Interested Observer
Platinum Member
- Mar 27, 2006
- 4,932
- 7,764
Mwiba,Niliwahi kusema hili la mke kuwa CCM au mume kuwa CUF au vinginevyo,hii inamaana wote wawili hawafai ,mke na mumewe watafute biashara wafanye ,haiwezekani haiwezekani ,maana hata kuelekea haielekei isipokuwa mnailazimisha tu ,na hili sio kwa walio nje ya Chadema hata wale waliokuwa ndani ya Chadema wanaliona ni jambo la ajabu kabisa ,ikiwa mke au mume ameshindwa kumshawishi mwenziwe kwa sera za Chama chake itawezekanaje kuwashawishi wengine ,ni lazima hapo pana walakin.
DR Slaa jitahidi sana kumshawishi mama watoto ajiunge na Chadema ,maana kama nikipiga picha unapata Raisi ni Chadema na First lady ni CCM ,yaani mmoja ataendeleza sera za mafisadiCCM na mwengine za Chadema.
Nimeshauriwa nisome yanayosemwa juu yangu na Profesa Lipumba na wenzake katika kundi la wana-CUF jinsi inavyoripotiwa ktk Jamii Forums; kwa hiyo nikafungua p.c. yangu na kuingia tena ktk JF baada ya karibu mwaka mmoja.
Nimesoma matamshi ya Lipumba na maelezo kwamba wana-CUF walionizushia ufisadi ni wasaidizi wake; na ametajwa bwana mmoja anayeitwa Marahagande. Naandika maelezo haya nikitumaini kuwa kuna mwanaJF atayemjulisha Lipumba na huyo Marahagande nisemayo ili wayasome.
Niliteuliwa Governor-Designate na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 1965 baada ya uamuzi wa kuvunja East African Currency Board na kuwa na Central Bank yetu wenyewe pamoja na sarafu yetu ya kitaifa. Mwalimu alijua uadilifu wangu na jinsi nilivyokuwa mchapakazi. Desemba 1965 Sheria ya Bank of Tanzania ilipitishwa na Bunge na iliposainiwa Januari,1966 ndipo nilikuwa Governor wa Benki Kuu rasmi. Mwezi wa Juni, 1966 tulizindua rasmi sarafu yetu ya kitaifa na operations za Bank of Tanzania.
Niliendesha Benki Kuu kama Governor mpaka Aprili, 1974 nilipoteuliwa Katibu Mkuu wa East African Community. Charles Nyirabu ambaye alikuwa Deputy Governor alichukuwa nafasi yangu. Bob Makani ambaye nilimwajiri hapo awali kama Exchange Control Manager lakini akaondoka Benki Kuu kwenda kuwa Deputy Attorney General, alirudishwa Benki Kuu na kuwa Deputy Governor kwa Nyirabu.
Jengo la BoT original lilijengwa kati ya mwaka 1966 na 1969 wakati huo nikiwa na deputy governor ambaye alikuwa expartriate. Nyirabu ama Makani hawakuhusika. Hawakuwepo.
Inavyofahamika, East African Community ilivunjika 1977 na mimi niliacha Ukatibu Mkuu nikaenda Dar es Salaam, nilipoteuliwa Waziri wa Fedha na Mipango. Wadhifa huo niliushikilia wakati wa vita dhidi Nduli Amin wa Uganda. Vita ilipokwisha, uchumi ulikuwa ktk hali ngumu. Hali hii ngumu ilichangiwa pia na sera za nchi. Majadiliano ya jinsi ya kuimarisha hali ya uchumi na fedha, baina yangu na bosi wangu, yalipelekea mimi kujiuzulu pale nilipoona bosi alikataa kata kata ushauri niodhani ni muhimu. Hiyo ilikuwa Desemba 1979.
Nimekuwa mkulima kuanzia wakati huo, licha ya kwamba kati ya Novemba 1982 na Novemba 1986 niliteuliwa Executive Director wa IMF huko Washington D.C. kuwakilisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika zinazoongea Kiingereza. Kwa hiyo wakati Jengo la BoT likiungua moto mwaka wa 1984, sikuwa naishi Tanzania na ilikuwa ni miaka 10 tangu niache majukumu ya kuendesha Benki Kuu. Nakumbuka rafiki yangu aliyekuwa Dar es Salaam siku hiyo alinipigia simu huko Washington akinieleza "jengo lako la BoT linaungua moto".
