

“Hivyo basi, kukosekana kwa miradi ya maendeleo kisiwani Pemba kunamaanisha kuongezeka kwa umasikini na hivyo kuamsha matokeo kadhaa yanayoletwa na umasikini.

“Katika hali hiyo, hivi mtu atashangaa akisikia wenye utawala Unguja wanawaagiza wananchi wenye asili ya Pemba wahame kisiwani Unguja. Hizo ndizo sera za CCM na ndiyo maana Wazanzibari waliochoka kubaguliwa na kugawiwa wanaikataa CCM kila uchao.

Jussa alikuwa akizungumzia takwimu hizo zinazoashiria ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Kisiwa cha Pemba, wakati alipoulizwa kuhusu ukweli wa taarifa kwamba hivi karibuni kulisambazwa vikaratasi mjini Unguja, vilivyokuwa na vitisho dhidi ya Wapemba, kwamba waondoke la sivyo watapata matatizo.

Kwa mujibu wa Jussa, Naibu Mkurugenzi wa CUF wa masuala ya haki za binadamu na mahusiano ya umma, Salim Bimani, aliwasilisha taarifa za vikaratasi hivyo kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Bakari Khatib Shaaban, ambaye aliahidi kufanya uchunguzi, na kwamba chama hicho kinasubiri taarifa za uchunguzi huo.

“Tathmini ya vitisho hivyo inaendelea kufanywa. Lakini wahenga wamesema usiangalie ulipoangukia, angalia ulipojikwaa. Hatua ya vitisho hivi ni mwendelezo tu wa sera za CCM za kuwabagua, kuwanyanyasa na kuwakandamiza ndugu zetu wanaotoka Kisiwa cha Pemba,” anasema.

Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed, aliongoza wabunge wenzake katika kufanya tathmini ya vitisho hivyo, na kwamba anakusudia kuwasilisha ripoti katika Bunge.



raia mwema


sasa wabaguzi ni nani? wao waliojibagua na kuikataa SMZ au wale waliokaa kimya kwa kukataliwa na wenzao.


inakuwaje CUF kujibagua kwa makusudi na serikali ya SMZ na hata wakipelekea maendeleo hufanya kila njia kufanya surbotage ili ionekane SMZ inawabagua?


jee tumchague waziri nani wakati wawakilishi wa pemba wote ni CUF?
 
CUF: SMZ ya Karume ina Ukaburu
Msaidizi Maalum wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)katika Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Ismail Jussa Ladhu, zinaonyesha kuwa kuna upendeleo wa dhahiri kwa Wazanzibari wenye asili ya Unguja, huku Wapemba wakibaguliwa katika nafasi mbali mbali za uongozi na maendeleo.

Bwana Jussa inafaa aelewe kuwa -Mtu huvuna akipandacho-. Kama ni ubaguzi unaofikia daraja ya ukaburu, basi ulianzishwa na CUF tokea pale ilipoanzishwa KAMAHURU baada ya Seif Sharif Hamad na Genge lake kufukuzwa CCM na katika Serikali ya Alhaj Idriss Abdulwakil. Napenda kukujuilisha kwamba rekodi na kumbukumbu zote zinathibitisha kuwa hapo kundi hilo ndipo lilipoaanza kushikilia bango la Upemba na Uunguja, hata likasababisha tukimbiwe na maswahiba zetu (sabuni ya roho) wenye damu ya Kipemba. Jee hivi sasa kweli wanahisi Enough is enough?
 
“Sijui ni wangapi kati ya Watanzania wanaelewa kwamba kati ya mawaziri 15 wa Zanzibar, ni mmoja tu anayetoka Pemba. Kati ya naibu mawaziri sita, ni mmoja tu anayetoka Pemba, kati ya wawakilishi sita walioteuliwa na Rais, ni mmoja tu anayetoka Pemba. Kati ya makatibu wakuu 15, ni wawili tu wanaotoka Pemba. Kati ya manaibu makatibu wakuu 12, hakuna hata mmoja anayetoka Pemba.
Jussa, suala la uteuzi wa mawaziri ufanyika kutokana na kuwa ni mwakilishi wa jimbo fulani. Iwapo CCM haina mwakilishi yoyote toka Pemba unategemea nini hapo?
 
Wanamalizana wao kwa wao!!!!
Naombeni kujua na wakristo idadi yake ni ngapi ktk hiyo serikali?
Hongereni wa-WATANGANYIKA ubaguzi ya kidini mmeyashinda kwa kasi kidogo dogo.
 
Wanamalizana wao kwa wao!!!!
Naombeni kujua na wakristo idadi yake ni ngapi ktk hiyo serikali?
Hongereni wa-WATANGANYIKA ubaguzi ya kidini mmeyashinda kwa kasi kidogo dogo.
Ah wewe namna gani? Hawamalizani hao wanatafuta mkakati wakikaa sawa suala jengine litakuwa Katika hiyo Serikali yenu Wazanzibar wako wangapi,na kwa nini hakuna uwiano unaomaanisha Muungano?
 
Kwanini Pemba isihamishiwe na kuwa Mkoa wa Tanzania bara....?

ungeyajua maneno usingetamka.

Pemba hawako tayari kabisa kuwa na bara, wao wanaamini bila ya kusita matatizo yao ni huko bora hata Unguja ukiwaambia hivyo alau watakusikia
 
Back
Top Bottom