Kwa watu wanaofuatilia siasa za Tz kuna wakati CUF walikuwa wanatumia falsafa ya ngangari na kujifanya wanatetea watu. Kuna watu nchi hii wameteswa na kupata tabu kwa ajili ya CUF. CUF walikuwa wanadai serikali ya Tanganyika na katiba mpya na haki sawa kwa wote. Kupewa cheo huko Znz kisicho na meno ndio kumewabadilisha hivi? Sasa kumbe walikuwa wanapigania vyeo na vihela vidogo? Ukweli kwa vile wamejifunga na CCM watazikwa pamoja. Wananchi wengi waliokuwa CUF sasa wamejua ni chama cha aina gani?
Haki hailetwi kwa kushirikiana na CCM. Haki inaletwa na katiba inayotokana na wananchi. CUF wangetumia nafasi hii kuweka mambo sawa maana muungano na ccm si wa kudumu ila katiba ni ya kudumu. Hivi CUF hawajui kuwa mkakati Znz ni kuhakikisha CUF haitakaa ishinde urais?