Nakuunga mkono mwenyeketi, basi tukae pembeni tuangalie huku tukiendelea kulalamika, na pindi inapotokea migogoro kama uliotokea CUF tusihangaike wala kujaribu kutafuta suluhu kama walivyofanya CUF. turaruane tu hadi hapo tutakapoishia kwa kuwa mambo haya husababishwa na siasa chafu za CCM na hatuna la kufanya. Siku CCM wakiamua kuwa vyama vya upinzani viendelee, basi watavisaidia kwa kila hali ili viendelee na hata ikitokea migogoro ndani yake, wakati huo watasaidia kuisuluhisha ili upinzani uendelee na uweze kuwatoa CCM madarakani kwa kuwa ndilo lengo lake kuu. Ipo siku tutakuwa na ccm ya namna hiyo, tuendelee kusubiri na kuangalia mwenyekiti!