CUF Mtaliwa wote, tafuteni suluhu! Shauri yenu!

CUF Mtaliwa wote, tafuteni suluhu! Shauri yenu!

Unatafuta suluhu na wahuni waliojizulu kisha kufukuzwa chamani? Kwanini ukae meza moja na msaliti aliyeamua kukimbia chama wakati ambao alikuwa anahitajika na chama kuliko wakati wowote ule? siku chache kabla ya uchaguzi? Kwanini ang'ang'anie CUF badala ya kuanzisha chama chake?

Mtume alikaa mezani na makafiri waliopigana naye vita sembuse waliotofautiana mitizamo sababu ya siasa ndio eashindwa kukaa mezani?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
CCM inaweza kuwa inafaidika sana kisiasa kwa kumtumia Lipumba kuivuruga CUF ila kuna chuki kubwa inajengeka kati ya wazanzibar na wabara kati ya wananchi na serikali.
Dhambi ya dhuluma hii inajenga chuki mbaya sana kwa taifa zima.
Wala katika hili musiisingizie ccm.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
hivi wale waandishi waliopigwa na wafuasi wa lipumba, imeishaje ile issue na ule mzozo wa sakaya na kambaya mpaka sakaya akasema ulipewa m25 ukampe msajili wa vyama ukapeleka 20, ile ilikuwa ni takrima,

nitakuunga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
 
Ushauri mzuri.

Kwa upande wangu nashauri Maalim Seif ahamie chadema pamoja na wabunge wake , na chadema wamuachie Maalim seif chadema upande wa visiwani ambapo ataweka wagombea wake anaowataka yaani aliotoka nao cuf.Hii itazididha uimara wa chadema na upinzani kwa ujumla.

Hasara yake Cuf itakufa.Lakini hata Maalim asipohama bado cuf itakufa tu maana sioni Lipumba akilegeza kamba wakati huo Maalim kabanwa
Hiki CHADEMA ndicho mlichokuwa mnatafuta....hongereni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu, kama CUF wasipotafuta suluhu, inakufa safari hii, si bara si visiwani tutabakia kuisoma kwenye vitabu vya historia. Kwa sasa ishu ni kuinusuru CUF isife na wala sio kushinda uchaguzi 2020. Upinzani kwa ssa wako very disorganized hawawezi kushinda 2020. Unasema waungane wawe kitu kimoja, shida kila chama kina power mongers tena ambao ni myopic! kama kungekuwa na visionary leaders humo tungewaona wakipambana kusuluhisha mgogoro wa CUF. kama ni vyama vya upinzani kuungana, wangeshaungana toka kitambo, kwa kuwa sababu za kuungana zilikuwepo toka kitambo
Jamani tusiwalaumu upinzani juu ya kutengeneza muungano. Sheria za tz haziruhusu muungano wa vyama sasa cjui tunataka waungane vp? Kinyume cha sheria ili tuwacheke tena
 
Msisahau machafuko ya Zanzibar 2001

Maana naona mnaongelea kufa chama tu, watu walichinjana kama kuku pale visiwani
 
Wala katika hili musiisingizie ccm.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
Ndugu yangu tangu Lipumba anavamiwa ofisi za CUF na kuvunja milango ni polisi wa CCM walimpa ulinzi na kuhakikisha anaingia ofisini.Aidha Msajili wa vyama, RITA na Spika wote wote hawana tofaoti na polisi waliosimamia uvunjaji wa milango ya ofisi za CUF buguruni.
God bless our country.
 
Kwanza haya kamwambie dikteta uchwara ambaye ndiyo chanzo cha yote haya kisha umuulize lini atakutana na Viongozi na Wabunge wa Chadema na CUF halali? Maana ni karibu miaka 12 sasa hajawahi kukutana na hata mmoja zaidi ya kuwatusi tu kama juzi kawaita vilaza.
Kwa hiyo hayo ndio yanayosababisha pasiwe na haja ya cuf kutafuta suluhu?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Jamani tusiwalaumu upinzani juu ya kutengeneza muungano. Sheria za tz haziruhusu muungano wa vyama sasa cjui tunataka waungane vp? Kinyume cha sheria ili tuwacheke tena
Pia hairuhisu watu wanaogombana kutafuta suluhu au kusuluhishwa?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Ndugu yangu tangu Lipumba anavamiwa ofisi za CUF na kuvunja milango ni polisi wa CCM walimpa ulinzi na kuhakikisha anaingia ofisini.Aidha Msajili wa vyama, RITA na Spika wote wote hawana tofaoti na polisi waliosimamia uvunjaji wa milango ya ofisi za CUF buguruni.
God bless our country.
Kwa hiyo unaunga mkono suluhu au?