Niliporejea nyumbani Novemba, 1986 nimeendelea na usimamizi wa shamba langu la kahawa mpaka leo. Mwaka 1992, Katiba iliporuhusu vyama vingi vya siasa nilijikuta nashirikiana na WaTz kadhaa kuanzisha CHADEMA, na kwa muda wa miaka sita hadi1998 nilikiongoza kama Mwenyekiti (Taifa). Bob Makani tuofahamiana tangu nilipomteuwa Exchange Control Manager, BoT. alijiunga na Chadema, akawa Katibu Mkuu wake wa kwanza. Nilipoachia kiti alichaguliwa kunirithi kama Mwenyekiti (Taifa) 1998.
Sasa hawa CUF na Profesa Lipumba wamepata wapi hii hadithi ya Edwin Mtei kuhusika na kuchoma moto Benki Kuu? Lipumba lazima akumbuke ni lini hilo jengo liliungua moto. Kama Marahangande anasema mambo yasiyoweza kuingia akilini, Lipumba ana jukumu la kumkanya au kumfafanulia ukweli.
Nimesoma posts kadhaa juu ya miropoko hii ya Lipumba na wasaidizi wake. Namheshimu sana Profesa kama economist mwandamizi hapa nchini; lakini kama ameshindwa kuona huu upotoshaji wa hali halisi kutokana na ari ya kukisakama CHADEMA, basi amekwisha. Na kama kweli kuna mkono wa mbali unaosukuma kutoshirikiana kwa CUF na CHADEMA, Lipumba anatakiwa atambue haraka, la sivyo hafai kama Mwana Mageuzi.
Namalizia kwa kuwasihi waniombe radhi hadharani kwa hii kashfa, la sivyo nikilazimika kuchukua hatua za kisheria, watakuwa de-railed as wana-Mageuzi.
Edwin Mtei

Mzee Mtei,
Shikamoo. Ni furaha iliyoje kukuona hapa Jamii Forums. Tena umeingia kwa jina lako mwenyewe. Mimi ni mwanao ingawa hapa naitwa Jasusi.
Ndio hivyo tukishaanza kupeana shikamoo na kuitana muheshimiwa ,tutashindwa hata kuhoji. Ila Chadema sidhani kama kuna viongozi waadilifu ni watu ambao pindipo wakiukwaa uongozi wa Nchi hii basi watatembea na bastola kiunoni kama Fideli Castro. Hivi sasa wameanza na makoti. WaTz lazima mfikirie sana .Watu wote hapa JF wangeingia na majina yao, nadhani SHIKAMOO zingekuwa kibao.
Ni kweli kabisa huo ni umbea wa mtu yeyote mwenye kiwango kidogo cha uchambuzi hivi RA ni na nani hata awe na nguvu ya kufanya lolote hivi kwa maoni yake kila mtu ni mroho wa pesa kama anvyofikiriTupe ushahidi wa hayo unayosema...kabla hatujaita ni umbea
Nikujibu kama Sumari alivyomjibu Slaa kuhusu meremeta -Mwiba tafuta hoja sio kila kitu lazima uandike ubaya wa chadema; talk about the ruling party; sijaona hata vyama vya kijamii vikipinga chama cha upinzani ambacho hakina dola; CUF mnaweza kuandika historia kwa hili maana inawezekana ikawa ndio mara ya kwanza ktk africa. vyama lengo lake ni kuchukua dola; sasa dola yenu iko chadema???Ndio hivyo tukishaanza kupeana shikamoo na kuitana muheshimiwa ,tutashindwa hata kuhoji. Ila Chadema sidhani kama kuna viongozi waadilifu ni watu ambao pindipo wakiukwaa uongozi wa Nchi hii basi watatembea na bastola kiunoni kama Fideli Castro. Hivi sasa wameanza na makoti. WaTz lazima mfikirie sana .
Nimeingia tena leo ktk Jamii Forums ili nione reactions juu ya maelezo yangu ya jana.
Kwanza nikiri kwamba ni Mheshimiwa Willibrod Slaa alinishauri nisome hii miropoko ya Lipumba na wana-CUF wenzake.
Pili, nawashukuru wana-JF walio-react positively kwa niliyoeleza. Nilimalizia kwa kusema kwamba Lipumba na wenzake waniombe radhi hadharani, laa sivyo nikilazimika kuchukua hatua za kisheria, juhudi zao za kuleta Mageuzi zitakuwa derailed. On further thought, I am now of the view that the professor and the likes of Maharagande are already no longer in the group of Wana-Mageuzi. Wanastahili kupumzishwa.
Tatu, I want to repeat that I ceased to be Governor of the Bank of Tanzania in April, 1974, more than 35 years ago and handed over to Charles Nyirabu ambaye ni marehemu sasa. Having regard to the time lapse, are those wana-JF implying that I might have stollen money from the BoT, serious great thinkers? There were external auditors at the end of every financial year of the BoT, during those days, and I believe they continued to give clean reports until recently, when President Kikwete was obliged to appoint Ernest & Young who unearthed the EPA scandal. Daudi Ballali, the Governor associated with the scum was the fifth governor.
