CUF Mtaliwa wote, tafuteni suluhu! Shauri yenu!

CUF Mtaliwa wote, tafuteni suluhu! Shauri yenu!

Ushauri mzuri.

Kwa upande wangu nashauri Maalim Seif ahamie chadema pamoja na wabunge wake , na chadema wamuachie Maalim seif chadema upande wa visiwani ambapo ataweka wagombea wake anaowataka yaani aliotoka nao cuf.Hii itazididha uimara wa chadema na upinzani kwa ujumla.

Hasara yake Cuf itakufa.Lakini hata Maalim asipohama bado cuf itakufa tu maana sioni Lipumba akilegeza kamba wakati huo Maalim kabanwa
Mkuu, una maono ya mbali sana.
 
Kuna wakati unatakiwa kuufahamu ukweli. Muda sio mrefu Lipumba anamtimua Maalimu, sijui hao wanaoshindwa kuangalia umuhimu wa maridhiano na maelewano. Lipumba amemkaribisha Maalim mezani, lakini kuna watu hawataki, hivi hawaoni wanaelekea kuzimu?
Maalim analipwa hapahapa duniani kwa mambo aliyokuwa anawafanyia wazanzibar kwa kuwacheza shere.Malipo haya ndio saizi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia hairuhisu watu wanaogombana kutafuta suluhu au kusuluhishwa?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
Pale hakuna suluuu hata maalimu akiamuakujishusha yataibuka mengine mengi sana bora wavutane hivi hivi ila ipo cku haki itakaa upande wake japo itachukua muda. Tena maalimu akilidhia kumtambua jamaa ndo hatari zaidi maana sasa atashughulikia kwa mujib wa sheria tena usiombe
 
Huu mpango ulitengenezwa kuja kuvuruga upinzani na sasa umeanz kazi nimeota hizi chokochoko zilianzia lumumba pale na kupewa baraka zoote n mkulu hii ndoto yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CUF acheni kutunishiana misuli, wenye hekima tushaona mnavyoenda mnaenda kubaya wote na sasa tunaona ipo haja ya kuwashauri kwa hekma ili muweze kunusurika.

Kimsingi kwa mtu yeyote ambaye ni mdau wa demokrasia, hawezi kufurahia kuona migogoro ndani ya vyama vya siasa ambayo inatishia kuviua vyama hivyo. Kwa mantiki hiyo, umefika muda sasa wa wadau wa demokrasia kuwasaidia CUF kupata suluhu ya mgogoro unaowakabili. Aidha, kwa kuwa CUF ni chama cha upinzani, vyama vingine vya upinzani vina jukumu la kuwasaidia CUF kufikia Suluhu kuliko mtu mwingine yeyote.

HATARI ILIYOPO KAMA MGOGORO HUU UTAENDELEA KAMA ULIVYO;
Ikiwa, mgogoro huu utaendelea kama ulivyo bila kusuluhishwa kwa njia za kidiplomasia, madhara ya fuatayo yanatarajiwa kujitokeza.
1. Kuzidi kwa chuki miongoni mwa wana CUF wenyewe kwa wenyewe hasa chuki kati ya wana CUF wa zanzbar/ pemba dhidi ya wale wa Bara.

2. Kuzidi kwa chuki ambayo haiwezi kuwa na faidia kwa yoyote kati ya Prof. Lipumba na Maalim.
3. Kwa upande mmoja CUF ya maalim Seif itakufa kwa kukosa uungwaji mkono wa kitaasisi na kisheria (kutokana na position ya mgogoro kwa sasa) na kwa upande mwingine CUF ya Lipumba itakufa vile vile kwa kukosa uungwaji mkono wa kutosha Zanzibar lakini pia kwa kukosa "Cause and Purpose" bara. CUF itapoteza wabunge wengi toka pande zote. Kwa hiyo wakiendelea hivi matokea yanatarajiwa kuwa "Zero sum game" kwa pande zote.

NINI CHA KUFANYA;
Kwa kuanzia,
1.Tunaziomba pande zote (Maalim na Prof. Lipumba) kwanza waache kutoleana kauli kali na za kuudhi ambazo zitaendelea kuleta uhasama.