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Huko tuendako Maalim Seifu akiona Maji yanataka kuzidi unga atahamia CHADEMA na kumuacha Profesa Lipumba na CUF yake. Maalifu Seif ndani ya CHADEMA ata-gain momentum lakini Profesa Lipumba ata-loose.

Huo ndio utakuwa mwisho wa CUF.

MUDA NI HAKIMU MZURI.
 
Ushauri mzuri.

Kwa upande wangu nashauri Maalim Seif ahamie chadema pamoja na wabunge wake , na chadema wamuachie Maalim seif chadema upande wa visiwani ambapo ataweka wagombea wake anaowataka yaani aliotoka nao cuf.Hii itazididha uimara wa chadema na upinzani kwa ujumla.

Hasara yake Cuf itakufa.Lakini hata Maalim asipohama bado cuf itakufa tu maana sioni Lipumba akilegeza kamba wakati huo Maalim kabanwa
Siasa ya pemba sio ya kusema maalim seif ahamie chadema na wafuasi wa cuf watamfuata, haiko hivyo siasa yao! Ni watazira kuliko kumfuata seif chadema! Kule cuf na sisiemu ni kama simba na yanga! Utahama wewe washabiki wanabaki!
 
mkuu, kama CUF wasipotafuta suluhu, inakufa safari hii, si bara si visiwani tutabakia kuisoma kwenye vitabu vya historia. Kwa sasa ishu ni kuinusuru CUF isife na wala sio kushinda uchaguzi 2020. Upinzani kwa ssa wako very disorganized hawawezi kushinda 2020. Unasema waungane wawe kitu kimoja, shida kila chama kina power mongers tena ambao ni myopic! kama kungekuwa na visionary leaders humo tungewaona wakipambana kusuluhisha mgogoro wa CUF. kama ni vyama vya upinzani kuungana, wangeshaungana toka kitambo, kwa kuwa sababu za kuungana zilikuwepo toka kitambo
Tatizo kuna watu wamenunua ugomvi sijui kwa faida ya nani.Kama wangeachwa wenyewe zanani wangekuwa wameshapatana lakini sasa kuna CUF vichwa ngumu hawaelewi wala hawana tena uzalendo ule wa wanachama kujilipia nauli mpaka Tabora toka Dar kusambaza chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri mzuri.

Kwa upande wangu nashauri Maalim Seif ahamie chadema pamoja na wabunge wake , na chadema wamuachie Maalim seif chadema upande wa visiwani ambapo ataweka wagombea wake anaowataka yaani aliotoka nao cuf.Hii itazididha uimara wa chadema na upinzani kwa ujumla.

Hasara yake Cuf itakufa.Lakini hata Maalim asipohama bado cuf itakufa tu maana sioni Lipumba akilegeza kamba wakati huo Maalim kabanwa
Hapo umenena mkuu.
Akiamia cdm maalim seif kwa zanzibar mgogoro utakwisha lakini upinzani zanzibar kwa upande wa cdm utaimarika na cuf visiwani humo itajifuta.

Kwa sheria za uchaguzi cuf ya lipumba itakuwa imekosa sifa ya kuwa chama cha siasa Tanzania kwa kuwa kitakuwa cha upande mmoja. Kwa hiyo kitajifuta au kufutwa kabisa kama shrria haitakuwa na macho maana wakati mwingine huwa inamacho na kuona huruma.