Nne, I have never claimed that I studied Economics at the Makerere University College. I specialized in Political Science and History and won the Shell Company Prize for the best student of the Faculty for the year 1957. I should also add that I never applied for the financial and economic posts I have been privileged to occupy in this country or abroad. They were given to me on the basis my performance in junior or related functions.
Someone has stated that I failed in running the BoT. I do not know how he has rated that performance and what successor governor he has compared me with. The English have a saying: "The proof of taste of the pudding is in the eating". And I would add: "Not in the recipe or the cook"!
Incidentally, some JF member attributes the problems currently confronting coffee farmers to failure of TaCRI, which I led as Board Chairman from 2001 to 2008. Coffee problems are basically international in the sense that overproduction has made its market a buyers' market. Other local problems are associated with inadequate inputs, taxation and farmers' education. The TaCRI has developed disease resistant varieties of high cup quality and yields which even the President recently praised. I am proud that it was during my chairmanship of the policy board that these scientists made the break through.
I want to end this reply, which regrettably diverts JF members from more important and relevant issues, by pointing out that even during my governorship of the BoT. the Governor of the Bank of England, where economists abound, was Lord O'Brien who was not an economist, but had only been the Chief Cashier of that Bank. Lastly, I never underated economists in my work, but used them fully. I also attended so many courses and seminars on financial and economic management that I almost became a professional attender.
Edwin Mtei
Sina Hakika Juu ya Kauli ya UFISADI wa Chadema Kaizungumza nani ktk CUF. I hope sio Lipumba. Kama Maharagande basi tumuonee Huruma na Matumaini yangu Prof.Lipumba anaweza kumuweka chini na pia Kuwaomba Radhi akina Hao Viongozi walotajwa.
Sijui Kwanini CUF au Chadema Kila mmoja anampiga vita Mwezie wakati wote hawana Serikali....Sijui Nani Kaanza na Mwezie anamaliza!!! Nionavyo CCM ndio wameplay a big role..either Ikiwa CCM as a think tank yao au Wafanyabiashara Wenye "Interest ktk SIASA" ambao wanapenda kumuona alie Madarakani ni Mshikaji wao au mwenye ushawishi Kwake...!!
Mafisadi either Mapapa au Nyangumi Kila mmoja hapendi kuitwa Hivyo...Kama wanaona kuna oppurtunity ya kuwatumia Wanasiasa ili kuzima au kuwamulika wa Upande mwingine kwake yeye ni "Mukidy"="POA"..
Atlast Wananchi Hawajui wanapelekwa wapi...na Atlast CCM ndio kitaibuka Kidedea!!!
Kanda2,Hapa mjadala ni wa kiswahili sisi wengine hatujui kizungu,kwanini uandike kizungu AU kiswahili kinakupa tabu?
uchumi wa Tanzania uliharibika kwa kitendo cha Mwalimu Nyerere kuwatumia wanasiasa kwenye sekta nyeti za kiuchumi.
kutokana na wewe kutokuwa na ujuzi ua maarifa ya uchumi ndio chanzo cha BOT na uchumi wetu kuyumba.
hata kama ulipata zawadi ya HISTORIA hutokuwa mchumi.lazima ukiri ufahamu wako mdogo kwenye uchumi uliyumbusha BOT.
kanda2,Hapa mjadala ni wa kiswahili sisi wengine hatujui kizungu,kwanini uandike kizungu AU kiswahili kinakupa tabu?
uchumi wa Tanzania uliharibika kwa kitendo cha Mwalimu Nyerere kuwatumia wanasiasa kwenye sekta nyeti za kiuchumi.
kutokana na wewe kutokuwa na ujuzi ua maarifa ya uchumi ndio chanzo cha BOT na uchumi wetu kuyumba.
hata kama ulipata zawadi ya HISTORIA hutokuwa mchumi.lazima ukiri ufahamu wako mdogo kwenye uchumi uliyumbisha BOT.ajira za kindugu na kikabila zilishaamiri kipindi cha MTEI mfano alimuajiri mkwe wake ambaye ni Freeman Mbowe BOT huku akijua kuwa MBOWE hana elimu ya kuajiriwa BOT.
Mtei njoo unijibu hizo hoja.
Kanda2,
You are brain is ruled by religious hate, I went through most of the messages you have posted, I am seeing that you have that "virus" which is going "away" with your organ! You either cut the organ or die with it; because a virus goes with an organ.
We all know this innocent old fellow; but just to show the reference; if you can remember, the WORST Finance Minister went by the name of Kighoma Ali Malima, who died in London in the 1990s. So please do not disturb this old fellow!!