2. Maalim aitishe vyombo vya habari akiwa pemba na kueleza wafuasi wake kuwa yuko tayari kufikia maridhiano na prof. Lipumba na Lipumba aitishe Press Dar akieleza utayari wake wa kufikia maridhiano na Maalim.

3. ACT (kwa sababu wanaweza kuaminika na pande zote), wawasaidie CUF kuwatafutia msuluhishi ambaye anaaminika na pande zote ambaye kwa haraka sana ataita wajumbe wa pande zote na kuanza hatua za maridhiano, kwa kuangalia uwezekano wa Lipumba kuendelea kuwa Mwenyekiti na Maalim kuwa Katibu kama ilivyokuwa awali.

MSULUHISHI
Napendekeza Msuluhishi awe ni Shekhe, Maalim Ally Basalleh wa dar es salaam. Hii ni kwa sababu kwa sasa kitu pekee kinachowaunganisha Lipumba na Seif ni dini, wote wanamfahamu vizuri Basalleh na wamekuwa wakiswali nyuma yake mara kwa mara. Aidha Shekhe basalleh ni msomi, mtu mzima, muelewa na mwenye busara kubwa sana.Naamini suluhu itafikiwa.

Nawatakieni suluhu njema.
Never ever!!!!! Kukaa meza moja na yule msaliti?.Maalim kuanza upya sio ujinga,go your way achana na huyo pandikizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri.

Kwa upande wangu nashauri Maalim Seif ahamie chadema pamoja na wabunge wake , na chadema wamuachie Maalim seif chadema upande wa visiwani ambapo ataweka wagombea wake anaowataka yaani aliotoka nao cuf.Hii itazididha uimara wa chadema na upinzani kwa ujumla.

Hasara yake Cuf itakufa.Lakini hata Maalim asipohama bado cuf itakufa tu maana sioni Lipumba akilegeza kamba wakati huo Maalim kabanwa

Maalim HAJABANWA
Mahakama itabariko bariki ya Lipumba kujiuzuru 2015 kama ilikua halali!
Hawa wabunge 8 wakienda Mahakamani kesho watalinda Ubunge wao
Kesi zipo Mahakamani tusubiri maamuzi yake
 
~~~>>>>Mgogoro wa CUF utafika tamati mara baada ya Lipumba ama Seifu ama wote kwa pamoja kuaga dunia.
 
Kama CUF kweli ni chama cha wananchi, basi wananchi mlio wanachama wa CUF inabidi mdhihirishe nguvu yenu! Wapigeni chini Maalim na Lipumba mfungue ukurasa mpya.

Vinginevyo, nitaendelea kuamini kuwa CUF ni mali binafsi ya partners wachache ambao kwa sasa wamefarakana! Neither Maalim nor Lipumba is wise enough to put your party's interests before his own!
 
Hii CUF ilikuwa imeshakuwa kampuni ya Seif Maalim.
Watanzania tunataka chama kimoja kikubwa cha upinzani dhidi ya CCM ni muhimu seif akakaa na Chadema kuweka mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Watanzania hatutaki vyama kufanya ndoa ya mkeka wa vyama kama mwaka 2015.
 
Kiukweli hali ya CUF ni mbaya sana..

Mpaka Prof Lipumba ameamua kufukuza wabunge 8 wa Maalim maana yake hiki CUF hivi sasa kipo shimoni...

Sasa Ndugai akiingia tu kwenye mtego wa kuwafukuza ( likely to be),CUF ndio basi tena.
Ndio basi vipii. Si Lipumba atateua wake..
 
Hii CUF ilikuwa imeshakuwa kampuni ya Seif Maalim.
Watanzania tunataka chama kimoja kikubwa cha upinzani dhidi ya CCM ni muhimu seif akakaa na Chadema kuweka mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Watanzania hatutaki vyama kufanya ndoa ya mkeka wa vyama kama mwaka 2015.
Unasema chama cha kiliberali kikae na chama cha ccm b.. duh..hiyo combination sijui itakuwaje
 
Moja ya kitu kinachoweza ifanya CUF iendelee kuwa hai ni JFK kwa wahusika wa hawa watu
 
Back
Top Bottom