But ikiwa itatokea huvyo CDM upande wa zanzibar wamuachie huyo mzee sawa sawa kwani ni mtumwenye nguvu kubwa huko visiwani japo siasa sio kitu cha kupeana ni nguvu ya hoja basi likiwa jema ni bora liwe hivyo na mgogoro utakuwa umeisha sasa tumuone re~profesel atakuwa na lipi ktk hili.

Nimejazia nyama tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CUF acheni kutunishiana misuli, wenye hekima tushaona mnavyoenda mnaenda kubaya wote na sasa tunaona ipo haja ya kuwashauri kwa hekma ili muweze kunusurika.

Kimsingi kwa mtu yeyote ambaye ni mdau wa demokrasia, hawezi kufurahia kuona migogoro ndani ya vyama vya siasa ambayo inatishia kuviua vyama hivyo. Kwa mantiki hiyo, umefika muda sasa wa wadau wa demokrasia kuwasaidia CUF kupata suluhu ya mgogoro unaowakabili. Aidha, kwa kuwa CUF ni chama cha upinzani, vyama vingine vya upinzani vina jukumu la kuwasaidia CUF kufikia Suluhu kuliko mtu mwingine yeyote.

HATARI ILIYOPO KAMA MGOGORO HUU UTAENDELEA KAMA ULIVYO;
Ikiwa, mgogoro huu utaendelea kama ulivyo bila kusuluhishwa kwa njia za kidiplomasia, madhara ya fuatayo yanatarajiwa kujitokeza.
1. Kuzidi kwa chuki miongoni mwa wana CUF wenyewe kwa wenyewe hasa chuki kati ya wana CUF wa zanzbar/ pemba dhidi ya wale wa Bara.

2. Kuzidi kwa chuki ambayo haiwezi kuwa na faidia kwa yoyote kati ya Prof. Lipumba na Maalim.
3. Kwa upande mmoja CUF ya maalim Seif itakufa kwa kukosa uungwaji mkono wa kitaasisi na kisheria (kutokana na position ya mgogoro kwa sasa) na kwa upande mwingine CUF ya Lipumba itakufa vile vile kwa kukosa uungwaji mkono wa kutosha Zanzibar lakini pia kwa kukosa "Cause and Purpose" bara. CUF itapoteza wabunge wengi toka pande zote. Kwa hiyo wakiendelea hivi matokea yanatarajiwa kuwa "Zero sum game" kwa pande zote.

NINI CHA KUFANYA;
Kwa kuanzia,
1.Tunaziomba pande zote (Maalim na Prof. Lipumba) kwanza waache kutoleana kauli kali na za kuudhi ambazo zitaendelea kuleta uhasama.

2. Maalim aitishe vyombo vya habari akiwa pemba na kueleza wafuasi wake kuwa yuko tayari kufikia maridhiano na prof. Lipumba na Lipumba aitishe Press Dar akieleza utayari wake wa kufikia maridhiano na Maalim.

3. ACT (kwa sababu wanaweza kuaminika na pande zote), wawasaidie CUF kuwatafutia msuluhishi ambaye anaaminika na pande zote ambaye kwa haraka sana ataita wajumbe wa pande zote na kuanza hatua za maridhiano, kwa kuangalia uwezekano wa Lipumba kuendelea kuwa Mwenyekiti na Maalim kuwa Katibu kama ilivyokuwa awali.

MSULUHISHI
Napendekeza Msuluhishi awe ni Shekhe, Maalim Ally Basalleh wa dar es salaam. Hii ni kwa sababu kwa sasa kitu pekee kinachowaunganisha Lipumba na Seif ni dini, wote wanamfahamu vizuri Basalleh na wamekuwa wakiswali nyuma yake mara kwa mara. Aidha Shekhe basalleh ni msomi, mtu mzima, muelewa na mwenye busara kubwa sana.Naamini suluhu itafikiwa.

Nawatakieni suluhu njema.
Hii ni ngumu sana.
Lipumba alijitoa CUF wakati wa uchaguzi ili CUF iadhirike.
Amerudi baada ya kuona CUF haikufaa na imezidi kuneemeka.Amekuja ili aimalize kimoja na anafanikiwa kwa baraka za mhimili uliojichimbia zaidi.
 
Back
Top Bottom